Kwa mashirikiano ya pamoja ya wanafunzi wa Tanzania wanaosoma vyuo mbali mbali nchini Malaysia, kufuatia ajali ya kuzama kwa meli siku ya tarehe 10/9/2011 iliyosababisha vifo vya watu wanaofikia zaidi 240. 

Siku ya IJUMAA tarehe 16 Sept. 2011 patakuwa na swala ya ghaibu (Swala ya Maiti) itakayoswaliwa mara tuu baada ya swala ya Ijumaa kwenye msikiti mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Kimataifa (International Isalmic University Malaysia) campus ya Gombak. 

Swala hiyo itafuatiliwa na kisomo cha Qur'ani kwa ajili ya kuwaombea dua ndugu hao waliofariki. Tunaomba taarifa hii wafkishiwe wanafunzi wote wa Tanzania wanaosoma Malaysia.

Tunategemea mashirikiano makubwa katika mkusanyiko huu wenye nia ya kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja katika kuwaombea marehemu wote.

Kwa wale ambao hawajawahi kufika campus ya IIUM Gombak unaweza kupanda basi nambari 91 kutoka KOTA RAYA au shuka LRT Rapid KL kituo cha Gombak kisha chukua basi nambari 231 au ulizia kupitia nambari ya simu 0173416793.

Ahsante

Kwa niaba ya kamati ya muda ya maandalizi.

IIUM, Gombak

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...