Jumuiya ya wanafunzi Watanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha kimataifa cha Kimarekani (USIU) jijini Nairobi; Nchini Kenya imepokea kwa simanzi zito na masikitiko makubwa habari ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander Alfajiri ya tarehe 10 Septemba, 2011 ikiwa safarini kutokea Kisiwani Pemba kuelekea Kisiwani Unguja. Hakika ni janga zito kwa Taifa letu kwa ujumla.
Jumuiya ya wanafunzi Watanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kimarekani (USIU) jijini Nairobi nchini Kenya inapenda kuwasilisha salamu zetu za dhati kabisa za rambirambi kwa Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Viongozi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Wazanzibar na Watanzania wote kwa ujumla, Ndugu zetu wote waliopoteza Ndugu, Jamaa, Rafiki, Mzazi, Mwenza na kadhalika. Tunamuomba Mola atupe Moyo wa Ustahimilivu na Imani ya kuweza kupita katika kipindi hiki kigumu kwetu sote.
Tunamuomba Mola aliye mwingi wa rehema awalaze Ndugu zetu mahala pema peponi. Pia, tunawaombea majeruhi wote wa ajali hii ya kusikitisha waweze pona haraka na kurejea katika shughuli za kujenga taifa. Amin.
Inna Lillahi wa Inna Illahi Rajuun.
Glen S. Kapya
Mwenyekiti
Jumuiya ya Watanzania
Chuo cha Kimataifa cha Kimarekani (USIU)- Afrika


Napenda mshikamano na upendo huu tulionao Watanzania. M/mungu atuunganishe sote milele tuzidi kupendana kwa amani, furaha na majonzi.
ReplyDeleteIla kwa kurekebisha ni kwamba LCT Spice Islander imepata ajali ya kupinduka na kuzama mkondo wa Nungwi ikiwa safarini kutoka zanzibar(Unguja) kuelekea Pemba. na sio kama mulivyoandika ikitokea kisiwani Pemba kuelekea kisiwani Unguja.
Naomba mupokee masahihisho haya.
mimi ni mtu kutoka tanzania bara lakini kwa muda wa miaka 2 naishi huku tanzania visiwani..hakika watanzania wote kwa ujumla wana umoja, basi tu sijui vipi. nimekuwa nikiperuzi kurasa ktk mtandao, salamu nyingi sana za rambirambi kutoka kwa watanzania walio nje ya nchi zimesha wasilishwa na zinaendelea kuja. hili si dogo yapaswa tujivunie...HIYO MELI ILIKUWA INATOKA UGUJA KWENDA PEMBA NA SI KUTOKA PEMBA KWENDA UNGUJA KAMA MLIVYOANDIKA...LAKINI YOTE TISA, KUMI NINA IMANI SALAMU ZENU ZIMESHAPOKELEWA NA MIMI KAMA MTANZANIA NIMEZIPOKE...nawaomba radhi kwa kuanza na t badala ya T kama nchi yangu, si makusudi bali ni uharaka tu....wasalamu
ReplyDeleteOn behalf of the Committed Youths for the Poor (C.Y.P),Loyola High School,I extend my condolence message to Tanzanian President, President of Zanzibar, Leaders and my fellow compatriots of United Republic following GRIEF reigned across the spice islands of Unguja and Pemba after the ferry accident that lost our dear friends, relatives and others their dear loves.
ReplyDeleteWe Tanzanian C.Y.Ps at LOYOLA HIGH SCHOOL join our hands in this sorrowful time when our National flag will fly at halfmast.
God Bless Tanzania,God Bless us ALL.
Elias Manaseh Mwana
COORDINATOR C.Y.P, Loyola High School
HEADBOY 2010-2011,Loyola High School