Wanamuziki wa bendi mbili za African Express na THE TANZANITES za Tokyo Japan, tunaungana na Watanzania wenzetu wote duniani kutoa salam za pole na rambirambi kwa ndugu zetu wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kufuatia ajali mbaya ya meli ya Mv Spice Islander iliyotokea usiku wa kuamkia tarehe 10/9/2011 huko Nungwi Unguja.

Tumepokea habari hizi kwa mshtuko na masikitiko makubwa. Tunawaombea wote waliopoteza maisha, Mwenyeezi Mumngu awapumzishe pema peponi. Pia wale wote waliojeruhiwa, Mungu awajaalie waweze kupona haraka na kurudi katika hali zao za kawaida.

Kwa wate waliofiwa, ndugu zao kujeruhiwa, kupotelewa na mali au kuathirika kwa namna yoyote ile kutokana na ajali hii, Mwenyeezi Mungu awape, nguvu, moyo wa subira na uvumilivu mkubwa katika kipindi hiki kigumu. Mungu atawapa na kuwaongoza.

Tunaamini kila jambo hupangwa na Mungu, na yeye ndiye atakaetuvusha na kutupa ushupavu wa kupambana na janga hili lililotufika sisi wote.

Poleni sana ndugu zetu.

Fresh Jumbe Mkuu
Kwa niaba ya wanamuziki wa bendi za 
African Express na The Tanzanites za Tokyo, Japan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...