Mkurugenzi wa Elimu na Michezo Kimataifa (IESC),Brad Morrow akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jembo na Madarasa ya watoto wenye ulemavu wa akili katika shule ya Mshingi Kilimani iliopo Manzese,jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Anthony Valonge na kushoto (mwenye nguo nyekundu) ni Mwenyekiti wa DMHCSG,Mama Rahma Bomani.
Rais wa Rotary Klabu hapa nchini,Douglas Bramsen akizungumza na walimu wa Shule ya Msingi Kilimani pamoja na Wazazi wa watoto wenye ulemavu wa akili wasomao kwenye shule hiyo,wakati wa kukabidhi madarasa pamoja na Madawati kwa ajili ya wanafuzi hao ikiwa ni msaada uliotolewa na klabu hiyo na Taasisi ya Dar Es Salaam Mentally Handcapped children Support Group.
Baadhi ya Wanafunzi wenye ulemavu wa akili wanaosoma katika shule ya Msingi Kilimani wakiwa darasani pamoja na walimu wao wakati wa uzinduzi wa jengo jipya lililokabidhiwa rasmi leo.
Mmoja wa walimu wa shule hiyo,Mwl. Jane Massawe akimfundisha mwanafunzi wake wa hatua ya pili,Mbegu Mlawa katika darasa jipya lililozinduliwa leo.
Wadau wa Rotary Klabu ya jijini Dar wakiwa katika moja ya Madarasa ya shule hiyo mara baada ya hafla ya kukadhiana na uongozi wa shule hiyo uliofanyika leo.
Wadau wa Rotary Klabu ya jijini Dar wakiwa katika picha ya pamoja na wanafuzi wenye ulemavu wa akili.
Walimu wa Shule hiyo na Wanafuzi wao.
Wazazi la watoto zao.
Hongera Rotary Club kwa kufanikisha ujenzi wa madarasa yatakayotumiwa na ndugu zetu wenye ulemavu wa akili
ReplyDelete