Habari yako Uncle Michuzi,
Tafadhali naomba uniwekee kwenye blogu ya jamii taarifa ya tatizo la umeme katika jamii ya watu wanaoishi Kigogo Luhanga karibu na Shule ya Sekondari Loyola.
Hadi wakati naandika ujumbe huu eneo husika halina umeme takriban kwa siku sita sasa. Juhudi tulizofanya ni kuwasiliana na Tanesco Magomeni kitengo cha emergency (0784 271461) wakatuambia wanafahamu tatizo letu na kuwa sababu ni hitilafu kwenye transforma katika eneo hili.
Ingawa wamekiri kufahamu tatizo hili sasa ni siku ya sita halijarekebishwa.
Tukitambua kuwa blogu ya jamii inasomwa na watu wengi tunaomba uwasilishe tatizo letu tukiamini kuwa tutasikilizwa kupitia njia hii.
Nakutakia Swaumu njema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...