WASANII wa kundi la muziki wa miondoko ya Salsa Mutati, wameahidi kutoa burudani ya aina yake katika tafrija ya hisani ya Shear Charity Ball 2011.


Kiongozi wa kundi hilo, Yassin Mutati, anasema wamekuja nchini mahsusi kwa lengo la kuburudisha tafrija hiyo ya Shear , hivyo wageni na watu mashuhuri watakao hudhuria hafla hiyo itakayofanyika Oktoba mosi katika hoteli ya Movenpick Dar es Salaam, watarajie kupata burudani ya aina yake.


Anawataja wasanii wengine wa kundi hilo kuwa ni pamoja na Triza Wanjeri Alice Kang’ara na Daniel Mutema.
wanamuziki na wanenguaji wa Kundi la Mutati kutoka nchini Kenya waliwasili nchini Jumatano mahsusi kwa ajili ya kutia nakshi usiku wa tafrija ya Shear Charity Ball.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Shear Illusions, Shekha Nasser, anatoa shukrani kwa vyombo vya habari, wadhamini wakuu ambao ni Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na wengine waliochangia mafanikio ya Shear Charity Ball 2011.


Anawataja wadhamini wengine kuwa ni pamoja na Kampuni Mama ya Bilicanas Group yenye Kampuni Tanzu za Free Media Limited ambao ni wazalishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Aishi Protea Hotels, Club Bilicanas na Much More Club.


Wengine ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Kampuni ya kimataifa ya ulinzi ya Group 4, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Fly 540.


Pamoja na Maxcom, Precision Air, Desktop Production (DTP), Peacock Hotel, Clouds Media Group, kampuni ya vifaa vya ujenzi ya SS Concrete, Benki ya Azania, Benchmark Production, Advertising Dar, SBC Tanzania (Pepsi), Tanzania House of Talent (THT), I-View Media, mafuta ya kulainisha ngozi – Coconat, duka la nguo la Tina Maria, Kampuni ya kupamba ya Hugo Domingo, Imaging Smart na AIESEC.


Nasser aliongeza kwa kusema kuwa mara baada ya kufanyika kwa tafrija hiyo kutakuwa na ‘After Party’ itakayofanyika kwenye ukumbi wa Much More uliopo ndani ya Club Bilicanas Dar es Salaam.


Nasser anaongeza kwa kusema kuwa usiku huo ni maalumu kwa ajili ya kuchangisha fedha zitakazopelekwa katika huduma za kijamii ambazo ni kuchangia upasuaji utakaofanyika katika hospitali ya CCBRT Dar es Salaam kwa kina mama wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula,huku fedha zingine zitapelekwa katika ukarabati wa mfumo wa maji safi na taka katika Hospitali ya Amana.


“Lengo letu la mwaka huu ni kuchangisha fedha kiasi cha sh mil. 50 ili kuweza kufikia lengo hilo,” anasema Nasser.


Tafrija hii inafanyika kwa mara ya pili sasa ambapo kwa mara ya kwanza ilifanyika kwenye Hoteli ya Double Tree iliyopo Masaki, jijini Dar es Salaam, na kiasi cha sh mil. 15 zilichangishwa na kupelekwa CCBRT ili kuchangia matibabu ya upasuaji kwa kina mama wenye kusumbuliwa na fistula pia kuchangia nyumba ya kulea watoto yatima (SOS).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...