Zoezi la kuopoa miili ya watu walionasa kwenye mabaki ya Meli ya MV Spice Islander lililokuwa likifanywa kwa pamoja na Wazamiaji kutoka nchini Afrika ya Kusini na Majeshi ya Ulinzi na Usalama hapa chini limeshindikana.


Afisa Habari wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, ameiambia Globu ya Jamii usiku huu kwamba kushindikana kwa zoezi hilo kunatokana na hali mbaya ya bahari na kina kilichozama meli hiyo tofauti na uwezo wa wazamiaji kutoka nchini Afrika ya Kusini.

Inspekta Mhina amesema kuwa uamuzi wa kusitisha zoezi hilo umetangazwa na Kamanda wa Operesheni hiyo kutoka nchini Afrika ya Kusini Bw. Wayne Combrink, ambapo amesema, wazamiaji wake na wale wa hapa nchini wameshindwa kuifikia meli hiyo baada ya kubaini kuwa ilikuwa umbali wa kina cha zaidi ya mita 300 chini ya Bahari. Uwezo wa Wazamiaji hao ni kuzamia kina kisichozidi mita 54 tu.
Kwa hiyo kutokana na hali hiyo, Kamanda huiyo amesema wameagiza meli maalum ya Sub Marine kutoka nchini Afrika ya Kusini ili kuja kukamilisha zoezi hilo ambalo amesema lisingewezekana kutekelezwa kwa wazamiaji wenye zana za kawaida pasipo kuwepo kwa chombo hicho.
Wazamiaji hao kutoka nchini Afarika ya Kusini waliwasili Zanzibar usiku wa Septemba 13 wakiwa katika kundi la watu 16 wakiwemo madaktari wanne pamoja na vifaa vya kisasa wakidhani kina kilichozama meli hiyo kingekuwa chini ya mita 54.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ni vizuri wamejaribu na kufanya maamuzi ya ziada ndani ya muda muafaka. Kila la kheri!

    ReplyDelete
  2. Nilichojifunza hapa ni kwamba inapotokea ajali wakati nchi nyingine zinapojitokeza kutoa msaada wa wazamiaji kama ilivyofanya Africa ya kusini ni vizuri kuwapa hali halisi la eneo husika ikiwa ni pamoja na kina ambacho meli imezama, sio lazima kina halisi lakini hata kwa makadirio. Nina imani mamlaka zinazohusika zinajua kina cha maeneo ambayo meli zinapita huenda wangefanya hivyo hawa jamaa wa africa kusini wangekuja na zana za ktosha. All in all, tunawashukuru Africa kusini kwa juhudi walizoonyesha

    ReplyDelete
  3. wahusika au wazamiaji wa kwetu walishindwa kupima kina cha maji hayo meli ilipoishia ili waweze kutoa kipimo hicho kwa hao wasauzi kabla hawajafika ili wajue ni jinsi gani ya kujiandaa na uokoaji huo??

    kila la kheri.

    ReplyDelete
  4. Kina cha bahari kuwa mita 54 tu? acheni usanii jamani.

    ReplyDelete
  5. Tumejifunza sana ila sidhani kama ni watekelezaji wa mafuzo tuliyoyapata kwa ajili ya baadae.Sio mara ya kwanza kwa ajali kama hii kutokea Tanzania na kwa mara ya mwisho ajali kubwa sana ya kutisha ni ile iliyotokea Lake Victoria miaka 15 iliyopita kwa kuzama kwa MV Bukoba ikiwa inafanana kimaumbile na hata namna ajali ilivyotoke na hii ya Spice Islander ya Zanzibar.

    Wapingambizi majini kutoka huko huko Afrika ya kusini na pengine ni hawawa waliopelekwa Zanzibar kwa kazi sawa na ile ya Bukoba ya kuopoa mabaki ya ndugu zetu na kutoa maelekezo muafaka juu ya usalama wa usafiri majini. Ila sisi ni wepesi wa kusahau , leo inakuaje kuleta wataalamu hao na kushindwa kuwapa hata tathmini ya makisio ya eneo lilozama meli, jee ninamna gani wameshirikishwa wenyeji wa bahari kama wavuvi na taasisi za mambo ya elimu ya bahari za Tanzania.?

    Hata hivyo tuwashukuru wote kwa kazi kubwa na jitihada zao M/Mungu awabariki wote "Amin"

    ReplyDelete
  6. Pia wangeingia kwenye google wange pata kina cha maji sehemu hiyo kabla ya kuleta wazamiaji hao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...