Wiki imepita lakini machungu na kumbukumbu mbaya za ajali ya meli iliyoleteleza kupoteza maisha ya idadi kubwa ya watu bado bado vingali nasi.
Jumuia ya Watanzania waishio Edmonton, Canada, kupitia chama chao cha TANA (Tanzanian Community Association of Northernn Alberta), wanatoa rambi rambi zao za dhati kwa wote waliopoteza ndugu na jamaa katika ajali hiyo na pia wanatoa pole kwa wale waliojeruhiwa. Wanawaombea kupona haraka kwa walionusurika, licha ya kwamba itawachukua muda kuondokana na kumbukumbu za ajali hii na wanawaombea mapumziko mema ya milele wale waliotangulia.
TANA pia inatoa rambirambi kwa waliopoteza ndugu na jamaa katika ajali ya basi la Garzia iliyotokea eneo la Ubena Zomozi, Morogoro hivi majuzi na pia inawapa pole majeruhi wote wa ajali hii. Inasikitisha kuwa tunazidi kuwapoteza wananchi wasio na hatia katika ajali ambazo nyingi ya hizo zingeweza kuepukika. Tunaviomba vyombo husika vijaribu kuibadili hali hii.
TANA iko pamoja na wote walio katika majonzi.
Imetolewa na TANA Exec.
Edmonton, Alberta, Canada.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...