Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo wakati akitangaza udhamini wa tamasha kubwa la bia ambalo ni la kwanza kufanyika nchini Tanzania litakalofanyika katika Viwanja vya Leaders club Octoba 1 na 2 mwaka huu.kulia ni Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania,Dorris Malulu.
Mratibu wa Matukio wa Kampuni ya Bongo 5 Media, Olive Nimaga akitoa shukrani zake kwa Kampuni ya Bia Tanzani kupitia bia yake ya Kilimanjaro kwa kudhamini Tamasha hilo kubwa.Kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe.

Kilimanjaro Premium Lager ikishirikiana na Kampuni ya Bongo 5, Alliance Francaise na Taasisi ya Goethe wameandaa tamasha kubwa la bia la kwanza Tanzania ambalo litafanyika katika Viwanja vya Leaders Octoba 1 na 2 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Bw. George Kavishe alisema tamasha hili litakalojulikana na Kilimanjaro Beer Festival, litakuwa la kwanza na la aina yake kuwahi kufanyika Tanzania na yenye madhumuni ya kusherekea miaka 50 ya Uhuru na kuwaleta Watanzania pamoja.

Alisema tamasha hilo litapambwa na burudani mbalimbali wakiwemo wasanii wa ndani na wa nje.bendi zetu kongwe za hapa nchini, Pia kutakuwa na sehemu za vyakula, vinywaji, zawadi na michezo mbalimbali.kwa kila rika

Miongoni mwa waalikwa ni wasanii mbalimbali wa Bongo Movies ambao Bw. Kavishe alisema watajichanganya na watu na kubadilishana mawazo nao.

“Kutakuwa na ulinzi wa kutosha kutoka kwa mabaunsa wetu na walinzi kutoka kwa kampuni maarufu ya huduma hiyo,” alisema.

Alisema tamasha hilo litaanza saa nne kamili asubuhi siku zote mbili hadi usiku na kwamba tiketi zitauzwa Tsh 10,000 kwa siku zote mbili na Tsh 7,000 kwa siku moja.

Aliwaasa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ili waburudike na kujivunia mafanikio yao baada ya miaka 50 ya Uhuru.

Kwa upande wake, Mratibu wa Matukio, Olive Nimaga aliishukuru TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa jitihada zake za kuwatambua na kuwathamini wateja wake kwa kukukubali kudhamini tamasha hilo la aina yake.

“Tunawahakikishia mazingira mazuri na salama wakati wa tamasha hili kwani itakuwa wikiendi yenye burudani mbalimbali,” alisema.

Alisema baadhi ya wasanii watakaotoa burudani ni pamoja na Linah, Linex, Chidi Benz, Godzilla, Offside Trick, Akudo Impact, Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wengineo. “Kutakuwa na nyamachoma na vyakula vingine vya aina mbalimbali,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Welcome to the "Dar es Salaam-October Beer festival"....ni ndugu yake na ile October festival ya Ujerumani..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...