Jumuiya ya waTanzania waishio New York,New Jersey,Connecticut na Pennsylvania ikishirikiana na Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York,unawataarifu Watanzania wote waishio katika maeneo hayo na ya jirani kuhudhuria katika ibada hii ya kuwaombea marehemu,majeruhi na wale wote waliopoteza ndugu,marafiki ama majirani zao katika msiba huo.


Msiba huu ni wa taifa hivyo jumuiya inasisitiza kila mwenye nafasi ya kuhudhuria dua hii afanye hivyo ili tuonyeshe umoja wetu.


Ili kufanikisha shughuli hii jumuiya inawaomba wale wote watakaoweza kusaidia kuleta chakula ama vinjwaji kuwasiliana na viongozi wa jumuiya ili wapate mwongozo wa kufanikisha hilo.


Vile vile jumuiya itatayarisha kitabu cha maombolezo ya msiba huu kwa wale watakaotaka kuchangia pesa kwa waathirika wa ajali hii.Dua itaanza saa nane(2:00PM) tafadhalini tuheshimu muda na mahali ni Mount Vernon,makazi ya zamani ya balozi anwani itafuatia.


30 OVERHILL ROAD
MOUNT VERNON,NY,10552


KWA MASWALI WASILIANA NA,
VINCENT MUGHWAI ;2407525404
SHABANI MSEBA :3477128539
MIRIAM ABU :9143162814
MAMA KISWAGA :2018507197
MASOUDI MAFTAH :6465004637


HAJJI KHAMIS
CHAIRMAN
NEW YORK TANZANIAN COMMUNITY

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mbona hakuna tarehe? Saa 8 ya siku gani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...