Ndugu zetu Watanzania,


Kwa niaba ya WANACCM CHUO KIKUU ARDHI,tumezipokea kwa majonzi na mshtuko mkubwa taarifa za ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spicer usiku wa tarehe 10/9/2011 iliyosabababisha vifo vingi vya Watanzania wenzetu.Hakika ni msiba mkubwa na pigo kwa kuwapoteza ndugu zetu wapata 240 na wengine kujeruhiwa.


CCM-ARDHI  tumepokea kwa masikitiko makubwa na tunawaombea majeruhi wote wa ajali hiyo wapone haraka ili waendele nashughuli mbambali za  ujenzi wa familia zao na taifa kwa ujumla. Kwa wafiwa tunawaombea kwa Mungu wapate nguvu katika kipindi hiki kigumu kwao na taifa.


Tunatoa salam za rambirambi kwa wahanga wote waliopata msiba huu mzito,Pia tunatoa salam za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar Mh Mohammed Shein.


Kwa niaba ya Uongozi wa TAWI LA CCM CHUO KIKUU ARDHI, tunapenda kutoa salamu zetu za rambirambi kwa wananchi wote wa Zanzibar na Pemba na Tanzania kwa ujumla waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki zao wapendwa.Na pia tungependa kuwapa pole wote waliokoka kwenye ajali hiyo ya kusikitisha na tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awapuguzie maumivu na awape nguvu na faraja.


Mwisho kabisa,WANACCM  tunapenda kutoa shukrani na pongezi za dhati kwa wote walioshiriki katika harakati za kuokoa maisha ya wahanga wa ajali hii na pia katika shughuli za kuopoa maiti. .Hakika mmefanya kazi kubwa sana na mwenyezi mungu atawalipa.AMINA


Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.


Kwa niaba ya VIONGOZI na  WANACCM wote CHUO KIKUU ARDHI
Katibu Siasa na Uenezi
Erick Godfrey Mkinga
+255 655 312 777 begin_of_the_skype_highlighting            +255 655 312 777      end_of_the_skype_highlighting

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...