Kamati ya Miss Tanzania ilikaa na kutafakati kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1.Taarifa kamili ya maafa tulipata sa 9:30 mchana masaa machache kabla ya mashindano ya urembo ya Miss.Tanzania kuanza.
· Jibu letu:Ajali ilitokea saa saba za usiku,waokoaji walifika tokea saa kumi na mbili asubuhi,vyombo vya habari ulimwengu mzima vilitoa breaking news tokea saa mbili asubuhi na pia maandishi ya breaking news yalikua yanapita tokea saa mbili asubuhi takriban dunia nzima BBC,SKY NEWS,CNN,ALJAZIRA,N.K
· Kusema kwamba taarifa mliipata saa tisa kwa Tanzania si kweli sisi wa Ugiriki tumepata taarifa kupitia BBC saa nne asubuhi tena baada ya kuambiwa na raia wa kigiriki kuwa kumetokea maafa na ndio tukaamua kuangalia TV.
2.Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo Yanga na Ruvu Shooting.
Jibu letu: Haya ni mawazo finyu,hata mtoto wa darasa la tatu hawezi kusema kuwa nimetoroka shule kwa kuwa rafiki yangu nae ametoroka,ila atatoa sababu kama nilikua naumwa nilienda hospitali na sio sababu za kipuuzi,Kwa upande wa Biashara : Unahitaji kujua nini kuhusu washindani wako ambacho kitasaidia kuimarisha biashara je mlijiuliza masuala haya?
(a)Wao ni nani? (b)Hao TFF Wana biashara gani? (c) Wanapangaje bei za bidhaa zao? (d) Wana idadi ya wateja wangapi ukilinganisha na ya kwenu? (d) Kushindana nao kunaleta faida na hasara gani? (e) Kuingia kwanu katika soko au bidhaa au huduma zenu katika soko au kubadilisha bei zenu wanachukulia vipi?.
Utapata jibu kuwa biashara zenu ni tofauti kabisa hazihusiani na pia kushindana nao ni upuuzi kutokana wao wana objectives tofauti na zenu.
3.Kumbi za starehe na mabaa,burudani na mziki wa bendi kumbi za disco burudani
ziliendelea kama kawaida.
· Jibu letu:Ukiwachia kuwa wao wana objectives tofauti na nyie pia zingatia kuwa Mashindano ya Miss.Tanzania ni ya kitaifa,na yanaangaliwa karibu duniani kote lakini hakuna hata mmoja anaeangalia bar gani inauza vinywaji gani,(Service and Product industries are two different things) havihusiani.huwezi kabisa kuangalia wao wanafanya nini,ina maana wao wakitenda maovu na nyie mfanye pia?
4.Muda wa kuwakilisha mshiriki wa Miss.Tanzania kwenye Miss.World ulikuwa
umekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kukosa nafasi.
· Jibu:Hii ni very poor strategic planning,Kila biashara lazima itafakari kitaalamu kutumia PESTLE,(Enviromental analysis includes PUBLIC CONCERN) unahitaji ku asses biashara yako kama kweli inajali ethical and moral issues au kupata faida tu . tuchukue mfano ingelikua kumeripuka bomu ndani ya ukumbi mlioandaa mashindano yenu na washiriki wamefariki jee,mgelimchagua nani kuwakilisha?
· Lakini good strategic planning ni kwamba mngelichagua miss wenu kabla ya muda wa mwisho wa kuwakilisha kutokana kama kungetokea lolote kati ya hao mamiss basi mna muda wa kutosha kabisa kuchagua miss mpya na sio dakika ya mwisho,hiyo ni bad management kabisa.kwa kuwa planning ni kuondoa risk kwa hiyo mmeshindwa kulitambua hili na kujua thamani ya raia,ila mmejali faida tu.(Rais Kikwete ameandaa safari muda mrefu na gharama kibao na pia ni safari ya faida kwa Watanzania lakini amewacha safari hiyo ameamua kuenda kwenye msiba.)
5.Tamko rasmi la kusimamisha shuhuli zote za burudani kitaifa lilianza tarehe 11 september,
· Jibu:Sawa na iwe limetoka tarehe hiyo,je wewe ni binaadamu umepewa akili,sio kama mnyama ambae anaeweza kufanya mapenzi mbele ya watu, ina maana kama kungekua na moto barabarani ungeliendelea kupita hapo hapo tu,kwa kuwa hujaambiwa usipite kuna moto? Si ungelitumia akili yako kuwa utaathirika? Na vipi wale waliojitolea kuokoa walikua wasubiri tamko la serikali wakaokoe?
Mwisho tunapenda kumfahamisha bwana Mkubwa kuwa sababu zote zilizoorodheshwa ni very poor kwanza hazihusiani kabisa katika mazingira ya kibiashara pili zimeendelea kuwapa maumivu Watanzania,Tatu inaonekana hata shule ya management bwana mkubwa hajapitia,na Nne inaonekana wanajali maslahi yao tu na sio ya Taifa.
IT Manager (Abdul)
Vijana wa Kitanzania Ugirikia
hivi Viodacom ni kampuni ya uokoaji au vipi?
ReplyDeleteshughuli zote ziliendelea kama kawaida, kuanzia kampeni, mipira, vituo vya tv kupiga taarabu na programu za kawaida lakini imekuwa kelele kubwa sana kwa voda na ishu yao ya "vichupi".
je ni voda ndio waliozidisha mizigo kwenye meli, ni voda ndio walioshiondwa kuokoa, je ni voda ndio waliwaambia watu wapande ferry la mizigo, je ni voda ndio ilimwambia capteni wa pili aondoe meli? tuache kutoa lawama pasipo na mpangilio, tutatue tatizo tuache kelele nyingi.
taifa lisilojali maslahi yake nani atayajali....!?
Ninyi vijana wa Kitanzania Ugiriki,nishirikiane na ninyi kwa kile mlichotushirikisha Watanzania na ulimwengu kwa ujumla juu ya tamko la kuomba radhi kwa kamati ya uandaaji wa tamasha la kumtafuta misi Tanzania kwa watanzania juu ya hali halisi iliyojitokeza siku tatu zilizopita.
ReplyDelete1]Majibu yenu ya hoja zilizotolewa na kamati ya maandalizi kupitia Mkurugenzi wake wa uandaaji wa tamasha hilo ni sahihi kabisa na yana logic za kiubinadamu na kiustaarabu.
2]Kwa mtizamo mwingine,hoja/majibu yenu yamelenga kutokukubalina na radhi/msamaha ulioombwa na kamati ya maandalizi kupitia Mkurugenzi wake kwa niaba ya wote walioshiriki tamasha hilo siku hiyo kupitia vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi.Hapa ninatofautiana na ninyi.Hamkuonesha kuridhia ombi lake la kuutaka umma wa Watanzania na ulimwengu kwa ujumla kuwasamehe kwa yote yaliyojili.
Kwetu sisi wana diplomasia,msamaha ni kitu cha kwanza endapo utaombwa na upande husika.Na huu ndiyo msingi wa ubinadamu na ustaarabu pevu.
3]Ujumbe wenu nadhani umefika,lakini kwenye aya zenu za mwisho mlionyesha kutumia hisia za jazba kwa kuanza kukosoa taaluma ya kamati na Mkurugenzi wa maandalizi ya tamasha kwa hoja zake alizozitumia kutuomba radhi watanzania wote kwa ujumla,ambapo maneno mliyoyatumia yamepotosha ujumbe wenu wote na kutufanya wasomaji na watanzania tutofautiane na ninyi kwa hilo.
4]Mwisho,Ni vizuri na ni busara kama taaluma zetu tulizonazo zitatusaidia kujenga,kurekebisha,kukosoa,kuonya,na pengine kuelimisha jamii bila kuonesha tofauti au ushabiki na pengine kutumia baadhi ya lugha/maneno yenye viasili vya kumomonyoa maadili yetu binafsi na Taifa kwa ujumla kwa kuzingatia
ukweli na usahihi wa mambo huku tukitumia falsafa ya muafaka wa mawazo kwa njia ya kidiplomasia.
Mdau.
Very interesting...wewe Abdul inaelekea una more reasons behind ur arguments! whatever u've written is not constructive at all... why not being practical and complain about the cause of this accident where innocent pple hv lost their lives in the first place?! Kweli kuna watu ngumu kuwaelewa wanapoingiza siasa kwa kila jambo...Forget abt Miss TZ mgnt, and chip in a concrete debate on the actual accident.. I'm very sure hukuacha kula ama shughuli zako za kawaida siku hiyo ya ajali, au nimekosea? then go figure...
ReplyDeleteMICHUZI KWA HESHIMA NA TAADHIMA NAOMBA UTOE UPUUZI HUU, TUKO KWENYE MAOMBOLEZO SASA.
ReplyDeleteWE DONT HAVE TIME FOR THIS BS, WE NEED TO DISCUSS ON HOW TO PREVENT SUCH DISASTERS AND NOT WHAT LUNDENGA DID, ESPECIALLY WHEN HE ALREADY APOLOGISE.
i like the way you analyse your points
ReplyDeletehawa watu wameandika POINT KBSAAAAAAAAAAAAAAAAA and am so happy uncle umeweka hii walai hawa ndo watu wakupewa kazi wanajua kufikiri na wana uchungu na nchi byzeway huyu LUNDENGA ASTAAFU sasa toka nazaliwa yupo kwenye kazi iyo iyo ONA SASA umri umeenda mpk kufikiri anshindwa cheki alivokosolewa yani yooooooooooooooote aloandika ni pumba VIJANA WAMEMUUMBUA KBS tehe tehe tehe ITS A BIG SHAME
ReplyDeleteAnkal inabidi kustopisha huu mjadala huu sio wakati wa kuonyesheana vidole wakati familia zipo katika wakati mgumu. Tumia hekima zako poteza huu mjadala kiaina la sivyo utaeneza chuki kwa kupitia mtandao huu wa jamii na this is not one of our mission! Huyu bwana Lundenga amechemsha big time kwa kuomba msamaha angekaa kimya kwani hakuna chombo cha habari kilicholalamika juu yao. Malalamiko ndo yanaanza sasa kwa kupitia mtandao huu.
ReplyDeleteIdumu blog ya jamii idumuuuuuuuu!
Huyu lundenga hana sababu moja ya msingi amefanya kwa makusudi na anajua anachokifanya Habari tanzania nzima ilikuwepo tangu asubuh siku ya tukio kwa aliechelewea kuipata basi si zaidi ya saa 4 asubuhi .Hivyo amefanya kwa makusudi ila reaction na pressure iliyotolewa na watu wanzibar pamoja na tanzania yote ndio iliyopelekea kufanya hivyo.Na sio yeye tu na hata serikali yote kwa upande wa bara pia ilizembea maana kama yeye kashindwa viongozi pia waliona hili na shindano pia lilikua wazi si siri,kwanini walilifumbia macho. hivyo maoni yangu Lundenga pamoja na viongozi pia wamechngia maana pia wanaweza kutoa amri kama wanavyofanya yanapoanguka majumba kariakoo tunaona jinsi wahandisi wanavyo nyang'anywa leseni zao dakika moja tu, kwanini hili la miss tanzania,mechi za tff, mabaa, la tbc na mengine wayafumbie macho. Naunga mkono Maneno ya mheshimiwa Zito "Taifa liko msibani Umoja wetu uko mashakani " mwisho kwa kunukuu
ReplyDeleteSawa sawa mkubwa kwa kuwapa maelezo ya kutosha. Kwani kitendo walichokifanya c cha kiungwana! Na kiongozi km huyo anatoa reason zisizo na msingi kabisa.
ReplyDeletesina cha kusema zaidi ya kukuunga mkono kwa majibu yako. huyu jamaa nikisema kuwa hana akili sijui kama nitakuwa nakosea sana maana sababu zake ni za kipunguani punguani hivi, nampa pole maana hata kuomba msamaha kwake hakuna maana. ni bora mara elfu kama angeomba msamaha bila kutoa hizo sababu zate za kipuuzi, mimi nadhani inabidi watengwe kama adhabu yao...kwanza nini miss!,kwamaba eti mtachelewa..siku moja ikufanye uchelewe?...wadanganywe au wapumbaze hao wenye upunguanai kama wake.watanzania?
ReplyDeleteVery well drafted
ReplyDeletenashukuru kwa ujumbe huu mithupu hakuubania, kwani nilituma majibu kiasi kama mawazo ya mtoa mada akayabana.nashukuru kwa majibu mazuri kwa mheshimiwa lundenga.LAKINI TUMSAMEHE ILA HATUTAMSAHAU.
ReplyDeleteYani Ndugu Yangu Abduli Sikufaham ila I share the same feelings na wewe...There is no excuse kwa waliofanya NO kabisa.Na ushaur wangu ni kuwa wangeomba msamaha then wakakaa kimya.Tabia ya kuomba msamaha na kuweka sababu zisizo mashikio ni kuendeleza dharau.Next time ukikosea sema samahani nimekosa.(nukta) do not go ahead tryn to justify your actions.It removes all the meaning ya msamaha wako.Learn from your mistake.BTW what has Miss Tanzania brought to this country ?Naomba niishie hapo nisije nikachafua hali ya hewa kama ilivyoandikwa hapo juu....Big up Mr Abdul
ReplyDeleteMI SIELEWI, KWANI INA MAANA SIKU HIYO ILIPOTANGAZWA MELI IMEZAMA, WATU WOOTE WALIACHA WANACHOKIFANYA NA KUKAA NYUMBANI KUOMBOLEZA. HII EVENT YA MISS TZ, IMEANDALIWA KWA MUDA MREFU SAAAANA. JE TULITAKA JAMANI SIKU HIYO WATANGAZE KUCANCEL KWA SABABU MELI IMEZAMA. HALAFU TULITAKA IFANYWE LN TENA HIYO EVENT? MIMI NAKUBALIANA NA KWAMBA MUDA PIA ULIWABANA, KWANI HII NI INTERNATIONAL BUSINESS, ILA NINAAMINI KM WANGEAMUA KUCANCEL, INGEWAPA VODACOM A BIG LIFT IN THEIR NAME. LAKINI NAONA SWALA HAPA NI KWAMBA WATU WAKO TU AGAINST NA MAMBO YA UMISS, THATS IT NOTHING ELSE. NDO MANA VITU VINGINE VILIVYOENDELEA WATU WAMEVINYAMAZIA KIMYA. MICHUZI NAKUSHAURI KUUPIGA CHINI HUU MJADALA KWANI MISS TZ INGECANCELL SIKU HIYO HAIMAANINISHI NDIO WANA HUZUNI SANA, CHA MUHIMU NI KUWA TAYARI KUSAIDIA KITU AMBACHO WAMETAKA KUFANYA LAKINI WAMEKATALIWA.
ReplyDeleteHapa sioni kwa nini kunajitokeza malumbano na kumlaumu muandalizi wa Miss Tanzania; nasema hakuna sababu ya kumlaumu kwa sababu. 1. Ameomba msamaha kwa wapenzi wa Miss Tanzania. 2. Wakati wa shindano washiriki na waandaaji walitoa heshima zao kwa msiba. 3. Kulikuwa hakuna kingine kamati ya Miss Tanzania ingefanya.
ReplyDeleteHaiingii akilini kumlaumu kwa kuendelea na shindano kutokana na ukweli kwamba, tayari tukio lilishatokea, maandalizi yalishafikia mwisho na kwamba kuahirisha kwa aina yoyote kungesababisha gharama ambayo hakuna ambaye angeweza kuilipa. Lakini kubwa zaidi, watanzania tunalielewa hili, kuwa hata harusi wakati mwingine huendelea wakati kuna msiba mkubwa ndani. jambo hili ukilitizama objectively utaona, ni kama watanzania sasa tuko tayari saaana kulia na kutoa misaada na pole za rambirambi. Lakini hii hatuwatendei haki waathirika, badala yake, TUSIMAME WOTE NA KUDAI KWA NINI TUKIO KAMA HILI LIMETOKEA TENA, NANI NI TATIZO, SERIKALI au MWENYE CHOMBO, NA KWANINI UOKOAJI ULICHELAWA. haya ndiyo tupiganie ili tuwatendee haki waathirika na siyo kuhamishia hasira kwa Lundenga ambaye naye anahangaikia kula yake na familia yake.
Nawakilisha, na Mwenyezi MUNGU awalaze mahala pema marehemu.
jamani yaliotokea yametokea,na kila mmoja hufa kwa ahadi yake.some times hatuwezi kupangua alilopanga mola..1 lundenga amekosea na uzuri amelingundua na kuomba msamaha hizo point ni katika kujitetea tu...2 hapa hakuna wa kuchuliwa hatua kamwe sababu binadamu tumepewa fahamu kama meli ilikua tayari imejaa walitakiwa kujali usala wao pia abiria wenyewe..ila alipangalo MOLA HAKUNA WA KUPANGULIA..MUNGU AWAPE KAULI THABIT NA AWASAMEHE MAREHU WOTE KWA UJUMLA..AMENAH
ReplyDeleteWhere is our moral obligation? I see no point of attacking Mr. Abdul for sharing his thought, the accident was tragic and how we deal with the aftermath is what defines us. I didn’t expect much from Mr. Lundenga “I’m not judging” it’s a matter of infamous reputations regarding his organization. Sometimes back circa 2003 after he hosted children “underage” beauty contests, one tabloid reported Muslim clerics has threatened to outlaw him and will not bury him according to the faith. He was good in words in ridiculing them; it didn’t bother him for his decaying body! Someone mocking his demise what do you think he’ll do to others?
ReplyDeleteIf the govt. of Tanzania still operates vessels like steamer MV. Liemba a 98 yrs. Old ship! Though how sad it is, we still have more tragedy to witness…
Showing concern for the bereaved is humanity. Lundenga anastahili lawama sana kuliko wengine kwa kuwa nature ya shindano lake ni live halafu ni sherehe fulani hivi. Are we not like one body when one organ is ailing the rest of body screams in pain? Napingana na wale wanaosema si wakati wa kumlumu Lundenga kwa kisingizio kuwa tupeleke hisia na akili zetu kutafuta chanzo cha ajali. Kitendo chake kama hakikulaumiwa kina athari pana zaidi, kwanza kitafanya tukio lile lionekane la kawaida tu na hata wazembe ambao kwa namna moja au nyingine wamesababisha ajali ile wanaweza wasijisikie guilt. why should they bother if the community itself is not concerned?
ReplyDeleteAjali hii ni kubwa na watu wengi walioadhirika, mpaka sasa maiti 202 zimepatikana. Haikuwa busara kuwatembeza watoto wadogo wa kike na vichupi kutafuta nani mzuri wao kwa siku ile. Hii biashara ya U-Miss inategemea wadhamini na wadhamini lengo lau ni kutangaza biashara zao, na biashara zao zinategemea wateja ambao ni binadamu wenye hisia. Huu si wakati wa Mwalimu, hivi sasa kuna bidhaa moja inauzwa na wafanya biashara wengi kwa ni rahisi mteja kuamua kwa sababu zake kwa nini anunue kwako asiende kwa mwengine. Tiger Woods kwa kukamatwa na nyumba ndogo tu wadhamini wake wamemkimbia itakuwa Lundenga kwa kuwavisha wasichane vichupi siku wananchi wengi wanatafuta maiti za watoto wao baharini?
ReplyDeleteWachangiaje wengine mnaniacha hoi. Yaani badala ya kuongelea whether alichofanya Lundenga ni sahihi au la mnaongelea meli ilijaa abiria waliyataka wenyewe. Hivi are you listeaning to what you are writing. Hamuoni aibu kuandika kitu kama hcho. Yani ni kama mnasema abiria wali diserve hayo maafa kwa hiyo ni sahihi watu kuendelea ku party. Muogopeni Mungu Jamani.
ReplyDeleteMajibu ni sahihi kabisa,SASA MBONA HUYU Bwana lUNDENGA AMEOMBA RADHI?Kwani ametenda kosa gani? Ikiwa ametoa pointi zake za kumuwezesha kuendelea na shindano,ina maana haina haja ya kusema nimeomba radhi angelisema tu,tuliendelea kwa kuwa tumeona kwa mtazamo huu hatujakosea,Kweli vijana wa Kigiriki mna akili sio kama tunavofikiria nyine ni mabaharia na wabeba boksi tu,Nadhani kamati nzima ya Miss.Tanzania ina mawazo finyu kama kweli walikaa na kutafakari wakaona wafanye hivyo kwa vijipointi finyu walivotoa,basi kweli hawana good management,kwa kuwa biashara lazima iwe na OBJECTIVES na objectives inatakiwa iwe SMART,ili kutimiza hizo OBJECTIVES kunatakiwa kuwe na strategic kama walivoeleza wenzetu na strategic inamaana kuna njia mbadala KUMETOKEA TATIZO tunabadilisha Objective na tunatumia njia gani SASA INAONEKANA HAWA miss tanzania hii biashara inaendeshwa ovyo ovyo tuuuu,haina hata kufikiria.WATANZANIA UGIRIKII HOYEE japo wengine wanakupingeni humu
ReplyDeleteKWANI NYIE WADAU MMEMUONA LUNDENGA NA MISS TANZANIA YAKE ND'O MWENYE MAKOSA?
ReplyDeleteMBONA MIKUTANO YA KAMPENI YA CCM, CUF, CHADEMA NA VYAMA VINGINE VINAENDELEA NA KAMPENI ZAO HUKO IGUNGA?
LUNDENGA KUJITIA KWENYE GLOBU NA KUOMBA RADHI NI KOSA. HAKUWA NA HAJA KUOMBA RADHI WAKATI WALIHESHIMU MAAFA KWA KUTOA HESHIMA ZAO KWA WALOPOTEZA MAISHA.
HUYO MDAU WA UTURUKI AMBAYE NAAMINI KABISA NI HUKO HUKO KULIKOTOKEA MAAFA, AMETOA HOJA NYINGINE ZIKIWA NA MIFANO FINYU, ELIMU TAHAFIFU NA ROHO YA KWA NINI KUMLAUMU NA KUMSHUTUMU LUNDENGA NA KAMATI YAKE KUENDESHA SHINDANO LAO KAMA WALIVYOPANGA.
MADAI "KAMA KUNGLIPUKA BOMU NA WATU WAKIWEMO WASHIRIKI KUUMIA AU KUFA, WANGEMCHAGUA NANI? AU MIFANO YA MTOTO SIJUI KAZUIWA KUPITA BLAH BLAH BLAH...HAINA MAANA WALA UZITO WOWOTE. NI MIFANO YA KITOTO, YA SHUKE ZA MSINGI AU CHEKECHEA ISIYO NA NGUVU WALA MWELEKEO.
MISS TANZANIA NI MEMBER WA MISS WORLD NA WANA MUDA WAO WA KUTAFUTA MWAKILISHI WAO KILA MWAKA ILI ASHIRIKI KUTAFUTA MLIMBWENDE WA DUNIA. SHINDANO LAO HUFANYIKA NOVEMBA-DISEMBA KILA MWAKA.
ILI MSHIRIKI AWAKILISHE NCHI YAKE VYEMA, LAZIMA AFANYINWE MATAYARISHO MENGI TU IKIWA NI PAMOJA NA KUKABIDHIWA BENDERA YA NCHI AWAKILSHAYO. KUNA PROTOCOL KIBAO AMBAZO ZINAHITAJI MUDA. NA MUDA WALONAO NI WIKI NI MFUPI.
UKITAKA KUTOA LAWAMA NA KAMA KWELI UNA UCHUNGU NA WALOKUFA, OMBA WADAU WENZAKO WASISITIZA SERIKALI IRUHUSU TUME HURU TENA TOKA NJE YA NCHI ICHUNGUZE MAAFA HAYO.
UNDA TUME YAKO HUKO TURKIYE IWAULIZE CLOVE GOVT WALIJIFUNZA NINI KUTOKANA NA AJALI YA MWAKA 2010 ILIYOTOKEA KWENYE MDOMO WA BANDARINI HUKU WATU WAKIPOTEZA MAISHA YAO BILA HATIA ILI KUZUIA MAAFA KAMA HAYO YASITOKEE TENA.
MAOMBO YA YAKHE YANAHARIBU SANA NCHI. MELI HIYO INASAFIRISHA ROHO ZA WATU HATA KAMA NI WAWILI, KWA NINI ISIWE NA CHOMBO CHA MAWASILIANO NA IDARA ZA POLISI NCHI KAVU NA MAJINI, BARUTI ZA KUTOA ISHARA PINDI TATIZO LIKITOKEA NA IDADI ZA KUTOSHELEZA ZA VYOMBO VYA UOKOAJI.
BADALA YAKE WALIKUA NA TAA YA CHEMLI, DINGI MOJA LILILOBEBA ZAIDI YA WATU 60 (ANGALIA PICHA MICHUZI). NAHODHA ALIKIMBIAJE KWANZA NA KUACHA ABIRIA WAKIZAMISHWA NA CHOMBO?
TUSILAUMU MTU MWINGINE AMBAYE HATA UNGFANYAJE ASINGEWEZA KUSAIDIA LOLOTE WAKATI WA TUKIO. UWEZO WAO NI KUTOA MSAADA KWA WAHANGA KAMA WAKITAKA. LAUMU SERIKALI YAKO ILIYOJAA UZEMBE, VIONGOZI TOKA ENZI YA UKOLONI BADO WAPO MADARAKANI DORMANT WITH NO NEW IDEAS. I WISH MI ND'O NINGUKUWA LUNDENGA!!!!
Familia ya Lungenga ingekuwa kwenye hiyo meli je?? How about Familia ya Kikwete?? Alipofariki baba wa taifa, hata harusi zilizuiliwa kupiga matarumbenda kwa muda wa siku 40. Tafakarini. hao waliokufa pia ni binadamu kama huyo Nyerere na wanastahili heshima pia.
ReplyDeleteAnkal funga huu mjadala. kwanza Lundenga hakuwa na cha kuomba msamaha. Kwani wangecancel mashindano hao waliokufa wangefufuka?? Na pia abiria wenyewe hawakuona kuwa meli imejaa? badala ya kumnyooshea Lundenga kidole, anzeni na raia wenyewe,ambao hata wakijazwa kwenye meli au mabasi kama nyanya wanakaa kimya.Ajali ikitokea ndo watu kama kina Abdul wanaanza kuchonga..its about time abiria wenyewe wawe responsible na maisha yao na sio kulalama day in,day out.
ReplyDeleteABDUL KAMA UNAUCHUNGU SANA NA AJALI YA MELI BASI TUMIA NGUVU ZAKO HIZO ZA ZIADA KUHOJI UZEMBE ULIOFANYWA NA WATENDAJI WA UNGUJA HADI KUSABABISHA AJALI.
ReplyDeleteMISS TANZANIA HAIKUWA NA CHOICE BALI KUENDELEA KWA MUJIBU WA MAELEZO YAO (DECISION YA KURUHUSU YALE MASHINDANO HAIKUWA RAHISI KAMA AMBAVYO TUNAVYOFIKIRIA SASA).
NI WAZI KABISA MISS TANZANIA INGEWEZA KUFUNGULIWA MASHTAKA KADHAA YA MADAI KUTOKA KWA WATU WALIOKWISHA KATA TIKETI NA HATA WADHAMINI WA MATANGAZO ETC.
WEKEZA NGUVU ZAKO KUJUA WHAT HAPPENED HADI AJALI IKATOKEA, NA NINI KIFANYIKE AJALI KAMA ZILE ZISIJITOKEZE TENA.
HALIKADHALIKA TUJIULIZE, KWANINI SMZ ILIKUWA NA TAARIFA TANGU MUDA MEZI IMEPATA MATATIZO LAKINI WALIKWENDA KUOKOA WATU ASUBUHI?
Nawaunga mkono watanzania wenzangu wa Ugiriki,na nashauri serikali yetu ijaribu kuwaangalia watu wenye tabia za kujali maslahi yao pekee kama LUNDENGA na ikibidi wachukuliwe hatua.Siku chache zilizopita mamiss hawa walifanya ziara mikoani na walioenekana wakishiriki katika shughuli za kijamii kumbe ulikua ni unafiki tu!!!wangekua wamestaarabika siku ile wangeenda zanzibar japo kuwafariji wafiwa kwani najua pengine suala la uokoaji kwao lingekuwa gumu.....leo hii lundenga bila aibu ana nena kwamba muda ulikua umeisha....je kama lundenga au mke wake(kama yupo) angefikwa na mauti siku ile bado tungeendelea na mchakato huo wa miss tanzania? na je kama miss mmojawapo naye angefariki ghafla tungeendelea na mashindano? Sisi vijana wadogo wa miaka ya themanini hatukupaswa kukukosoa wewe baba yetu Lundenga ila kwa maamuzi unayoyafanya unatukatisha tamaa na kutupunguzia vitu ambavyo tungependa kuiga au kujifunza kutoka kwako.....
ReplyDeleteMeli imezama tangu saa 7 usiku, uokoaji umeanza saa mbili asubuhi, bandarini kuna vyombo vya usalama lakini wameruhusu meli iendelee na safari, naodha aliona mwenzie kagoma yeye kaendesha meli kwenda kuua watanzania. Kweli Lundenga ana makosa lakini ni nani hasa apigiwe kelele katika hili. Je ni nani azungumzwe zaidi. Nashauri tupige kelele zaidi kwenye hizi mamlaka zetu hazifanyi kazi zake (interest zao ela tu).
ReplyDeleteUgiriki yenyewe kwa sasa inazama na inahitaji rescue
ReplyDelete