Mkurugenzi wa Biashara Precision Air Bw. Phil Mwakitawa akizungumza katika hafla fupi iliokutanisha shirika la ndege hiyo na wadau wake katika utangulizi wa kuzindua safari za Hahaya, Comoro na Johannesburg, Afrika Kusini. Hafla hiyo ilifanyika Southern Sun Hotel jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita. Mkurugenzi huyo alisema kwamba wako tayari kupokea ndege yao mpya aina ya Boeing 737-300 wiki hii kutoka Luton, London-Uingereza tayari kwa kuanza safari za Comoro tarehe 17 na Johannesburg tarehe 24 mwezi huu wa Agosti.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Allan Sharra (kulia) akizindua dansi baada ya kutoa hotuba yake ilyoongelea ufanisi wa ndege yao mpya aina ya Boeing 737-300 itakayofika wiki hii. Alisema ndege hiyo itaongeza idadi ya wasafiri kutoka 17,000 kwa wiki hadi kufikia 70,000 kwa wiki.
Wadau wa Precision Air wakitoa 'cheers' kwa ishara ya kuzindua safari za Hahaya na Johannesburg na kupokea ndege mpya ya Boeing 737-300.
Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Masoko wa Precision Air, Bi. Elizabeth Mungwe (Kulia) akiwa na Meneja Mauzo Bw. Prosper Lawrence na Afisa wa Mauzo Bi. Happiness Gachuma, wote kutoka The Citizen.
Mawakala mbali mbali wa usafirishaji wa anga pia walikuwepo katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Precision Air.
Naomba kufafanuliwa tofauti kati ya kitengo cha masoko na kitengo cha mauzo.
ReplyDeleteWatanzania tuna tabia ya kupotoshana sana.eti Boeing 737-300 mpya.hizi 300 series ni ndege za early 80s.Sa hivi kuna kuna 737-700 series mpaka 737-900 series ndo waweza sema ni mpya zaidi ya hapo ni kuongopeana.Prevision air walease au kununua ndege iliyotumika tayari na si mpya
ReplyDeletehttp://www.boeing.com/commercial/737family/background.html
Mie nadhani ni hii series ni mpya kwenye hii industry ya Aviation kwa hapa bongo. Ni kweli kuwa ni series ya late 80s na mara ya mwisho series kama hiyo ilitengenezwa na kuuzwa kwa Air New Zealand mwaka 1999 na Boeing hawajawahi zalisha ndege ya series hiyo. Kwa kifupi sio ndge mpya kama precious wanavyodai, Ila kwa hapa bongo ni mpya. ni sawa na tunavyooagiza mitumba ya magari hapa bongo. Ila niwapongeze Precision maana wametutoa kimasomaso.
ReplyDelete