Mh. Anna Abdallah (MB)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa, Anna Margaret Abdallah (Mb) kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Korosho.

Sambamba na uteuzi huo, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe kwa mujibu wa Sheria ya Tasnia ya Korosho na 18 ya mwaka 2009, Kifungu cha nne (4) amewateua Wajumbe wengine Nane ili kuiongoza Bodi hiyo itakayosaidia kupeleka mbele sekta ndogo ya zao la Korosho.

Wajumbe wa Bodi hiyo ni kama ifuatavyo: Bwana Twahir Nzallawahe, Mtaalam wa Agronomia kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika; Bwana Muzamii Karamagi, Mwakilishi wa Wabanguaji wakubwa wa korosho na Bibi Tumpale S. Magehema, akiwa Mjumbe kutoka kundi la Wabanguaji wadogo wa Korosho.

Wajumbe wengine ni Bwana Madanga Allon, Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU), Bwana Yusuph S. Namila, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba Newala Cooperative Union (TANECU) na Dkt. Peter Massawe, Mtaalam na Mtafiti wa zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Zao la korosho Kanda ya Kusini, ARI – Naliendele.

Aidha, Waziri Maghembe amewateua pia Mheshimiwa Jerome Bwanausi, Mbunge wa Lindi, Profesa Haji Semboja, Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Bwana Hemed Mkali, Mkulima wa Korosho Mkoa wa Pwani na Bwana Mudhihir Mohammed Mudhihir Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mchinga Mkoani Lindi. Uteuzi huo unaanza mara moja na utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika,
Dar es Salaam,
Simu: 2861319; 0769-239946; 0718-128653

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hivi hawa akina Anna Abdalla, Pius Msekwa, Getrude Mongela, Kingunge Ngombare Mwiru, Mark Bomani, George Kahama, akina Kaduma, akina Iddi Simba na wanaofanana na hao, ni lini hatutawasikia tena kwenye siasa, uenyekiti na ujumbe wa bodi kumikumi na uongozi mwengine? Waliokua wana akili miaka ya 60 waliwasikia, wa miaka ya 70 nao waliwaona na kuwasikia, tulioanza a,e,i,o,u miaka ya 80 tumewasikia, chipukizi wa miaka ya 90 wanawajua fika, wa miaka ya 2000 nao wamo, sasa tuko muongo wa kuanzia 2011 bado tuko nao, hawachoki, hawazeeki, hawaachii hizo nafasi, as if wengine wenye uwezo hawapo!!! Jamani, hata kama hao wanaowapa hivyo vyeo wanajipendekeza, nyie hamna moral responsibility ya kukataa na kuwashauri kwamba mmelitumikia taifa katika nyadhifa hizo kiasi cha kutosha sasa mnaomba mng'atuke muwaachie damu changa?! Kwanini isifikie mahali mkae pembeni muwe washauri kama alivyowaonyesha mfano Baba wa Taifa?? Tumechoka jamani kuwasikia nyie kila siku tumechokaaaaa...wengine wapo wapeni nafasi!! Tutafikia mahali Tanzania itakuwa na viongozi wakongwe tu, kutakuwa na ombwe la uongozi hapa katikati kwa sababu hatuachiani vijiti na kuelekezana kazi kuchanganya damu mpya na ya old school. Itakapofika wakati wenu wa kuachia ngazi hata kumbukumbu zitapotea, na macho hayatakuwa yanaona, handover mtafanyaje???!!!

    ReplyDelete
  2. Duh Anony wa hapo juu umekonga!!! Big Up

    ReplyDelete
  3. Tumchokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.....

    ReplyDelete
  4. hii ni sababu mmojawapo ya nchi kurudi nyumbani kwa sababu ya watu kama hawa amabo basically hawana mawazo mapya tena. kwa sababu michuzi nafanya kazi na wazee kama hawa ni wagumu sana kubadilika kwani ukitaka mabadiliko ili kuendana na wakati wanakuwa ni vikwazo vikubwa kwa sababu they can not keep up with changes ambazo zinatokea kila baada ya miezi tunaitaji damu mpya na watu wapya wenye mawazo mapya.

    ReplyDelete
  5. Well said. Nilikuwa na mawazo kama hayo ila sikutegemea kama yangerushwa. Tunahitaji inclusive governance. Si sura hizo hizo tuuuu

    ReplyDelete
  6. FOR PETE'S SAKE HII KASUMBA TUIACHE JAMA, MAJINA HAYAHAYA TU TANGU PRE, DURING, POST NA MPAKA SASA ULTRA-POST INDEPENDENCE? SASA UNAKUA USHAMBA HUU. MNAONESHA KABISA HAPO JUU HAMNA IMANI NA MAJORITY YA WANANCHI NA WASOMI/WANATAALUMA WA NCHI HII. YANI NYIE NI HAKO KA-CLIQUE, KA-INNER CIRCLE KA SURNAMES, IN-LAWS NA WASHKAJI TU... UZAMANI WA HALI YA JUU HUU, UJIMA ULIOTUKUKA NDIO MAANA HAKUNA MABADILIKO WALA MITAZAMO MIPYA KATIKA SEHEMU NYINGI ZA UCHUMI, SIASA, NA UONGOZI WA NCHI YETU. HATA SONI HAMUONI?

    ReplyDelete
  7. Mkapa alishawahi kuwajibu wadau wenye maoni yaliyotawala kwamba mna 'wivu wa kike'. Sasa mnataka Mama Msekwa akale wapi? Kama hampendi sana hii hali tumieni nguvu ya kura zenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...