ASALAAM ALEYKUM
Watanzania tuishio Uholanzi tumesikitika sana kupokea salaam za msiba huu mzito kwa taifa letu.Msiba ambao umesababishwa na kupinduka kwa Meli ya MV Spice Islander siku ya tarehe 10-09-2011,sisi kama sisi tumeona kua ajali hii imesababishwa na uzembe na tamaa ya pesa kwa baadhi ya watu wachache.
Kwa niaba yangu na wenzangu tungeomba mpokee salaam zetu za rambirambi na pole ndugu jamaa na marafiki zetu wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa msiba huu mzito.
Pia tunawapongeza na kuwashukuru wale wote walioonyesha moyo wa uzalendo kwa kutoa msaada wa hali na mali katika kufanikisha uokoaji, na uopoaji wa maiti.
Mwisho tunaungana na watanzania wote kuwaombea marehemu mwenyezi mungu awasamehe makosa yao, na awalaze mahali pema peponi. Na walionusurika Mwenyezi mungu awaponye na awape urahisi kwenye jambo hili zito kwa binaadam yoyote .
Shukran
M.Lunyungu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...