ankal assalamallaikum. 


Ankal mpwao nimekwama naomba msaada hapo tuta
la pili tafazali kupitia mtandao wako .
mimi nahitaji mwanaume wa kunioa sio kuchakachua!
ni mwanamke wa kiislam nina miaka 38 na nina mtoto. ni msomi
wa elimu ya degree na nimeajiriwa katika idara ya serikali nina kipato cha
kati tu. nahitaji kupata mwanaume wa kunioa, popote duniani mradi tu awe
Mtanzania,  Muislam na anaejua nini maana ya Uislam. awe na kipato chake cha
kuajiriwa au kujiajiri.( asiwe wa kumaliza makochi kwa kutazama tv) asiwe na
umri wa chini ya miaka 35 na asizidi 50.

mwenye kutaka kuwasiliana kwa sifa nilizotaja atume email ktk address
M2193M@gmail.com. Please ankal keep my name

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mimi ni Muislam anaishi Zanzibar ningependa kuongeza mke wa pili na nipo tayari kuwa uishi Dar nitakuwa nikija wiki-end na niwapo safari na likizo.

    ReplyDelete
  2. wanasema "mnajuana kwa vilemba"

    ReplyDelete
  3. mimi ninasifa hizo ulizosema,lakini PAGUMU kwangu ni je baba wa huyo mtoto yupo wapi?,na pili huyo mtoto ulimzaa na huyo mwanaume mkiwa mmefunga ndoa au la?,na kama mlikuwa mmeona mmeachana kwa talaka na kufuata sheria za DINI?,naomba ufafanzi wa hayo nami ntajua nianzie wapi
    SHUKRANI

    ReplyDelete
  4. Asalaam Aleikum,mimi nina swali moja tu la msingi je uko tayari kuolewa mmke wa pili, na ulichelewa wapi kutafuta mchumba au ndo ulikuwa unamalizia ujana? jibu tafadhali

    ReplyDelete
  5. mimi namgawa wa kwangu ana sifa ulizotaja ila nimemchoka tu. tutawasiliana dada nawe ujaribu bahati yako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...