Salam,
Shikamoo wakubwa na vijana wenzetu mambo vipi? kwanza kabisa tunapenda kuwashukuru Mabloga wote popote Duniani kwa kuendelea kutusaidia kwa kiasi kikubwa sana kutufikishia ujumbe wetu pale tunapo omba kusaidiwa, Baada ya shukrani hizo za kipekee kabisa.

Pia tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wale wanavyuo,watumishi wa vyuo na wadau wote ambao wameendelea kuipa sapoti kubwa website ya MATUKIO NA WANAVYUO. Ili kuendeleza kuwaunganisha wanavyuo wote Tanzania na kuwakutanisha na wanavyuo wengine ambao ni watanzania lakini wanasoma nje ya nchi tumeamua sasa kuwaletea njia mbadala ambayo itawaunganisha kirahisi kabisa nayo ni Socilal network. Hivyo basi kwa heshima na taadhima tunapenda kuwatambulisha kwenu kiunganishi kipya kabisa ambacho kinakwenda kwa jina la UNIVERSITIES CONNECTS.

Katika website hii maalum kabisa wanavyuo na wanafunzi mbalimbali pamoja na wadau wataweza kukutana humo, kubadirishana mawazo ya kisomi zaidi na kufahamiana zaidi ikiwa ni pamoja na kupata mawazo mapya, pia wataweza kupata marafiki wapya na kama haitoshi kuna Visual Discussion Room ambapo wataweza weka Mada mbali mbali na kuijadili moja kwa moja, na zaidi ya yote utapata nafasi ya kuchati muda wowote.

Pia kwa kuzingatia kuwa wanafunzi wengi wanatumia Mobile phones, basi kupitia Mtandao huu utaweza pia kutumia simu yako ya mkononi kuendelea kuwasiliana. Ni matumaini yetu ya kwamba mtandao huu wa kipekee na mpya kabisa utaenda kukuunganisha wewe na mwenzako... Tunaomba ukipata taarifa hii umwambie na mwenzako pia ajiunge ni Bure kabisa. Tunatanguliza Shukrani zetu asanteni sana.

Sisi,
Matukio na wanavyuo Crew
twanavyuo@live.com

ILI KUJIUNGA MOJA KWA MOJA BOFYA HAPA CHINI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Michuzi, hebu waambie hawa jamaa wa-edit kidogo. It is not YOUR THE FUTURE, it is YOU ARE THE FUTURE.

    ReplyDelete
  2. It shouldn't be "We Connect you Because we know your the future" it is supposed to be "We Connect you Because we know you're the future" or
    "We Connect you Because we know you are the future"

    ReplyDelete
  3. Mdau nafikiri ungeita "UNIVERSITIES CONNECT"....badala ya "UNIVERSITIES CONNECTS"...revisit your English notes...

    ReplyDelete
  4. Kazi nzuri wanazuoni,
    Bila shaka ni itilafu ya haraka ya uchapaji ktk jedwali la mwisho kulia...kuhusu sentensi ya makaribisho: "(Your Here)please......" au kama ni ujenzi mpya wa lugha basi kun'radhi nabaki mtiifu kurekebishwa.

    MAINA A. OWINO.

    ReplyDelete
  5. Hata vipofu wana kiongozi wao. Na sisi wasomi sharti tuungane ili tuendelee kusoma kiingereza na kizungu KWA pamoja katika pilika pilika za kujiandaa kuongoza taifa letu lenye wasomi wengi wa shule za reja reja na jumla. AS LONG AS YOU HAVE SCHOOL FEES TO PAY, PASSING GRADE IS NOT A PROBLEM. remember that UNIVERSITIES CONNECTSSSSSSSSSSSSSSSSS.

    ReplyDelete
  6. Tunashukuru sana kwa maoni yenu wadau tumeyafanyia kazi yote

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...