Mengi yamesemwa sana kuhusiana na kuparanganyika kwa kundi hili na hatimaye kutokea Wenge zaidi ya sita huku mbili kubwa ya JB Mpiana na ya Werason zikionyesha upinzani wa hali ya juu.
Kuanzia wiki hii Blog yako ya Spoti na Starehe itakuwa nkiwalete Makala ya Historia Ndefu ya WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE. Ilikujua nini Hasa kilitokea baada ya kupata mwanya wa mmoja wetu kuongea na mtunzi wa kitabu cha Historia hiyo. Makal hizi zitakuwa zikikujia Kuanzia Jumatatu, Jumatano na Ijumaa ikiwa ni muendelezo, kujua kwa undani nini kilitokea na kusababisha bendi hii ya kizazi cha nne cha Musiki wa Congo kuparanganyika, ungana Spoti na Starehe kwenye masimulizi haya ya kusisimua EXCLUSIVE.
Nilibahatika kukutana na mdau mmoja mwana familia mwenzetu wa wenge ambae yeye amekwenda mbali kidogo,ameamua kuandaa kitabu maalum kwa ajili ya Clan ya wenge “THE STORY OF CLAN WENGE”,Kitabu ambacho mimi kwa mtazamo wangu nadhani kitatusaidia sana wana wenge family dunia nzima tujue nini hasa kilitokea mpaka wenge musica bcbg 4×4 Tout Terrain original kutokuwepo tena ulimwenguni na kuifunga kabisa ama kuipunguza mijadala ya malumbano baina ya wana familia wa iliyokuwa wenge musica ya ukweli.
Kitabu kitakua katika lugha mbili,kitakua mkifaransa na mkilingala lakini nimejaribu kumshawishi akiweke pia mkingereza ili watu wa afrika mashariki pia waweze kukisoma na kukielewa kwani nimemueleza kwamba pia sehemu hizo na zambia,malawi,zimbambwe ambako wanaongea zaidi english wapo wanafamilia wengi sana wenge,ameniahidi kulifanyia kazi hilo,hivyo likifanikiwa nadhani itakua ni fursa nzuri hata kwa wasiojua french au lingala kufahamu kilichojiri hasa kwa kuwa mwandishi amejitahidi sana kuzungumza na wahusika wakuu wa iliyokuwa wenge musica original kuanzia wanamuziki viongozi mpaka wanamuziki wa kawaida,mapromota mpaka maproducer na wadau wa karibu sana.
Kujua zaidi ungana na Blog yako ya Spoti na Starehe, Bofya hapa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...