Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mgeni Baruani, akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tisa , yaliyoanza Septemba 20, mwaka huu mjini Morogoro kwa wadadisi wa sensa ya majaribio ya watu na makazi ya mwaka 2011 kutoka baadhi ya mikoa iliyoainishwa kwa zoezi hilo, linalotarajia kuanza Oktoba 2, mwaka huu na kuandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu , ( kushoto ) ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo, Aldegunda Komba.
Washiriki wa mafunzo ya wadadisi wa sensa ya majaribio ya watu na makazi ya mwaka 2011 iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakimsililiza kwa makini Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mgeni Baruani, ( hayupo pichani) wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tisa yaliyoanza Septemba 20, mwaka huu kwa wadadisi hao wa kutoka baadhi ya mikoa ya iliyoainishwa kwa majaribio hayo yanayotarajia kuanza Oktoba 2, mwaka huu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mgeni Baruani, (wapili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki na mafunzo ya siku tisa ,yaliyoanza Septemba 20, mwaka huu mjini Morogoro kwa wadadisi wa sensa ya majaribio ya watu na makazi ya mwaka 2011 kutoka baadhi ya mikoa iliyoainishwa kwa zoezi hilo, linalotarajia kuanza Oktoba 2, mwaka huu na kuandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu , ( wa kwanza kulia ) ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo, Aldegunda Komba.Picha na John Nditi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...