Ankal habari,
Kwa heshima kubwa naomba utoe kilio chetu kupitia blogu yetu ya jamii, kuhusu mabosi wetu tunaofanya nao kazi.
Sisi watumishi kada ya usekretari tunapata shida sana tuwapo ofisini Kama ifuatavyo:-
Kwanza ni kuchelewa kutoka kazini baada ya muda wa kazi.
Unakuta bosi anamkalisha ofisini Sekretari, hadi saa tatu usiku tena bila kazi yoyote ya msingi ili mradi tu bosi bado hajaondoka. Na hii ni kila siku.
Na muda huo bosi akitoka anaaga “haya tutaonana kesho”. Bila kujua huyo aliemkalisha mpaka usiku wa saa 3 usiku au zaidi atafikaje kwake. Wengi wanadhurika ikiwa ni pamoja na kuporwa na vibaka.
Muda mwingine bosi anatoka wakati wa muda wa kazi, anarudi tena ofisini saa 9 au 10 alasili, ndio anaanza kazi hadi usiku.
Tatizo linakuja kwa wenye familia, tukitoka muda huo, mpaka kufika nyumbani ni saa 4 usiku au 5. Tukifika tuko hoi, hata tukidaiwa kile chakula cha usiku tunakuwa hatuwezi. Sasa hii inachangia kutuvurugia ndoa.
Kwani tumekuwa tumechoka sana kiakili na kimwili hasa Ukizingatia tunatakiwa kuwahi ofisini kabla mabosi hawajafika hiyo ni saa 12.00 asubuhi hadi moja kasoro. hilo sio tazito, tatizo linakuja kwenye muda wa kutoka.
Ombi letu kwa mabosi ni kuwa watufikirie na sisi kuwa ni binadamu na tuna familia zetu hasa watoto wanatuhitaji. Hivyo tunaomba ikifika saa 11 jioni turuhusiwe kurudi nyumbani. Basi tukicheleweshwa sana isipite saa 12 jioni.
Unakuta mabosi wengine hawana wenzi (Mke/mume) hivyo hawaoni umuhimu wa kuwahi kurudi nyumbani.
Pili, Siku za Mwisho wa wiki (weekend)
Ni siku za kupumzika ili jumatatu tuwe fresh kiakili. Lakini kwa sisi ma sekretari hilo hatuna. Tunatakiwa kuja kazini hata bila sababu za msingi, tena muda wa kutoka hata siku za weekend ni saa 12 jioni tukiwahi saa 10. jamani tuonewe huruma. Hii inachangia kutofanya kazi kwa ubora.
Mama Mh. Hawa ghasia sikiliza kilio chetu.
Wadau wa Blogu ya Jamii


No comments yet
ReplyDeleteaisee! ulijuaje? tena unaweza ukakaa usiku wote huo, unamchapia kazi zake binafsi za kampuni zake we acha tu! nasome kozi nyingine nibadilishe kazi sekretari wewe, muhudumu wewe, yaani we acha tu unachemsha maafisa machupa ya chai mpaka 10 kisa we ni sekretari wo, nga mchoka mae, nga mshindwa kabsa, kuchukuchu
ReplyDeleteKwa muda mrefu nchi ilikuwa ikiendeshwa kidikteta kwa hivyo utamaduni wa kufanyakazi TZ umekuwa wa kidikteta. Hii ni katika kila sehemu ya kazi. Hata wewe sekretari nawe unajifanya bosi kwa mgeni anayetaka kumuona bosi wako. Utamaduni wa kufanya kazi TZ bado ni wa kienyeji. Masaa ya kazi ni 1.30-9.30 zaidi ya hapo ni maamuzi ya mtu. Hii haina maana kama hukukaa masaa zaidi ndio ufukuzwe kazi au usipewe mafunzo na mafao mangine. Tatizo kubwa nchi yetu haifati sheria ndio kila mwenye nafasi ya kazi anafikiri ameshakuwa mungu mtu. Awe bosi, sekretari, trafiki, mapokezi, masjala, afisa mafunzo, mbunge, waziri, rais wote ni sawa. Nchi inataka mageuzi ya makubwa sana.
ReplyDeleteMdau hii mada uliichelewesha wapi? yaani jamani kwa kweli Hawa Ghasia liangalie hili, ndoa zetu zimekuwa hatarini kwa ajili ya maboss kuchelewa kutoka kazini, wakati mwingine hana hata kazi, amekaa tu anaangalia internent, basi utasubirii wee, mpaka atakapojisikia kuondoka, ndo anaaga tutaonana kesho, basi hapo ujijue usafiri, Mama Hawa Ghasia lifikirie hili kwa undani kabisa, uwaeleze hawa maboss wetu.
ReplyDeleteDuh!
ReplyDeleteSasa kwanini hamna ujasiri wa kuwaeleza mabosi wenu hayo yanaywasibu? Chaguo ni lenu mwaweza pima panapo zidi uzani ndipo mwelekee athi.
ReplyDeleteacha kazi
ReplyDeletehuyu mama anasomeka kama mtu aliyelazimishwa kufanya kazi, kama kazi hailipi achia ngazi mama. wako vimwana mahsususi, wataichangmkia mara moja!! upo hapo??
ReplyDeleteHao vimwana wa siku hizi kazi kuuza sura, hawajui kazi, wanajidai eti wana diploma, hawajui kutunza siri za serikali/makampuni/mashirika. Masekretari walikuwa wale wa enzi za mwalimu sio sasa na hao maboss utakuta ni vijana tu, enzi zile time ilikuwa inafuatwa, na mtu akikaa zaidi ya saa za kazi boss anatumia lugha nzuri ya kumuomba kubaki amalizie hiyo kazi. Siku hizi utamaduni wa kuheshimiana umekwisha kabisa, sijui tunaelekea wapi.
ReplyDeleteAt least labda kwa sababu mume wangu na bosi wangu wote ni wateja wa MICHUZI BLOG tatizo hili nitakuwa nimelitatua kiaina, maana ni kasheshe! ...Thanx again kwa mtoa mada.
ReplyDeleteTunaomba wakati wa kukaa kazini tuangaliwe na usafiri wa kurudi majumbaji kwetu. maana karibu wote ni wana mama na ni hatari kwa kuweza kukabwa au kukabwa njiani usiku. Tuandikie waraka wa kueleweka wa kutoka kazini siyo kila siku usiku tu saa 3 mpaka hata saa nne
ReplyDeletemama Hawa kujali sisi wote
My dears, Makatibu wahutasi, Mie nililiona mapema nikapunguza shughuli zote za starehe na kuanza kujiendeleza maana niliweka nadhari sitamtengenezea tena bosi yeyote chai nifikikapo miaka 30. My dear nimeweza
ReplyDeleteUshauri
Kwa wale vijana naomba wajiendeleze na masomo mbalimbali wajikwamue inawezekana pale ukiweka nia.
Kazi za u-sekretari zimebaki zaidi maofisi ya serikali hivyo hakuna haki ofisi nyingi bosi anajua kila kitu haitaji msaidizi.
wale wenye umri endeleeni kupigania haki yenu inawezekana kujikwamua.
Ni mimi sekretari wa zamani sasa ni bosi fulani.
unajua tatizo hili limebaki katika ofisi za serikali ambapo kuna watu wa kada mbili wasekeretali na madereva hao wanajua muda wa kutoka majumbani mwao awajui muda wa kurudi makwao,sasa dereva anakaa majohe bosi anakaa mbezi mwisho,inamlazimu dereva kuwa anaamka kabla ya adhana ili kumuwahi boss.mm nadhani hawa watu wangeangaliwa katika hali nya kipekee,ofisi iwe na mabasi watu wafanye kazi ikifika saa 11 dereva unapaki gari funguo unakabidhi unasepa boss kutoka ofisini kurudi kwake atumie ile gari tuliyomkopesha kama si kuufutia ushuru
ReplyDeletepoleni masekretari. mimi nilikuwa sekretari ila niliichukia kutokana na kusumbuliwa na maboss kwa kutaka rushwa ya ngono. boss alitaka kunifukuza kazi kwa kukataa kutembea nae. kwa kweli hiyo ilinifanya niichukie kazi ya usekeretari. Kwa vile nilikuwa na msimamo alishindwa kunifukuza ila nilipata vitisho vingi. sitamani kufanya kazi hiyo tena. niliacha nikiwa na umri mdogo na kuamua kufanya shughuli zangu mwenyewe.
ReplyDeleteNilikuwa sijui mambo ya usrkretari bado yapo Tanzania. Kwanza kwenye ulimwengu huu wa sayansi na Tekinelogia sekreteri hana kazi. Nchi zetu ni masikini lakini zina ajira za ajabu zilizo pitwa na wakati. Na fikiri kwenye Organization kubwa labda mtendaji mkuu ndiyo anahitaji sekretari jaribuni kubana matuminzi kwani ukitaka kuandika barua ya aina yoyote uta upload kwenye kumpyuta hata ukitaka ku tengeneza Cv haiitaji utaalamu utapata kwenye kompyuta yako kazi yako ni kusoma Word na Excel itakusaidia huhitaji kujua kompyuta kiivyo inatosha
ReplyDeleteacheni ukiritimba wa kutengeneza ajira zisizo na maana, kuhusu bosi kumkorogesha sekretari wake chai huo ni upuuzi kwani bosi mwenyewe hawezi kujitenenezea chai?