Waziri wa miundombinu wa Serikali ya mapindizi ya Zanzibar 
Hamad Masuod Hamad
Na Hamad Hija maelezoZanzibar

Waziri wa miundombinu wa Serikali ya mapindizi ya Zanzibar Hamad Masuod Hamad, amezinduwa rasmi kamati ya chuo cha mabaharia na kamati ya usafiri wa anga ambazo zitasimamia uundwaji wa vyuo hivyo hapa zanzibar.

Halfa ya uzinduzi wa kamati hizo ambazo zitakuwa na majukumu ya kusimamia uanzishwaji wa vyuo hivyo imefanyika leo huko uwanja wa ndege wa zamani kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Akizitaja kamati hizo Waziri wa miundo mbinu na mawasiliano,Hamad Masuod Hamad amewataja watakao unda kamati ya usafiri wa anga kuwa ni pamoja na Abdulla Hussein Kombo kuwa Mwenyekiti capteein Said mligati ,Said Suri na wengineo na kwa upande wa kamati ya anga wamo capteein Ali Haji,Abdulrahman Chande, Engeneer Haji vuai Ussi pamoja na Salma Suleiman omar

Amesema kuwa wamefikiria kuanzishwa kwa vyuo hivyo kwa kuwa muda wa kufanya hivyo umefika kutokana na kuwa Zanzibar kuna mabaharia wengi,ambapo wengi wao wanafanya kazi ya ubaharia bila ya kuwa na taaluma ya fani hiyo.

Amesema kusudio la kuanzisha vyuo hivyo viwe vyuo endelevu na vyenye hadhi ya vyuo ambapo watu wengi watapata nafasi ya kujifunza hapa Zanzibar na sio viwe vyuo vya kienyeji

Aidha Masud amesisitiza kuwa, wanavyokusudia katika uanzishwaji wa kamati hizo ni kuona lengo la kuzipa uwezo wa kiutendaji hadi kuanzishwa kwa vyuo hivyo hapa Zanzibar.

Aidha amefahamisha kuwa pamoja na kuanzisha kamati hizo hivi sasa hakuna fungu la pesa ambazo zimetengwa kuendeshea lakini pesa za kuendeshea shughuli hizo zitatoka katika taasisi husika ambazo zipo.

Akitaja kazi za kamati hizo ambazo zimezinduliwa leo waziri huyo alisema kuwa miongoni mwa kazi zao ni pamoja na kuangalia kwa kina utaratibu wa kuanzisha chuo cha ubaharia hapa Zanzibar pamoja na mfumo mzima wa uendeshaji wa chuo hicho

Alisema kuwa pia kutakuwa na jukumu la kamati hizo kuangalia kwa kina soko la chuo hicho hapa zanzibar na nje ya Zanzibar pamoja na kutowa mapendekezo ju ya taratibu zitakazo tumika katika kutowa mafunzo katika chuo

Aidha alitaja kuwa kazi nyengine zitakuwa kutowa na kupendekeza mipango ya muda mrefu na muda mfupi ya kitaalamu ya uendeshaji ambapo pia kutakuwa na majukumu ya kupendekeza taratibu za kutambuliwa chuo hicho duniani.

Na kazi nyengine ambazo zimetajwa kuwa zitakuwa na jukumu kubwa la kuorodhesha wataalamu waliopo hapa Zanzibar ambao watatumika katika kuendesha mafunzo ya vitendo na nadharia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...