Wasanii wa muziki wa asili walioshiriki Tamasha la tatu ta Mtemi Milambo mwaka huu lililofanyika Julai 8-10,201 katika viwanja vya Uyui sekondari Tabora na kufunguliwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mhe.Abeid Mwinyimussa wamepata udhamini wa kurekodi nyimbo za muziki wa asili za makabila ya Kisukuma na Kinyamwezi.

Wasanii waliofanya vizuri mwaka huu Ali Mango,Asha Kaombwe,Hamis Mpiga,Paulina Muhala,Paul Magadala wataungana na wasanii wengine wa miaka iliyopita na kuunda bendi ya muziki wa asili iitwayo Mwana Milambo ambayo itakuwa inapiga muziki huo katika mahoteli,maharusi na kumbi mbalimbali za burudani.

Nyimbo zitakazorekodiwa ni Kamnyagara kane, Usoga wi kuwa, Kushoke kukaya, kana nabuta, Sensema malunde, Ng,ombe yalala, Wela wa kulya, Nzagamba ya Sukuma na Miaka hamsini ya Uhuru

Lengo kuu ni kuzihifadhi nyimbo mbalimbali zilizotumiwa na wazee wetu wa kale katika vita, kilimo, harusi,na mazishi.

Nyimbo hizi nyingi huimbwa sehemu mbalimbali lakini ni muhimu kuzirekodi kwa ajiri ya faida ya vizazi vya baadae. Nyimbo hizo zote zitarekodiwa katika studio ya Aegies chini ya muandaaji maarufu Peter John a.k.a Nice P.
  
Amon Mkoga
Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions.
www.chiefpromotions.or.tz
0755 638 004/0655 638 004 begin_of_the_skype_highlighting            004/0655 638 004      end_of_the_skype_highlighting

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...