Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, akipokea hundi ya sh. Milioni 40 kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kwa ajili ya Rambirambi kufuatia kuzama kwa Meli ya Mv Spice iliyotokea hivi karibuni katika eneo la Nungwi Kaskazini Unguja. Makabidhiano hayo yamefanika leo katika ofisi ya Makamu wa Rais mjini Zanzibar.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Makamu wa Rais wa Zanziba leo jioni.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi akibadilishana mawazo na Mwenyekiyi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe walipokutana katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar leo jioni wakati wakitoka kwa nyakati tofauti kutoa pole kwa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kutoa mkono wa pole kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, ambapo kwa upande wa CHADEMA Mwenyekiti huyo alitoa ubani wa shilingi milioni 5 kwa ajili ya ajali ya Mv Spice iliyotokea hivi karibuni katika eneo la Nungwi, Kaskazini Unguja.
MZEE MENGI MUNGU AKUZIDISHIE KWA MCHANGO YAKO KATIKA JAMII,PIA UNGEFANYA JAMBI LA BUSARA SANA KUBADILISHA NAMBA ZA SIMU YAKO ULIOMPA MBOWE PLS'E.
ReplyDeletemiwani mbili mbili rais mtarajiwa za nini. huo si ujana viongozi wetu ni ulimbukeni. ficha hiyo usiyovaa au mpe bodi wako. duh. viongozi wetu hawa jamanii. well done mengi nice dress up.
ReplyDeleteAnonymous wa kwanza hapo juu inaonekana unaroho mbaya sana, sidhani kama mumeo anao hata marafiki, hapa walikuwa hawabadilishani namba, kwataarifa yako wanafahamiana kitambo sana na wamekuwa wakionana mara kwa mara, wakati picha zinapigwa sim ya Mh Mbowe iliita ndipo akawa anaiattend kwa kutuma msg nadhani ya kumwambia mpigaji amcontact baadae hakutaka kuharibu mazungumzo na Mzee Mengi.
ReplyDeleteDume Jeuri
Hizi pesa zitafika kwa walengwa au kuna jitu mmoja tu litaziweka mfukoni and nothing will happen to him. Mjinga mmoja kala rushwa amesababisha ajali na wala hatujasikia lolote kuhusu chanzo cha ajali.
ReplyDeleteWatu wengine muwe mnaelewa,miwani miwili sasa inakushangaza nini mbona mnakuwa malimbukeni.Unaiona kabisa unaona mmoja ni wa jua na mwingine ni wa macho au kusomea!!!Hiyo ina kazi tofauti.try to think big
ReplyDeleteWazee, kweli sasa mko serious! kila kona..mpo? ..mimi nadhani sasa mpewe tu NCHI!
ReplyDeleteAnonymous wa tatu umemwambia wa kwanza kuwa hata mume wake hana marafiki umejuaje alieandika hapo kama ni mwanamke, labda ni dume?
ReplyDeleteWatanzania sisi ni watu wa ajabu kabisa. Tuko kama tunashangilia au tuonekane tunatoa rambirambi. Ukweli ni kuwa watu zaidi ya 200 wamekufa, Ziwa victoria 400 na ushee, reli ya kati sijui wangapi, mererani sijui wangapi, Ajali kila siku zinachinja kama si ndugu yako basi wangu au wa mwenzetu Mtanzania na bado watakufa wengine....sisi tunahangaika na rambirambi tu....HAZITASAIDIA KITU.
ReplyDeleteWATANZANIA TUNAO WAJIBU WA KUWA WAKALI TENA SANA KWA SERIKALI IWE MAKINI KUEPUKA AJALI ZA KIJINGA KWA KUHAKIKISHA SHERIA ZINAFUATWA. NA IJIANDAE KUKABILI MAJANGA YANAPOTOKEA.
FIRE AND RESCUE SERVICES ZIIMARISHWE(fIRE N aMBULANCE)
COAST GUARD AND RESCUE SERVICES ZIIMARISHWE.
INAVYOONEKANA WENGI KAMA SIO WOTE WANGEWEZA KUOKOLEWA LAKINI VIFAA HAKUNA, WAOKOAJI HAKUNA, HELCOPTER ZA UOKOAJI HAKUNA......SASA WAKUBWA WANAMWAGIKA NA VITAMBI NA MASHANGINGI KUTOA RAMBIRAMBI KWANI WAO NI WAFUFUAJI?!!
TUACHE HII TABIA YA KUSHEREKEA RAMBIRAMBI BALI TUANGALIE UKWELI, TUULIZE MASWALI, TUDAI HAKI!!! .....WAFE WANGAPI NDIO TUAMKE????!!!!!!!!!
MZAWA!!!