MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKIWA NA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA SHULE YA MBARALI BW, ALI PANDU HAJI KATIKA MAZUNGUMZO YAO BALOZI SEIF AMESEMA MCHANGO UNAOTOLEWA NA SHULE BINAFSI UNASAIDIA SERIKALI KWA KIWANGO KIKUBWA KATIKA KUPUNGUZA MZIGO WA KUWAHUDUMIA WANAFUNZI NCHINI
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKIMKABIDHI MKURUGENZI WA SHULE YA MBARALI BW, ALI PANDU HAJI SHILINGI MILIONI MOJA NA NUSU IKIWA NI UTEKELEZAJI WA AHADI ALIYOITOWA WAKATI WA MAADHIMISHO YA MIAKA KUMI TOKEA KUANZISHWA KWA SHULE HIYO.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema mchango unaoendelea kutolewa na skuli binafsi umewezesha kuisaidia serikali kwa kiwango kikubwa katika kupunguza mzigo wa kuwahudumia wanafunzi maskulini.
Balozi seif amesema hayo hapo Afisini kwake Vuga wakati akikabidhi shilingi milioni moja na nusu kwa uongozi wa skuli ya Mbarali ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitowa wakati wa maadhamimisho ya miaka kumi tokea kuanzishwa kwa skuli hiyo.
Fedha hizo ni ahadi ya kwanza miongoni mwa alizoahidi tarehe 16/7/2011 kusaidia madeski ya darasaa moja, kompyuta moja, milioni moja kusaidia ununuzi wa madaftari, na shilingi laki tano kwa vikundi vya wanamichezo na wasanii waliotumbuiza siku ya sherehe hiyo.
Balozi Seif amesema sekta ya elimu nchini hivi sasa ni ya kuridhisha kutokana na mchango huo wa skuli binafsi licha ya changamoto zinazoikabili serikali katika ukamilishaji wa baadhi ya vifaa.
Amesema Skuli nyingi bado hazijawa na madeski na juhudi zinaendelea kuchukuliwa ili kuona tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi kwa kushirikiana na taasisi na mashirika ya maendeleo.
“ Kima cha Madeski kwa Skuli zote za Unguja na Pemba kimekadiriwa kuwa Madeski 35.000 kiwango ambacho bado ni changamoto kwa Serikali ”. Alisema Balozi Seif.
Balozi Seif amefarahisha kwamba Serikali bado inaendelea kukabiliana na kazi kubwa ya kuzijengea uwezo wa Kimaabara skuli zake kwa lengo la kuimarisha Somo la Sayansi.
Amesema hatua hiyo inakusudia kuongeza kiwango cha wanafunzi wa fani hiyo ambayo bado iko chini hasa ikilinganishwa na ukuaji wa sayansi na teknolojia uliopo Duniani hivi sasa.
Amesema mazingira hayo yatawapa fursa Vijana kufikia lengo la kuwa wataalamu mahiri wa Taifa hapo baadaye.
Akipokea msaada huo Mkurugenzi wa Skuli ya Mbarali Bwana Ali Pandu Haji amempongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa Juhudi zake za kusaidia Skuli Binafsi.
Bwana Pandu amesema katika kuunga Mkono juhudi za Serikali Uongozi wa Skuli ya Mbarali umeweka Kiwango kidogo cha ada ya wanafunzi ili kumuwezesha kila mtoto anapata Haki yake ya Elimu na msingi. ..
Imeandaliwa na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
2/9/2011.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...