Na Mdau Sunday Shomari.
Bondia wa Tanzania anayepigana ngumi za kulipwa Marekani katika uzito wa unyoya Rodgers Mtagwa (pichani) anaingia tena ulingoni kujaribu tena nafasi nyingine ya kutwaa taji la dunia. Rodgers Mtagwa safari hii anakutana na bingwa wa uzito wa unyoya wa WBC Jhonny Gonzalez katika pambano litakalofanyika huko El Paso Texas.
Jhonny mwenye rekodi ya mapambano 49 na kushinda (43 kwa njia ya KO) na kushindwa 7 atapambana na Mtagwa Alhamisi usiku katika ukumbi wa Coliseum huko El Paso Texas , bingwa huyo wa WBC amesema anafahamu fika kuwa Rodgers Mtagwa ni bondia hatari mwenye uwezo wa kuvumilia makonde lakini yuko tayari kupambana na walio bora kwenye uzito wake.
Rodgers Mtagwa mwenye rekodi ya mapambano 27, kushinda 14 (19 kwa njia ya KO) na kushindwa 2 ana bahati au tuseme ana meneja mzuri kupata tena nafasi ya kuwania mkanda wa dunia lakini si hivyo tu alijiwekea jina hapa Marekani baada ya kuonyesha uwezo mkubwa alipopambana kiume na kushindwa kwa pointi katika pambano aliloonekana wazi kuwa ameshinda dhidi ya bingwa wa WBO Juan Manuel Lopez huko Madison Square Garden New York January mwaka jana.
Baada ya hapo alipewa nafasi nyingine pale alipopambana na bingwa wa WBA wa uzito unyoya ambaye kwa sasa anaonekana hana mpinzani Yuriokis Gamboa wa Cuba ambapo Mtagwa alishindwa kwa KO katika raundi ya pili.
Pambano hilo litaonyeshwa LIVE kwenye ESPN 3 saa 2.30 usiku saa za Washington Dc.
nilikuwepo katika pambano na sasa ndo nataka lala, pambano lilikua zuri ila uwezo wa kijana wetu ulikua mdogo kulinganisha na gonzelez, amepigwa ktk round ya pili, ila naamini kijana akifanya mazoezi makali na kupata kocha mzuri atakua yishio duniani, MUNGU IBARIKI TANZANIA,Mungu mbariki mtagwa.
ReplyDeleteMambo gani tena kudundwa raundi ya pili jamani wakati unawakilisha nchi yako! Halafu siyo kudundwa tu, ni kibano haswa mpaka knockout. Siamini nimepoteza hela yangu kwenda kuangalia hii mechi. Technique ya huyu ndugu yetu ni mbovu sana--papala papala nyingi ulingoni badala ya kutulia na kumsoma vizuri mpinzani wake. Atafute kocha mwingine, la sivyo atakuwa anakuja kufanya utalii tu nchi za nje na kupata kibano mara kwa mara.
ReplyDeleteUshauri wangu wa bure kwa bwana Mtagwa: Hakikisha kila kabla haujaingia ulingoni kwenye pambano, uwe umeisoma kwa makini sana video ya mpinzani wako ili uifahamu vizuri staili yake. Kwenye hili pambano inaonekana kabisa kwamba huyu jamaa alikuwa ameshakusoma zaidi kuliko wewe ulivyomsoma yeye. Kila hatua uliyochukua, huyu jamaa alikuwa tayari ameshahisi utafanya nini. Huu mchezo unahitaji akili vile vile, siyo kurusha masumbwi tu hovyo hovyo. Ndiyo maana ulichoka na ukashindwa hata kuji-difendi vizuri raundi ya pili tu. Bongo bwana, we have a long way to go in almost every sphere. Nchi imejaa ushabiki mwingi, pride nyingi lakini we just never deliver. Inauma sana aisee.
We also have to train our athletes to seriously think on their feet and be very smart and improvising when approaching a match especially in critical situations. It begins with self-confidence and the belief that you can do it and will win in the end no matter what. Ndugu zetu wamerekani weusi huwa wanayo hii "killer instinct" lakini sisi mmmmhh. Aisee, I am very frustrated and almost ran out of words to say, kazi tunayo jamani. Mungu Ibariki Tanzania
http://www.boxingscene.com/third-shot-no-charm-jhonny-gonzalez-defends-easy--43819
ReplyDelete