DJ mkongwe kuliko wote nchini, Seydou, bado anaendeleza libeneke na hivi sasa ile midundo uliyokuwa unaipata RSVP Discotheque (Mbowe hotel) enzi hizo kaihamishia kiota cha maraha cha Fairways kilichopo Tegeta Namanga, kiasi cha nusu kilomita hivi toka njia panda ya Wazo hill katika barabara ya Bagamoyo. Ukitoka mjini iko upande wa kulia. Hapo ma Old Skul ya ukweli yote unayoyajua utayapata kila weekend kuanzia Ijumaa. Kama unatafuta Old Skul na DJ halisi wa mangoma hayo tembelea Fairways utabroo...
 "....Unaikumbuka hiyooo??" DJ Seydou akimuuliza Ommy Sydney, bingwa wa kucheza disko enzi hizo, wakati kibao cha 'Love is Contaigious' cha Taja Sevelle (BOFYA HAPA) cha mwaka 1988 kilipokuwa kinapigwa. Maveteran wengi wa Old Skul ya Bongo huwakosi hapo Fairways
Meza kuu ya Fairways wakiwa na mwenyeji wao (wa pili shoto) pamoja na Papaa Freditto (kati) na Mzee mzima  wa Break Point Club Alison (wa pili kulia) na wadau. Hapo hakuna kinachoharibika....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. OMMY SIDNEY YUPO WAPI JAMANI. HUYU MTU ALIKUWA NI MKALI SANA WA DISKO ENZI ZAKE. MCHIZI ALIKUWA ANATUTESA SANA MTAANI NA VIATU VYA MATAITI. ENZI HIZO ATA KANDAMBILI ILIKUWA ISSUE. MKUBWA KAMA UPO SALAM SANA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...