Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) akieleza nafasi ya Bunge katika Maswala ya Mambo ya Nje kwa Mwenyekiti wa Kamati ya mambo ya Nje kutoka Bunge la Norway Mhe. Ine Marie Erikson (Mb) mara baada ya kamati hiyo kutoka Finland kutembela Bunge la Tanzania kwa ziara ya kubadilishana uzoefu.
Ujumbe wa kamati ya Mambo ya Nje kutoka Bunge la Finland ukiwa katika kikao cha pamoja na wabunge wa Tanzania kubadilishana uzoefu kuhusu uendeshaji wa shughuli za kamati hususani katika maswala ya uhusiano wa kimataifa. Kamati hiyo kutoka Norway ilikutana na Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge na wabunge kutoka kamati nyingine.
Ujumbe wa kamati ya Mambo ya Nje kutoka Bunge la Norway ukiwa katika kikao cha pamoja na wabunge wa Tanzania kubadilishana uzoefu kuhusu uendeshaji wa shughuli za kamati hususani katika maswala ya uhusiano wa kimataifa.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao na Kamati ya mambo ya Nje kutoka Bunge la Norway iliyofanya ziara katika Bunge la Tanzania kwa lengo la Kubadilishana uzoefu
Wajumbe wa kamati ya mambo ya nje kutoka Norway wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) pamoja na baadhi ya wabunge wa Bunge letu.
Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...