JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Emmanuel John Nchimbi (Mb) amemteua Bw. Dionis Malinzi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Aidha pia amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa.

Mhe. Jenister Mhagama (Mb)
Mhe. Mkiwa A. Kimwanga (Mb)
Bw. Jamal Rwambow
Bw. Venance Mwamoto
Bw. Juma Pinto
Dkt. Cyprian Maro
Bw. Kanali Eliot Makafu
Bibi Jeniffer Mmasi
Bw. Ramadhani Dau
Bw. Alex Mgongolwa
Bw. Maulid Kitenge

Wengine ni Wajumbe wa kuteuliwa kutokana na nafasi zao:

Mkurugenzi Mkuu - Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Kamishna wa Elimu - Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Mwakilishi - TAMISEMI
Mkurugenzi wa Michezo – Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Mwakilishi - Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Wajumbe kutoka Wawakilishi wa Vyama vya Michezo (Makatibu) ni:

CHANETA - Chama cha Netiboli Tanzania
TPC - Tanzania Paralympic Committee
AAT - Automobile Association of Tanzania
TSA - Tanzania Swimming Association
BFT - Boxing Federation of Tanzania
RT - Riadha Tanzania
TFF - Tanzania Football Federation
TBF - Tanzania Basketball Federation
TOC - Tanzania Olympic Committee
TTTA - Tanzania Table Tennis Association

Uteuzi huu umefanywa kwa kuzingatia Mamlaka ya Waziri chini ya kifungu cha 3(2) cha nyongeza ya Katiba ya Sheria ya BMT Na. 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake katika Sheria Na. 6 ya mwaka 1971.

Wajumbe hao watalitumikia Baraza kwa kipindi cha miaka mitatu.


Imetolewa na Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo
22.09.2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hii inaonyesha jinsi Tanzania tutakavyoendelea kuwa wababaishaji katika suala la michezo...hivi ukizungumzia michezo tu..basi una sifa za kuwa kiongozi? Marehemu Said Mziray(RIP) aliwahi kusema masuala ya michezo Tanzania yanachukuliwa kimchezo mchezo na ndilo hili..kati ya wajumbe walioteuliwa mimi sioni umuhimu wa baadhi yao, ambao kwa hakika wamechaguliwa kwa umaarufu wa majina yao zaidi, kuliko mchango wao kwa masuala ya ufundi na ufahamu wa michezo.. kwa mtaji huu, nami siku moja nitakuwa Waziri tu.......

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana mlochaguliwa, Duh! kumbe Dau na kwenye michezo yumo!

    ReplyDelete
  3. Haya ndio mambo yanayishinda kuelewa na watu wakilalamika tunaambiwa tuko sensitive. Hivi kila kitu lazima tu apply theories za birds and ponds?

    Whats so difficult Dr Ramadhani Dau akaitwa kwa cheo chake? Huyo mwingine mbona mmemwita kwa cheo chake ? halafu hawa BMT inasemekana hata vikao huwa hawakai wala kuitisha.

    Halafu mbona hatujapewa hizo profile za hao wajumbe ? seriously, mtu kama Jestina Mhagama ana sifagani ya kuwa mle? ana contributions zipi?

    Nadhani its about time Nchimbi & Co wakawa wazi kuhusu haya mambo na kutuhabarisha the ins and outs za huu uteuzi wa akina Pinto na wenzie.

    -WIMBI LA MBELE

    ReplyDelete
  4. Nina hasira sana na baadhi ya hawa watendaji wa Tanzania, kweli katika TANZANIA- hii ndio Cream bora kabisa ya kuendeleza michezo?
    Hii ni kulipana fadhila na kulindana kwa kupeana majukumu ambayo yanalenga kukiritimba maamuzi na kupeana majukumu ya kujijengea majina. Tanzania hatutaweza kufanya vizuri katika michezo tukiamini waongeleaji masuala ya michezo wanafaa kuwa watendaji kwenye masuala ya michezo..Juma Nkamia awe Waziri wa mivhezo, Charles Hillary awe katibu Mkuu wizara hiyo, Dr Riki Abdalah awe mkurugenzi wa michezo..maana hawa wote wanaizungumzia soka kwa ufasaha sana...Pole Tanzania!!!

    ReplyDelete
  5. mdau wa kwanza, marehemu alitwa Sylasaid Mziray(mwanangu) (RIP)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...