Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi-Zanzibar

ZANZIBAR ALHAMIS SEPTEMBER 15, 2011. Jeshi la Polisi nchini limeanza juhudi za kumtafuta kapteni wa meli ya MV Spice Islander iliyozama Baharini katika eneo la Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja usiku wa kuamkia Jumamosi September 10, 2011.

Taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa na Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa, imemtaja Kapteni wa Meli hiyo kuwa ni Said Abdalla Kinyanyite, ambaye ni mkaazi wa Nzasa Mbagala charambe wilaya ya Temeke jijini Dares Salaam.

Kamishna Mussa amesema kuwa Kapteni wa Meli hiyo, ambaye hakuweza kupatikana mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo , ni mwenyeji wa Kijiji cha Mbwemkuru tarafa ya Pande katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

Kamishna Mussa amewaomba wananchi kupitia mpango wa Polisi jamuii na Ulinzi Shirikishi kutoa taarifa katika Kituo chochote cha Polisi endapo watapata taarifa za mahali alipojificha Kapteni huyo ili akatoe maelezo kuhusiana na jinsi ajali hiyo ilivyotokea.

Taarifa hiyo inasema kuwa tangu kuzama kwa Meli ya MV Spice Islander, Kapteni wa Meli hiyo hakuweza kupatikana hali ambayo iliyowalazimu Polisi kutafuta Picha yake kwa lengo la kurahisisha utambuzi kwa watu wasiomfahamu pindi wamuonapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. wanamtafuta kapten wa nini kwani yeye nde aliyesababisha meli kuzama au ni wakata ticket na mafundi wa meli? wawakabe hao mafundi na wakata ticket na owner wa meli

    ReplyDelete
  2. ASANTE SANA KWATAARIFA HII LAKINI TUNAOMBA PICHA ILI IWE NI RAHISI KUMFAHAMU PALE ATAKAPOKUWA.

    ReplyDelete
  3. Kapteni amekimbilia Ugiriki sasa na tayari ameshajiandikisha kwa agency za kuwatafutia mabaharia kazi kwenye meli!!!

    ReplyDelete
  4. kwani vipi...wanadhani alipindisha meli katika kona spidi 120 ikapinduka? siasa zinatafuta mchawi wa kuokwa moto hapa, na sio kutatua tatizo pana linalojionesha...fanyeni kuwajibika kikweliii!

    ReplyDelete
  5. Watu wengi inabidi wawajibishwe na hili janga; mara ya mwisho hii meli ilifanyiwa ukaguzi lini, kuna log book ya shughuli zote za ufundi katika meli hii? Hapo kuna watu wa kujibu. Pili ni nani alitoa kibali kuiruhusu iondoke siku ya tukio na uzito zaidi ya uwezo wake - naangalia hapa kuna watu si chini ya kumi wajieleze!

    ReplyDelete
  6. atlast,kitu kinafanyika..nyie ni hamjui tu lakini Captain,hawi captain hivi hivi,anasoma na anapewa cheti,anaduties na responsibilities kwenye meli yake,sawa he does not own the ship lakini as long as anaiendesha yeye ni yake..ni almost kama pilot tu!ni responsibility na duty yake kujua meli inatakiwa iwe na kiwango gani cha mizigo,na isizidi namba ya watu wangapi,na ni duty yake pia akiona imezidi kupunguza,kwa sababu anajua what will happen,kwa hiyo captain lazima atafutwe and be hold accountable pia for his negligence kwa kweli,yote hii kisa hela,ajali ya majini jamani sio kama zingine,ukishashindwa ni unajiachia,yani unajua kabisa kwamba ndio nakufa,yani unajiona,its not right kabisa

    ReplyDelete
  7. kapten si wakulaumiwa hata kidogo istoshe alitoa taarifa mapema kwamba hali si nzuri kama wanajali mbona wasifike kwa wakati? wawaulize hao owners suala zima la ajali coz watakuwa wanajua chanzo.

    ReplyDelete
  8. hahahahaaaaa elimu bwana nchi hii elimu yetu bado
    sasa meli imjaa kupita kiasi, Kapten yupo katika ajira \\

    yeye anang'oa nanga tu unataka apoteze ajira yake kwa kuacha kung'oa nanga?
    hebu muacheni huyo kapteni Nunueni meli nzuri za serikali na mdhibiti watu na mizigo msikwepe majukumu. Na nyie polisi acheni kupoteza mawazo ya wananchi kwani hamjui kuwa chanzo cha ajali ni kujpakia kupita kiasi?
    wewe kamanda angalia sana bwana toa amri serikali inunue meri mpya bwana. kwani ile ndege na rada tukiviuza hatupati meri kweri?

    ReplyDelete
  9. ndege, meli, basi(gari), vinapokuwa safarini vinakuwa chini ya maamuzi ya nahodha au dereva kwa 100%, kama chombo kiondoke au kisiondoke, kiongeze abiria, mizigo au kipunguze, kufuatana na taaluma na ujuzi wake. ni muhimu nahodha akapatikana ili kupata maelezo yake kitaalamu kama kuna sababu nyingine mbali na overladding iliyochangia ajali ile, ili itolewe kwa meli nyingine kama tahadhali kwamba mbali na overladding pia sababu hiyo iangaliwe ili kuepusha ajali ya kupinduka na kuzama kwa meli.
    The Brain

    ReplyDelete
  10. Hivi mbona hunielewi wewe??? Mara ngapi nikuambie hii picha sio halali??? Bora uweke picha ya meli kabla haijazama kuliko picha ya meli iliyozama ambayo sio hata meli yenyewe kama hapo juu!!?
    Unaboa sasa Michuzi na hii usiibanie.
    Mdau Ugirki.

    ReplyDelete
  11. hawa mafundi wa hii meli walikuwa mafundi wa mv bukoba?

    ReplyDelete
  12. Acheni kupoteza muda na fedha za Watanzania! Ina maana hamuwaamini maelezo ya hao walionusurika ni jinsi gani ajali ilitokea? Huyo Nahodha anapaswa kulipwa fidia kwa kupewa meli mbovu na kwa kujaziwa kinyemela abiria na mizigo kupita uwezo wa meli! Kamateni mmiliki, aliyetoa kibali cha meli mbovu kuruhusiwa kufanya kazi na waliojaza mizigo na abiria bila kufuata utaratibu!

    ReplyDelete
  13. Kumtafuta kapten pekee haitoshi ingawa anakosa sana kuindoa meli wakati akijua imejaa sana kwanini asikatae kuindoa pale bandarini na kuripoti katika vyombo husika. Lakini ni vyema wakamatwe pia waliokatisha ticket,walinzi,mmiliki wa hiyo meli maana vyombo vya habari vilisema kuwa aliambiwa kuwa meli yake imejaa kupita kiasi lakini bado aliiruhusu meli iondoke hivyo hivyo. Mimi kwa upande wangu ndio angekuwa wa kwanza kukamatwa maana alijali pesa kuliko usalama wa maisha ya watu.Wengine ni maofisa wa SUMATRA wa Zanzibar ini maana hawakuwepo wakati meli inaondoka, nao wakamatwe na kufungwa. Vile vile Wizara husika haiko makini katika utendaji kazi yake katika masuala ya usafiri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...