Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profes Ibrahim Lipumba (kulia),akimwinua mkono kumnadi mgombea wa ubunge wa chama hicho katika jimbo la Igunga, Lucas Mahona, wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho, kwenye Uwanja wa Sokoine leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akihutubia katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika jimbo la Igunga,uliofamyika kwenye Uwanja wa Sokoine leo.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiwa na mgombea Ubunge wa chama hicho Leopold Mahona kwenye mkokoteni wa punda na katika maandamano ya wanachama kwenda katika viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho.
Profesa Lipumba akizungumza jambo na mgombea ubunge wa chama cheke katika jimbo la Igunga, Leopold Mahona.
 Moja ya malori ya Chama cha Wananchi (CUF), likiwa limebeba watu kutoka vijiji mbali mbali kuwapeleka katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za jimbo la Igunga, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoineleo.
" HATUMWAGII TINDIKALI KAMA WAO" moja wa wafuasi wa CUF akiwa na bango linalosomeka hivyo, wakati wa maandamano ya kumpokea Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye baadaye alizindua kampeni za chama hicho katika viwanja vya kumbukumbu ya Samora mjini Igunga mkoani Tabora. Wiki iliyopita mfuasi mmoja wa CCM alimwagiwa tindikali na watu wanaodaiwa kuwa wa CHADEMA.
Mlinzi wa CUF (kulia) akiwa kazini wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. nshimimana aka dumisaneSeptember 13, 2011

    huyo mlinzi vipi tena, yaani CHADEMA vazi lao la kawaida ni la kijeshi kuliko la huyo hapo? job true true.. kazi kweli kweli

    = = =
    buffalo,
    new york

    ReplyDelete
  2. Duh aisee CUF wamechoka vibaya... hawaeleweki wako upande gani.

    ReplyDelete
  3. kumwagia watu tindikali ni uchanga wa kisiasa,tunashukuru kama CUF mmeliona hilo.

    ReplyDelete
  4. Hili suala la haki za wanyama linapigiwa kelele kila siku ulimwenguni CUF haliko kwenye sera zao? au ndo kupagawa na uchaguzi

    ReplyDelete
  5. hongera CUF kwa siasa safi na za kistarabu
    waacheni hao wamwagie watu tindi kali nyie ombeni kura tu

    ReplyDelete
  6. HAWA CUF WAPO WAPO TU,KWANI HAWA SI WAMESHAFUNGA NDOA NA CCM,NANI ASIYELIJUA HILI.CUF SI CHAMA PINZANI KM TUNAVYOJUA WAO NI HEWALA TU KWA CCM,WAMEKWISHAUMBUKA SASA kdddk.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...