Ndugu Ankal Michuzi,
naomba usiitie hii habari kapuni kwani ninalotaka kuongea hapa ni mfano mdogo tu wa mambo mengi ya namna hii yanayotokea nchini hadi sasa inaonekana kama vile ni kawaida. wakati fulani mambo kama haya yanatokea katika shughuli ambazo ni nyeti sana kitu ambacho kimeanza kutoa picha na kuonyesha kuwa watanzania tumesha kuwa watu wa hovyo hovyo tu!
Sitaki kuzunguka kichaka ni bora nikikabiri. Suala lenyewe kwa kuzingatia uzito wake ni sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Mimi nina ndugu yangu (simtaji jina hapa) amechaguliwa kuwa mmoja wa wakufunzi watakao fundisha vijana wa halaiki kwa ajili ya sherehe hizi hapo tarehe 9/12/2011.
Kwa sasa wakufunzi hawa wakitanzania wanapewa mafunzo zaidi na wataalamu kutoka Uchina kabla hawajaanza kazi ngumu na muhimu ya kuwafundisha vijana. Hawa wakufunzi wa kitanzania wamekuwa wakitumiwa katika maandalizi ya halaiki katika sherehe nyingi za kitaifa na za chama cha CCM.
Ni watu wazima wenye umri na heshima zao lakini wanafanya kazi kwa kujituma, uadilifu na kwa kutambua kuwa wanalitumikia taifa kwa maana hiyo hawajaweka maslahi ya kifedha mbele. Wanafanya mazoezi magumu kila siku kuanzia asubuhi ya saa tatu na kumaliza saa kumi.
Haya mazoezi yataendelea hadi hapo zitakapotimia wiki tatu hapo mwisho wa mwezi wa kumi, na baada ya hapo kuanzia tarehe 1/11/2011 wataanza kufanya kazi na vijana.
Kabla hawajaanza mafunzo haya kuna watu kutoka serikalini waliwaambia kuwa baada ya kukaa kikao na kufanya maamuzi wameona kuwa itakuwa vyema kwa wakufunzi hawa wa kitanzania kulipwa Tsh 50,000 kwa siku hadi tarehe 9/12/2011.
Hayo ni malipo ya kila kitu ikiwa ni pamoja na chakula na nauli ya kwenda kazini na kurudi majumbani kwao. Sasa cha ajabu ni kwamba tangu wameanza mafunzo haya hawajalipwa kitu.
Cha kushangaza ni kwamba hata kabla hawajalipwa Tsh50,000 kama walivyoahidiwa waheshimiwa wanaosimamia maandalizi haya wamekuja kuwaambia kuwa sasa kuna mabadiliko baada ya maamuzi kufanyika katika kikao ambacho waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda alikuwepo. Mabadiliko yenyewe ni kwamba sasa watalipwa Tsh10,000 kwa siku, kwa wiki tatu, na kisha watalipwa Tsh 50,000 kwa wiki ya mwisho watakayofanya kazi na vijana.
Swali ni kwamba hivi watanzania tumerogwa? Hivi ni nani asiye na ubinadamu aliyekaa kwenye kikao na kuamua kuwa mtu mzima mwenye ujuzi wake, mwenye familia, anaye shinda kutwa nzima akifanya kazi nyeti kama hii anaweza kulipwa Tsh 10,000 kwa siku? Katika zama hizi za maisha aghali kama haya elfu kumi inakusaidiaje! Hivi kweli waziri mkuu anafahamu kuwa mabadiliko haya yamefanyika?
Kuna maswali mengi sana ya kuuliza hapa na ninaimani wakufunzi hawa pamoja na ndugu yangu wanaogopa kulalamika, kugoma au kulipeleka mbele. Wameambiwa sherehe hizi zinasimamiwa na ikulu moja kwa moja na ukisha taja ikulu basi :)
Wanafanya kazi kwa unyonge wakijua kuwa kuna mizengwe hapa wanaendelea kufanya kazi ingwa wakirudi majumbani wana lalamika sana na kusema wanaonewa lakini hawana mtetezi. Hivi Tanzania ya leo imekuwa ya kula! kula! kula! kula! kula tu! bila hata kufikiria nini madhara yake siku za usoni. Hivi watu serikalini mnafikiria vipi kama wananchi hawatakuwa na imani na serikali yao?!
Sherehe hizi tungependa ziwe ni za kihistoria na kivutio hata kwa watu wa nje kwani hii ni nafasi ya pekee kabisa. Tanzania haitakuja kuwa na miaka hamsini tena.Kama hawa wakufunzi hawajaridhika tusishangae halaiki ikajakukosa kiwango na tuka aibika. Hii kauli mbiu ya 'TUMETHUBUTU,TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE' iwekeni katika vitendo kwani kama mambo ndiyo haya tutakuwa 'hatuja weza kitu na hatusongi mbele bali tunajirudisha nyuma''.
Ni AIBU kumdhurumu hata mwenye kiduchu. Kama hili halitashughulikiwa tutafanya kila liwezekanalo ili ujumbe uweze kufika kwa kila mtu atakaye hudhuria sherehe hizi za miaka 50 ya uhuru tarehe 9/12/2011 ikiwa ni pamoja na mkuu wanchi. Naomba magazeti yafuatilie ufisadi huu na kuwatetea wavuja jasho hawa.
Kwa leo naishia hapa.
Ni mimi Morris
Wakati mbunge anasizia bungeni anakula laki kwa siku. Hiyo inaitwa aliyenacho anaongezewa na asiye nacho ananyang'anywa hicho kidogo alichonacho!!
ReplyDeleteJamaa wamekula na wewe unalilia kula Tanzania hakuna kujenga nchi wala kufanya kitu kwa maslah ya nchi nikula na kijilimbikizia basi!!
ReplyDeleteBwana Michuzi kwa heshima yako naomba hii kitu ujaribu kuitafutia ufumbuzi wa kuitangaza kiaina ili tu watu wapate picha kamili si wote wanaoingia internet na wakiingia net wana facebook tu hawasomi mambo yanayoendelea nchini kwao ili ni jambo la aibu alafu serikali inasema eti maisha bora kwa mtanzania kulipwa elfu kumi wakati matumizi ya ndani leo hii yanazidi elfu kumi hii sio ishu kabisa then kuna ishu nyingine ya kwamba kuna pesa ambayo imetolewa na serikali kwa wale wanaoishi nje ya tanzania wote wakutane kusherekea siku hiyo ya miaka hamsini ila bado tunaambawa kuchangia tena kidogo hii ndio inamaanisha nini mi nipo kenya
ReplyDelete