Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha wakuu wa mikoa aliowateua hivi karibuni.Sherehe za kuwaapisha wakuu hao wapya wa mikoa imefanyika leo asubuhi katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam.Pichani ni Mkuu mpya wa Mkoa wa Tabora. Bi.Fatuma Mwassa akila kiapo mbele ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete na kukabidhiwa miongozo ya kazi.(picha na Freddy Maro).
Home
Unlabelled
Rais Kikwete awaapisha wakuu wa mikoa Ikulu jijini Dar es Salaam leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Huyu Fatuma Mwasa tunamfahamu sana tu,alikuwa muandishi wa habari wa mitaani tu,akapachikwa ukuu wa wilaya Mvomero sasa mkuu wa mkoa,Hii inadhihirisha kuwa katika serikali yetu watu hupewa vyeo kwa kujuana,na hicho kitu kinasababisha nchi hii kuwa na matatizo sugu,watu wanaaaowekwa madarakani na rais wengine hawana qualiicatins zozote wala experiance ya uongozi,bali wanajuana na rais au ni marafiki wa first lady.Inasikitisha sana haijulikani tutakakoishia ni wapi na hii system.Uonevu na ufisadi utakwisha tu Tanzania na siku itafika,maana hata Gadaffi haamini yanayoendelea nchini mwake.amebaki kujificha kama panya.Mungu ibariki Tanzania yetu ya mateso na ufisadi.
ReplyDeleteKeep it up dada Fatuma Mwassa, hongera sana
ReplyDeletePole yako kama huna wa kukuweka kwenye nafasi ya juu.
ReplyDeleteSidhani kama unamfahamu dada Fatuma vilivyo, alikopitia baada ya uhandishi wa habari?!
Na sidhani kama unajua kazi alizozifanya Mvomero, utabakia kua HATER tuu.. Pole sana anon wa kwanza..