Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idi akizindua kitabu cha Ripoti ya ukatili dhidi ya Watoto Zanzibar,katika ukumbi wa Salama Holl Bwawani Zanzibar.
Makamo wapili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akionyesha kitabu cha ripoti ya Ukatili dhidi ya Watoto wa Zanzibar,katika ukumbi wa Salama Holl Bwawani Zanzibar
 Mtoto mwisi juma pamoja na Ahmed wakisoma utenzi wenye maudhui ya kukataza unyanyasaji wa kijinsia katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha ripoti ya Ukatili dhidi ya Watoto Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idi akibadilishana mawazo na Muwakilishi wa UNICEF Bi Dorothy Rozga katika hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Ripoti ya ukatili dhidi ya Watoto wa Zanzibar,hafla iliofanyika katika ukumbi wa Bwawani  Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Makamo= kipimo hasa cha urefu wa kiumbe kilicho hai.
    Makamu= mtu mwenye madaraka ya kumsaidia kikamilifu mwengine aliyepewa madaraka kamili.
    k.m MAKAMU wa Rais.

    Waandishi kumbukeni kuwa mnasomwa na wengi, mnapo potesha matumizi ya neno, basi mjue kuna wasiofahamu na watalifuata kulitumia kama muandikavyo. Ina athari ya kutokomeza utumiaji sahihi wa lugha yetu hii safi na nzuri.
    Kueweni makini kidogo.

    ReplyDelete
  2. Ndugu Michuzi ninaomba kama kuna mweledi wa masuala ya ukatili dhidi ya watoto anitoe tongotongo (na tuweke siasa kando): nimekuwa nikisoma na kusikia katika ripoti kama hizi kuhusu mazingira ya shuleni kwamba watoto kuadhibiwa kwa kuchapwa viboko ni aina mojawapo ya ukatili dhidi ya watoto. Hapo sina ubishi. Swali, je watoto kukalishwa kwenye mawe na sakafuni darasani wakipinda migongo wakati wa kusoma nao ni ukatili dhidi ya watoto? Na kama jibu ni ndio nani mhalifu - wazazi au serikali (ya kijiji, kata, wilaya, mkoa, kuu)inayoruhusu darasa au shule kuendesha shughuli zake bila kuwa na madawati? Je hivi vitabu vya ripoti tunazooneshwa zikizinduliwa kwa mbwembwe zinabainishaje suala la shule kuruhusiwa kupokea watota ilihali hazina madawati! Ninatanguliza shukrani kwa atakayeweza kunitoa tongotongo!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...