Ofisi ya Rais; Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China inaendelea na mpango wake wa kuwapatia mafunzo maafisa wakuu wa Serikali kupitia Ushirikiano wa Kiufundi na Kiuchumi uliotiwa saini kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Watu China.
Mafunzo hayo ni ya awamu ya tatu ambayo yatahusiana na Usimamizi wa Rasilimali Watu (Human Resource Management) ambayo yatawashirikisha Wakurugenzi na baadhi ya Maafisa waandamizi ishirini na nne( 24) kutoka Wizara na Taasisi mbali mbali za Serikali ambao wanasimamia Rasilimali Watu na waandishi wa habari wawili(2).
Aidha, mafunzo hayo yatakua ni ya siku ishirini(20) na washiriki pia watapata fursa ya kutembelea maeneo mbali mbali ikiwemo ‘Beijing Urban Planning Exhibition Centre’ na kufanya majadiliano na ‘Xiangan High-Tech Development Zone’ ya mji wa Xiamen. Washiriki hao wanatarajia kuondoka Nchini siku ya tarehe 16 Sepemba, 2011 na kurudi siku ya tarehe 9 Oktoba, 2011.
Sikina H. Salum,
Afisa Mawasiliano,
Ofisi ya Rais - Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo,
Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...