SALAM

URBAN PULSE CREATIVE inawaletea cinema fupi inayoitwa KARMA. Sinema hii fupi ilitengenezwa na Baraka Baraka Kutoka Urban Pulse wakati wa masomo kama assignment ya mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha DE MONTFORT hapa mjini Leicester mwaka 2007 ambapo kila mwanafunzi alitakikana kutengeneza stori yenye kueleweka chini ya dakika Nne bila kutumia maneno bali ni vitendo tu.

Maudhui ya Sinema hii yametokana na misingi ya Dini ya Kihindu yakimaanisha kwamba kila Tendo lifanywalo huwa na madhara yake. Kwa lugha nyingine inamanisha kuwa Ukianzisha balaa, balaa litakurudia hivyo ni vizuri tukawa tunafikiria mara mbili mbili kabla hatujafanya maamuzi magumu.

Asanteni,

URBAN PULSE CREATIVE
Kutoka kushoto Baraka Baraka Na Frank wa URBAN PULSE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Tusidanganyane hawa wadau bado kabisaa...kitu wanachotuonyesha hakipo kabisa kwenye hayo mazingira...Ulaya huwezi kaufanya wizi wa kipumbavu namna hii,polisi wapo kila kona na kuna wazee kazii yao kukaa madirishani na kuchungulia kinachoendelea mitaani kwao na kuripoti polisi kwa kwa kile wanachokiisi si cha kawaida..kwa kifupi hawa wanatakiwa waumize vichwa kwa kuwaburudisha wananchi kwa kile kilicho bora zaidi..tena wanabahati ya kuwa mbele lakini si elewi tatizo ni nini? sina ubaya na mtu ili ni changamoto kwao na ni vizuri mtu akueleze ukweli na ukikubaki kuupokea ukweli basi utapiga atua..Thanks.

    ReplyDelete
  2. We Anony wa 02:02:00. Ni vizuri kuwa Critical lakini wewe kazi yako iko wapi? na kama ni nzuri mbona hatuioni? watu wanaocritique ni wale walioko mbele sio nyuma. maana kama na wewe hauna maendeleo yoyote na wewe mwenyewe basi pengine ujuaji wako haukusaidii. Sikatai watu kutoa critique zao lakini wakati mwingine ni wivu umetujaa, kila mtu anajaribu dunia hii na hakuna kazi iliyo perfect, tutiane moyo na tusaidiane, kama unaona hao jamaa hawafanyi vizuri, watafute uwasaidie kwani kuandika hapa ni kutaka kuconvince na watu wengine waamini chuki uliyonayo na maendeleo ya Vijana hawa; kwa kweli haisaidii wenzako hawataacha kusonga mbele, because of your comments POLE SANA kuumiza kichwa wa maendeleo ya watu wengine.

    ReplyDelete
  3. Baraka, Ujumbe ni mzuri ila filamu haiendani na Mazingira ya UK. Mfano huwezi kumpora mtu barabarani halafu Police wasitokee kwa muda wote huo wakati jamaa wanakimbizana barabarani, labda kama mimi sijaelewa maudhui ya filamu hii! au mwisho wa picha umekatishwa. Mdau, mlp3010@gmail.com

    ReplyDelete
  4. Tabu kweli kweli, ni aibu hata kuiweka hapa hiyo video.

    ReplyDelete
  5. Jiwekeni sawa kwanza vijana, kazi zenu nyingi bado ni za upuuzi upuuzi tu, najutia hizo dakika nilizopoteza kuangalia huo upeezi wenu

    ReplyDelete
  6. Ingawa kuna mapungufu but its a good start. keep it up.

    ReplyDelete
  7. Wanatafuta majina kwa nguvu!

    ReplyDelete
  8. kazi ya sanaa ni ngumu jamani na ni lazima tuwapongeze awa jamaa kwa kazi waliyofanya. Ukiangalia lengo la sinema hii ni kutotenda mabaya kwani kwani kila mtenda mabaya basi tunaamini yatamrudia.

    watu wengi waliochangia wameangalia zaidi mtu anavyokimbizwa kwa muda mrefu bila watu wengine kusaidia lakini hii ni fasihi unatakiwa na wewe unayeangalia uumize kichwa ujue kwanini mtunzi ameamua kuweka hivi usiangalie mtu kukimbizwa kama unamuona anakimbizwa fikiria leo kwenye jamii zetu kuna watu wanafanya matukio ya ajabu kwa muda mrefu bila kukamatwa lakini kuna siku anakuja kukamatwa.

    Kwa upande wangu jamaa wamefanikiwa kuleta ujumbe kwa jamii. Tukumbuke hakuna fasihi yoyote isiyokuwa na mapungufu hata kidogo. Kingine tukumbuke hii habari ilitakiwa iwe dakika nne tu.

    Kila la heri katika kazi zenu.

    SINA

    ReplyDelete
  9. Ulipata ngapi kwenye hii assignment hapo De Montfort?

    ReplyDelete
  10. baraka let's get it realistic. hivi kweli kibaka akikupora chako utakuwa na nguvu za kumfukuza? kwanza utapigwa na shock. pili joko litakaribia kukutoka. tatu utatafuta njia ya kukimbia mwenyewe kwani hujui alokupora ana silaha gani siyo hilo nyororo la kufungia baiskeli.nne; movie bubu haina mwelekeo. nd'o mana movie zako nyingi haziendelei kwa sababu haziendani na hali halisi kijamii au matukio. nenda koleji elimu ya directorate ya filamu ipo hapo leicester koleji. kubali kukosolewa (critics) kwani ni moja ya somo. usiharabu kazi za watu nollywood wanaishi humo.

    ReplyDelete
  11. Hiyo ilikuwa katika kujifunza fani na bado naendelea kujifunza zaidi. Pia nimesikia maoni yenu wote na nita yatafakari. @ Anony 06:49:00 nilipata Distinction ndugu yangu.

    Baraka
    Urban Pulse

    ReplyDelete
  12. Mbona mumeanza kuponda kabla ya hata kuangalia nini maana ya film hii? Huyu kijana alikuwa mwaka wa kwanza ndiyo kwanza ameanza kujifunza hiyo filming. Nyinyi mumeanza kutwanga kama yeye ana uzoefu wa kutosha. Angekuwa mzoefu asingekwenda kusomea hiyo fani.

    Kwenye course moja tuliambiwa tutengeneze script ya dakika tano kuhusu mada tuliyokuwa tunasoma. Nakwambia ilikuwa kasheshe mpaka jasho la meno limetutoka tuliishia dakika moja.

    ReplyDelete
  13. Kwanza nyie wote mnasema kazi mbaya mara sijui nini hivi mmesoma mkaelewa kwamba hii ilikuwa assignment alipokuwa mwaka wa kwanza au mnacomment ilimradi mcomment? Haya basi nyie kazi zenu ziko wapi tuzione? Hebu acheni kuvunja watu mioyo.

    ReplyDelete
  14. Hongera kwa kufaulu vizuri. Na nashukuru umejibu. Nadhani utakuwa ni mmoja wa waTanzania wachache wanaosomea fani hii katika chuo kikuu nje ya nchi.

    ReplyDelete
  15. no let make it simple wewe man tunapenda drive yako unataka ktoka lakini hizo kazimbovu zote usiziweke huku mpaka utakapo mprove manake sasa unakushusha hio hadhi yako hata kama mlikua nataka kufanya kazi na wewe nitaogopa maana ni kama mimi nichukue kamera na kuanza kuchukua picha bila ujuzi wowote hata kama ulikua mwaka wa kwanza au haukwenda kabisa university, weka move zitakazokupa soko na sio huo upuuzi man unakua kama hauna kazi ulikua boadi na page ya michuzi ilikua wazi ukaamua ku apload anything kilichopo mbele yako

    ReplyDelete
  16. hata kama ulikuwa mwaka wa kwanza lakini huwezi mkimbiza mwizi kwa speed hiyo braza!!duh!!hata mtoto unadanganyi!!!
    Anyways its a good start!!

    DAvid Mun
    Manchester

    ReplyDelete
  17. Hahahah haters wakubwa nyie kama kutoka amesha toka hiyo mkubali msikubali eti asiweke huku kwani hii blog yakwenu nyie? Ankal hana ubaguzi kazi yeyote anarusha. Nyie ni chuki binafsi zimewajaa na mtabakia hivyo hivyo wenzenu wanasonga mbele. Ni hayo tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...