Blogs katika nchi yetu ya Tanzania pamoja na sehemu nyingi duniani zimekuwa kiungo muhimu sana katika kuupasha umma habari. Alianza Michuzi kublog wakafuatia wengi na wengi wao wakiwa waandishi waliobobea na wasiobobea katika Nyanja ya habari Tanzania.
Nimesukumwa kuandika haya ya leo kutokana mwenendo wa bloggers wengi ambao kwa hakika unaelekea si tu kutukanisha taaluma ya habari, bali pia kuvunja maadili ya uandishi wa habari kwa ujumla. Blogs zina kusudi la kufikisha ujumbe kwa mtindo uleule ambao websites nyingine za habari kama cnn.combbcworld.com, ippmedia n.k zingefikisha ujumbe kwa jamii. Ni dhahiri kwamba kanuni na sheria za uandishi wa habari zinapaswa kuzingatiwa na wanablogu pia.
Tanzania tuna blogs nyingi ambazo zimepoteza mvuto hasa kwa sababu ya ama kuhamisha habari za wenzao au kuingia mikataba na wenzao ambayo inafanya zisiwe na jipya zaidi ya kuhamisha kila kitu kilichotolewa na wenzao. Imefika wakati ambao nadhani hata bloga anaweza kurusha habari za siku nzima akiwa chumbani kwake kwani teknolojia ya ‘copy & paste’ inamruhusu kufanya hivyo. Lakini ni kosa kubwa kwani wasomaji hutegemea mhabarishaji aliyejitolea kutoa habari kwa umma ajishughulishe kutafuta habari na sio kunakili mapicha na habari zilizoandikwa na bloga mwingine…. HII INABOA!
Nimeona blogs nyingi ziki post story na picha kwa namna ile ile kitu ambacho inaonyesha kabisa kwamba habari zimehamishwa tu kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Zamani wakati naripoti kwenye magazeti tulikuwa tunaelekezwa na wahariri wetu kuandika habari kutoka angle tofauti mara unapokutana na mwandishi mwenzio aliyetoka chombo unachokifanyia kazi ili msiandike habari inayofanana. Siku hizi mambo hayako hivyo, mtu mmoja anaweza kuandaa habari na kuzirusha kwenye blogs kubwa tano tofauti…NI AIBU!
Nawasihi mabloga wa bongo mjitahidi kuingia mtaani kutafuta habari na sio kukaa baa na kunakili tu habari zilizotolewa na wenzenu. Itaongeza msisimko zaidi pale utakapofungua blog ya Michuzi ukakuta ina picha ama habari tofauti na Mjengwa, au Michuzijr, au Mtaa kwa Mtaa, au Hakingowi. Na hata habari zikifanana, basi ziwe na taste tofauti. Ni dhahiri kwamba siku nyingine unakuta blogs zote zina kila kitu kinachofanana hata kama kuna typos.
Changamoto nyingine ninayopenda kuwagusia wanabloga hawa ni kuchangamkia breaking news. Kumekuwa na umaskini wa kuripoti matukio ya dharura au matukio mengine muhimu kutokana na kutohangaikia habari. Unaweza kukuta tukio lililotokea saa nane mchana linakuja kuripotiwa na magazeti kesho yake asubuhi, na hata bloga mmoja akilidaka hilo basi hiyo habari utaikuta kwenye blogs zote kwa staili ile ile ya mmoja! Na hii si sahihi kabisa maana hata sponsors wenu wanategemea kuona page zimesheheni habari na matukio yanayoendana na wakati. Hivyo nawasihi bloggers wetu mjishughulishe kupata habari.
Proofreading ama kuhakiki mnacho post ni ufa mwingine ambao si tu unakera bali pia unatia aibu kwa taaluma ya uandishi kwa ujumla. Imefikia mahali ambapo hata majina ya watu au vielelezo muhimu hukosewa bila hata mabloga hawa kusahihisha, ni jambo la aibu. Nisingetegemea kuona gazeti la mzalendo, nipashe, mwananchi nk zimetoa habari kwenye front page au kurasa nyinginezo na kukosea spelling halafu wakaendelea kwa mtindo huo bila kujirekebisha. Blogs zetu zinapaswa zifuate utaratibu wa kuzipitia na kusahihisha habari zao kabla ya kuzirusha.
Otherwise napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa kwenda na wakati, kwani bila kujitolea kwenu kuanzisha blogs tungekuwa tunapitwa na mambo mengi sana, lakini tunapaswa kupashana pale tunapoona panahitaji marekebisho ili twende sambamba na kasi ya dunia.    
Mwandishi wa kujitegemea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ni kweli kabisa hii ina BOA! tulimwambia Michuzi alipokuja hapa Marekani kwamba huu utaratibu si Mzuri hata kidogo. Utaona kwamba mara baada ya kuingia blog moja huna hamu ya kuingia blog nyingine, utakuta habari ni ile ile, yaani picha na lugha ya mwandishi wa kwanza ni ile ile imetumika. Lakini hili tatizo amelianzisha Michuzi mwenyewe alipo anzisha utamaduni wa "BLOG dada' utaona kwamba mapicha yote ya michuzi utayakuta kwenye blog za wengine wote na wao vile vile utayakuta humo kwa michuzi na hawasemi kwa Hisani ya........" kama kutoa credit.. badirikeni na huu utalatibu si mzuri hata kidogo.

    ReplyDelete
  2. Maoni yako yanakubalika kabisa. Lakini ujue si kila blog inasomwa na kila mtu. Hivyo ili habari iweze kuwafikia watu wengi kadiri iwezekanavyo, inabidi habari hiyohiyo irudiwe kwenye blog zingine. Kwani hujawahi kuona habari moja ikitangazwa na CNN, ITV, TBC1 nk? Nafikiri kutoa habari zinazofanana ni jambo la kawaida. La kuzingatia tu ni kwamba wanablog wajitahidi kuwa na habari za nyongeza ili kuifanya blog ionekane na kitu cha ziada.

    ReplyDelete
  3. Hivi ni nani huyu mwandishi wa kujitegemea ameandika hii? Maana nimeiona kwenye blogu mbalimbali kiasi kwamba nashindwa kuelewa source yake kuu ni ipi. Wekeni basi hata source.

    ReplyDelete
  4. Hongera mtoa, mada, nakubaliana na hoja yako kabisa, ni kweli kunakufanana kwa habari baina ya vyombo vya habari, lakini ni kweli lazima kuwe na tofauti ya tukio linavyoripotiwa kati ya chombo na chombo, kama ni mfuatiliaji wa makini utaona kuna tofauiti namana Al jazeera ilivyokuwa inaripoti mgogoro wa Libya ukilinganisha na cnn ,bbc na vyombo vingine. kwa kweli wana bloger wetu inabidi wawe wabunifu, watafiti na watafutaji habari. kingine kinachokera kwenye blog zetu ni tarifa binafsi za bloger mwenyewe, mara nipo kijijini, mara nipo vakesheni, mara nipo hivi nk. pia lugha inayotumika mfano mtu atakwambia eti leo ukweni kumetokea hivi, ukerewe kumetokea hivi, hizi ni lugha za mtaani na sio lugha makini kwa bloger. nina meengi lakini kwa sasa niseme hayo machache

    ReplyDelete
  5. ni kweli kabisa ukisoma michuzi hiuna haja ya kusoma jiachie, othman michuzi, mroki mroki, mjengwa, na bukuku inakera sana jamani

    ReplyDelete
  6. huyu ni mpuuuuzii unafukiri blog yako ni kila mtu anaijua?na kama swala ni kupeana habari nini lengo lako la lulalamika,kama unapewa credit shida yako nini,tatizo la bloggerz wa kitz wana roho mbaya sana...........kwahali hii tutabaki kuwa nyuma kimaendeleo tuu,tafakarii huna akili wewe

    ReplyDelete
  7. Labda nimjibu Anoy wa Sun Sep 18.06.37.00 AM 2011 kuhusiana na blogu kuwa na taarifa binafsi za mambloga wenyewe. Sidhani kama kuna tatizo hapo kama utakuwa unajua maana halisi ya blog. Blogu haina maana kuwa ni kwa ajili ya news tuu. Blogu ni kitu binafisi na zinaendeshwa na watu binafsi. Blogu sio sawa na sites za Aljazeera, BBC au CNN. Hizo ni sites specifically kwa ajili ya news.

    Blogger yenyewe ambayo ndio chanzo cha blogs nyingi ikiwepo hii ya Michuzi inasema: "A blog is a personal diary. A daily pulpit. A collaborative space. A political soapbox. A breaking-news outlet. A collection of links. Your own private thoughts. Memos to the world."

    Blogger inaendelea kusema: "Your blog is whatever you want it to be. There are millions of them, in all shapes and sizes, and there are no real rules.": http://www.blogger.com/tour_start.g

    ReplyDelete
  8. Blogging si lazima iwe News reporting. Blogger anaandika chochote ambacho anapendelea, katika topic yoyote ile, inaweza kuwa mapishi, michezo, muziki, na hata kwenye hizo, anaweza kuwa specific zaidi, mfano ndondi, au soka, au baiskeli.
    Vile vile inaweza kuwa 'analysis' ya mambo. Naweza kuwa na blog na nisiweke habari hata moja, ila nikachambua pengine mienendo ya kisiasa au chochote. Hivyo ni kweli, Blogger anaweza kushinda chumbani hata mwaka mzima na akawa na blog nzuri tu, cha msingi anachoandika kiwe na wafuatiliaji.
    Ila la waTz kukopiana habari limezidi, tunahitaji blogger wa aina tofauti zaidi ya kuripoti matukio tu.

    ReplyDelete
  9. SAFI SANA MTOA MADA HII,MIMI NI MSOMAJI MZURI WA BLOGS,NIMEKUWA NIKIKERWA SANA NINAPOKUTA HABARI ZILEZILE KWENYE BLOGS KARIBIA ZOTE.NINA KAWAIDA YA KUSOMA MICHUZI,JIACHIE,MTAA KWA MTAA,NA HAKI NGOWI.UKWELI NI KWAMBA KARIBIA KILA KITU UTAKUTA KIMEJIRUDIA ,SANA SANA TOFAUTI NI MTAA KWA MTAA ATAKAPOKUWA AMETEMBELEA IRINGA,NDO ANAWEZA KURUSHA KITU TOFAUTI KIDOGO NA WENZAKE.HII INACHOSHA NA KUMKERA MSOMAJI,TUNATAKA KUPATA VITU VIPYA SIYO KITU KILE KILE.KAMA MICHUZI ALITUMIA MTINDO HUU KUWABEBA WADOGO ZAKE ILI WAJULIKANE,BASI IMETOSHA TUMESHAWAJUA WASIMAME KWA MIGUU YAO SASA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...