Na Nafisa Madai Habari Maelezo.Zanzibar
Jahazi ijulikanayo kwa jina la Asaa Robo yenye namba za usajili 328 iliyokuwa ikitokea Tanga kuelekea Wete Pemba imezama leo asubuhi nje kidogo ya Bandari ya Tanga.
Jahazi hiyo iliyokuwa na wafanyakazi tisa akiwemo Nahodha wote wameokolewa na Boti ya kijeshi ya Tanzania Bara iliyokuwa ikipiga doria kwa kazi zake za kawaida.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo baada ya kuwasiliana na kamanda wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Yahya Rashid Bugi , Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Gavu amesema kuwa, jahazi hiyo ilichukuwa mizigo ya vyakula na magodoro ambayo inamilikiwa na Mkubwa Omari Saleh.
Amesema kuwa kuzama kwa jahazi hiyo ni kutokana na kugonga mwamba na baadae kutoboka hali ambayo ilisababisha kujaa maji na baadae kuzama.
Aidha alivitaka vyombo vyote vya baharini kwa ujumla kuwa makini katika kupakia mizigo yao na kuhakikisha kuwa mizigo wanayochukua inalingana na uwezo wa vyombo vyao.
Naibu Waziri huyo alisema, ni vyema vyombo hivyo kuzingatia sheria na kanuni ili kuepusha kutokea ajali za mara kwa mara , ambazo zinaweza kuepukika ikiwa sheria zitafuatwa.
Gavu amewataja walionusurika katika ajali hiyo ni pamoja na Nahodha wa Jahazi hiyo, Issa Sharifu Issa , Mabaharia ni Hussein Saleh Omar, Ali Rashidi Ali, Ahmed Bakari Saleh, Ali Bakari Saleh, Hamad Rashid Ali na Abrahmani Bakari Othman.
Wengine ni Khamis Hamad Seif na Ali Sharif Ali ambao wote hivi sasa wamehifadhiwa katika Gati kongwe ya kiwanda cha mbolea Tanga na hali zao zinaendelea vizuri.
Kutokana na ajali hiyo Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano imelazimika kuitisha kikao kati yao na wamiliki wa majahazi siku ya jumatatu, kwa lengo la kuweka mikakati na kudhibiti hali kama hiyo isitokee.
Mapema leo Boti ya Seabus 1 ikitokea Pemba kuja Unguja ilishindwa kuendelea na safari yake , kutokana na hitilafu ya mashine na kulazimika kurejea Bandari ya Mkoani.
Wakati huo huo Boti ya Seastar hapo jana iliyokuwa ikitokea Zanzibar kuelekea Dar-es Salaam nayo ililazimika kukatisha safari yake,mara tu baada ya kufika katika kisiwa kidogo cha Chumbe , na kurejea Bandarini Malindi Zanzibar kutokana na hitilafu ya mashine kuzima kutokana na mafuta kuingia maji.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...