Kama Mtanzania,niliezaliwa Zanzibar,nilieshtushwa na kusononeshwa sana na ajali iliotufika,msomaji sana wa blogs za nyumbani Tanzania, naomba kwa dhati kabisa kumpongeza sana KAKA MICHUZI NA TIMU YAKE kwa kiwango kikubwa cha urushaji wa habari ya ajali ya meli huko Zanzibar na habari zingine mbali mbal.
Binafsi nimefurahishwa sana kuona blog hii inaongoza kutoa habari hizi ukilinganisha na nyengine zote,naomba nitoe dukudukulangu hili la kukupongeza kaka Michuzi na timu yako.
Hii ndio inavyotakiwa wakati linapotokea jambo kama hili.Na mchezakwao hutunzwa. Mungu awape nguvu zaidi,moyo wa dhati na uwezo zaidi,hasa katika mambo yanayoigusa jamii mojakwamoja badala ya siasa tupu.
Asante sana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...