Jengo la Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam lenye Ukumbi wapili  wakisasa wa Maonesho Tanzania.
 Sehemu ya nje ya Ukumbi wa Maonesho ya Jukwaani. Wasanii na watanzania kwa ujumla wategemee mambo mazuri muda si mrefu.
 Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt Paul Msemwa Kushoto akisema jambo kwa Wataalamu wa Makumbusho wanaoshirikiana na Wale wakutoka Sweden. Ukumbi huu utaweza kuchukua watu 500 
 Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt Paul Msemwa mwenye shati jeupe akishuhudia zoezi la Ufungaji wa Vifaa vya Sauti na Mwanga katika Ukumbi wa Makumbusho wa Maonesho ya Jukwani
Wataalamu kutoka Sweden wakishirikiana na wataalamu wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam wakifunga vifaa vya Mwanga na Sauti katika ukumbi wakisasa wa Maonesho ya Sanaa.Picha na Mdau Sixmund Begashe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Safi, safi, safi sana!!! Sekta isiyo rasmi ni ajira kubwa. Tukimaliza hili tuelekeze nguvu kwenye kuzuia wizi wa kazi za wasanii. By the way, huu ukumbi unabeba watu wangapi?

    ReplyDelete
  2. Nimekuwa impressed with huu ukumbi I guess kwanza ni wa serikali si sekta binafsi and kama mtoa mada moja sasa tuelekeze nguvu kwenye kazi za wasanii sasa ili sanaa iwe moja ya njia kwa pato la taifa

    ReplyDelete
  3. Swali la dhati, sio kizushi: ubunifu wa hili jengo umeakisi kwa kiasi gani utamaduni wa Kitanzania (mchanganyiko wa tamaduni za makabila)?

    ReplyDelete
  4. KAZI NZURI SANA DKT. MSEMWA, UTAACHA LEGACY ITAKAISHI MILELE NA MILELE KWA WASANII NA WATANZANIA WOTE. HII NDIO DEFINITION YA UZALENDO N KUIPENDA NCHI YAKO - UNAPOKUWA KATIKA NAFASI YA KULETA MABADILIKO KUSAIDIA WENGI UNAITUMIA KWA MOYO WOTE BILA KUJIFIKIRIA BINAFSI.

    SIO WALE JAMAA WA MFUKO WA UTAMADUNI, WANGECHAKACHUA HELA ZOTE ZA MRADI HALAFU WAJENGE KIDUDE CHA KUEZEKA KWA MANYASI KUWADANGANYIKA WATU! SHAME ON THOSE CREATURES!

    ReplyDelete
  5. Ni kazi nzuri sana uliyofanya Dr. Msemwa. Tunakupongeza sana. Achana na na wenye roho mbaya wasioona jitihada zako, hao ni MAFISADI walitamani wawe wao waufisadi Mradi. Kaza buti baba simamia mradi huu hadi mwisho

    ReplyDelete
  6. Watanzania wenye moyo km wako Dr Msemwa ni wachache tumeuona uzalendo wako na wale waliotaka kukuhujumu sasa wanaaibika Tunakuhitaji uwe na moyo wa kuto kata tamaa. Tunakupongeza kwa moyo wako wa uvumilivu. Watanzania tuutumie ukumbi huu wa kisasa ipasavyo kwa manufaa yetu..

    ReplyDelete
  7. HONGERA SANA Dr MSEMWA KWA KUSIMAMIA VYEMA MRADI HUU MUHIMU KWA MASLAI YA TAIFA LETU, WEWE NI MMOJA KATI YA WACHAPAKAZI MAKINI WA KATIKA SERIKALI YETU. NAAMINI HAPO WAPO WENYE UBINAFSI WALITAKA KUWEKA MAMIKONO YAO HUMO ILI KUKUARIBIA LAKINI WATASHINDWA TU. UMETUBEBA WASANII BABA. HONGERA KWA SERIKALI YETU KWANI KATIKA JAMBO LAKIISTORIA LILILO WAHI KUFANYA NI PAMOJA NA HILI LAKUTUPA UKUMBI HUU. WASANII TUJIPANGE SASA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...