CHUO cha Ustawi wa Jamii, kimeingia mikataba na wahadhiri wapya 12 ambao watashirikiana na wahadhiri 45, waliokuwepo awali kutoa elimu kwa wanafunzi
chuoni hapo.


Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mafunzo chuoni hapo Bw. Andrew Mchomvu, alisema wameamua  kuingia mikataba na wahadhiri hao ili wanafunzi waendelee na masomo baada ya kufukuza wahadhiri 21.


Alisema chuo hicho kilifungwa tangu wahadhiri 21 walipoanza mgomo wa kutoingia darasani.


“Hivi sasa tumeajiri wahadhiri 12 wenye sifa zinazotakiwa ambao watatumia muda wao wa ziada kufundisha wanafunzi wetu kwa kushirikiana na wahadhiri wengine waliopo,” alisema.


Alisema kuwa Juni mwaka huu, walilazimika kufunga chuo hicho baada ya wahadhiri 21, kufanya mgomo wa kutoingia darasani wakidai nyongeza ya mishahara, kupandishwa daraja, kuthibitishwa kazini na kutoona maendeleo ya taasisi.


“Madai yote waliyotoa hayana ukweli ndani yake, mtu anapotaka kupandishwa daraja lazima afikie vigezo, awe na shahada ya uzamivu na kuandika maandiko ambayo yatapitiwa na watu wengine na kudhibitishwa,” alisema Bw. Mchovu.
Chanzo: Majira

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...