Kituo cha utafutaji na uokoaji majini (MRCC) kinachoratibiwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), kimepokea taarifa za kushambuliwa kwa meli ya utafiti wa mafuta iitwayo Ocean Rig Poseidon.
Tukio hilo limetokea tarehe 3/10/211 saa 2:15 usiku, umbali wa maili za baharini 23 kusini mashariki ya kisiwa cha Mafia sawa na maili 82 kutoka Dar es salaam.
Tukio hilo limetokea tarehe 3/10/211 saa 2:15 usiku, umbali wa maili za baharini 23 kusini mashariki ya kisiwa cha Mafia sawa na maili 82 kutoka Dar es salaam.
Katika tukio hilo maharamia 7 waliokuwa katika boti ndogo waliishambulia meli hiyo kwa silaha. Mashambulizi hayo yalijibiwa na walinzi wa meli na Jeshi la Wanamaji wa Tanzania na maharamia walidhibitiwana kukamatwa na wanashikiliwa mikononi mwa jeshi la Wanamaji.
Imetolewa na:
E.S Wapalila
K.n.y: Msajili wa Meli
kazi nzuri sana waliofanya ulinzi hapo hii habari itapeleka ujumbe hatutaki maharamia huku
ReplyDeleteDuuuh hawa jamaa sasa wamezidi! Nafikiri sio wasomali peke yao lazima kuna mikono ya watu wengine.
ReplyDeletehao ni kuwadhibiti tu haiwezekani wakatuchezea namna hii lazima wachukuliwe hatua madhubuti
ReplyDelete