Mwakilishi wa Umoja wa Africa (AU) nchini Marekani, Balozi Amina Salum Ali, akiweka sahihi kwenye kitabu cha kumbukumbu ya Maombolezo kutokana na ajali ya meli iliyotokea huko Zazibar wiki iliyopita kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, ulioko mjini Washington DC, jana Alhamisi September 15, 2011. 
 Balozi Amina Salum Ali akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Mwanaidi Maajar, nje ya jengo la Ubalozi huo lililoko mtaa wa 22, North West katikati ya jiji la Washington DC nchini Marekani
Balozi Amina Salum Ali, akibadilishana mawazo na afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Suleiman.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Kuvaa kiislam hakukuondelei usomi au wadhifa wako. Wala hakukufanyi uonekane wa zamani au kupitwa na wakati.

    ReplyDelete
  2. hivi hizo picha za JK za nini hasa. Hazina uhusiano na msiba jamani.

    ReplyDelete
  3. kipi kiswahili fasaha saini au sahihi?

    ReplyDelete
  4. watu wengine bwana! kwani kuvaa kiislam ndio kukoje? kuna mavazi maalum kwa wana dini ya islam? mbona mnataka kutuchanganya? vazi ni maamuzi ya mtu... acha mtu aamua anavyotaka kutokana na anavyopenda yeye? si ulifikiri hawezi kuacha shungi? sasa tuulizane? kwani shungi ndio dini? au? naomba "mnidadavulie"

    ReplyDelete
  5. sahihi na saini yanatumika ila kwa maana tofauti: sahihi ni neno la kiswahili fasaha maana ya kuonyesha kitu ni "sawa", au "sawia", saini ni tafsiri sisisi toka neno la kiinglish (yaani "sign")

    ReplyDelete
  6. Picha ya Nyerere Ukutani ubalozini imepinda... Tunaweza kumuambia Ndugu Suleiman kuirekebisha?

    KenRon - New York

    ReplyDelete
  7. Sasa wewe mdau hapo juu unaleta point ya kuvaa kiislam una maana gani?
    je ?hizi picha zinazoonekana hapa za hawa waheshimiwa akina mama zina uhusiano gani na uislam ?Msipende kuleta upuuzi wa mambo ya dini pahali pasipohusika,dini zenyewe zililetwa na wakoloni sisi tuka jipendekeza tu,na dunia inabadilika haraka sana kutokana na sayansi na teknolojia iliyopo,muda si mrefu hizi dini zote watu wataziacha maana ndicho chanzo cha matatizo na mizozo duniani kote,mtu ana uhuru wa kuvaa anavyotaka ili mrai asikae uchi,jamani tujikomboe ki fikra ndipo tutaweza kuenda na wakati na nchi yetu kuendelea mbele,tusiwe na mtazamo finyu wa kila kitu.

    ReplyDelete
  8. Hee BI AMINA umekuwa hivi unaenda uchi makubwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...