Mtoto Cecilia wakati akiwaomba wasamalia wema waweze kumsaidia.

Mtoto Cecilia alitangazwa hivi karibuni na Vituo mbali mbali vya habari akiomba msaada wa kusaidiwa pesa za matibabu ambazo zingeweza kumwezesha kufanyiwa operesheni ya moyo ambao umempelekea mpaka Tumbo lake kuvimba kama unavyoliona.

Taarifa za Cecilia ziliweza kutolewa na Miss Tanzania wa mwaka 2009 Bi .Hoyce Temu pale alipoamua kujitokeza na kumtangaza Cecilia akiomba msaada huo. 

Wasamaria wema walijitokeza na kumsaidia Cecilia mpaka akaweza kwenda India kwa matibabu, cha kusikitisha sana ni kwamba matibabu yake kwa njia ya operesheni yameshindikana kutokana na moyo wake kwa upande mmoja kuathirika na sumu ambayo madaktari wa India wamesema inasababishwa na Sumu ambayo ipo kwenye Mihogo, sumu hiyo huwaathiri sana watoto wenye umri kama wake.

Kwa hiyo imekuwa ni vigumu kumfanyia operesheni hiyo, wakashauri atumie dawa tu ili kuweza kuitoa sumu hiyo, Mtoto Cecilia mpaka sasa hali yake sio nzuri anawaomba watanzania mumuombee ili aweze kupona na aweze kutimiza azma yake ya kuwa Mwalimu. 

Watanzania tunashauriwa tukiona hali ambayo ni tofauti kwa watoto wetu tuwawaishe Hospitali mapemakwa uchunguzi tunaweza tukawahepusha na hali kama hii aliyofikia Cecilia.
Hapa Mtoto Cecilia akitoka Hospital ya Regency Dar akiwa ameshikwa mkono na afisa mmoja wa Channel Ten tayari kwa kuelekea Airport kuanza safari ya kwenda India.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Pole sana na inasikitisha kweli kweli. Nimekuombea na nitaendelea kufanya hivyo. Nguvu za mwenyezi mungu zitafanya mahajabu, na upone mapema, Amen.

    ReplyDelete
  2. Pole sana. Mola atafanya miujiza yake na utapona.Tunakuombea.

    ReplyDelete
  3. Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike ,Duniani kama mbinguni,utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu kama tunavyo wasamehe na sisi wale waliotukosea, usitutie katika vishawishi lakini utuopoe maovuni, amen.
    Mungu aliye kuumba na ndiye Daktari mkuu atakuponya, kwakuwa imeandikwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu, amen.

    ReplyDelete
  4. Hali hii inasikitisha kwakweli... Ningependa kujua madaktari wetu nyumbani nao wanasemaje; je hali hii (sumu ya muhogo) imekwisha jitokeza kwa watoto wengine? Je kuna madaktari ambao wako willing kuifuatilia "case" hii? Just wondering!

    ReplyDelete
  5. Michuzi.
    Najua kuna uwezekano wa huyo binti kutibiwa kwenye nchi zilizoendelea kama vile U.K, USA, EUROPE etc. Kama inawezekana endelea kutuhamasisha kuchangia gharama za huyo binti ili watanzania tuchange aweze kupona. Ahsante.

    ReplyDelete
  6. yestu ni afya ya wagonjwa, yesu ni mtenda miujiza. Ee Mtakatifu Yuda Mtenda miujiza haijasika kamwe ulimuacha mtu aliyeomba msaada kwako nasi kwa matumaini hayo tunakuomba Mt. Yuda Tadei ukamtendee binti huyu naomba nyoosha mkono wako kwa binti huyu tuma malaika wako amsimamie na kumponya. Amen. Inauma sana, jamani nimeumia sana mimi...Ee mwenyezi mungu tunaomba umsaidie umpiganie roho yake apone Amen.

    Frida

    ReplyDelete
  7. Damu ya Yesu husafisha kabisa, shetani na magonjwa ameshindwa!

    ReplyDelete
  8. Eee Watanzania haishindikani kumchangia mtoto huyu aende hata nchi nyingine ili aweze kupona jamani,tunaomba ufanyike utaratibu kama kuna baadhi ya nchi wataweza kutibu ili kuokoa maisha ya mtoto huyu jamani' inauma jamani hebu ufanyikw utaratibu na Watanzania tujitoe kwa roho moja kuchangia.
    Ee Mungu mwenye nguvu zote wewe uliye mkuu wa yote naomba kwa aajili ya mtoto cecilia ufanye uponyaji kwa ajili yake na arudi ktk hali ya kawaida ili aje kutimiza ndoto zake nzuri za kuwa mwalimu.AMEN

    ReplyDelete
  9. Eee Watanzania haishindikani kumchangia mtoto huyu aende hata nchi nyingine ili aweze kupona jamani,tunaomba ufanyike utaratibu kama kuna baadhi ya nchi wataweza kutibu ili kuokoa maisha ya mtoto huyu jamani' inauma jamani hebu ufanyikw utaratibu na Watanzania tujitoe kwa roho moja kuchangia.
    Ee Mungu mwenye nguvu zote wewe uliye mkuu wa yote naomba kwa aajili ya mtoto cecilia ufanye uponyaji kwa ajili yake na arudi ktk hali ya kawaida ili aje kutimiza ndoto zake nzuri za kuwa mwalimu.AMEN

    ReplyDelete
  10. Pole cecilia na kuombea kwa mungu upate afya njema na kurudia hali ya kawaida.

    ReplyDelete
  11. kaka kuna sheikh mmoja yupo mkuranga kwa muarab anaitwa sheikh maramba, haitaji hela yoyote na kama magonjwa yako ni ya kutibiwa hospital anakwambia, nakuomba michuzi nakuomba kaka yangu vunja kazi zako siku hii moja mpeleke, mimi dada yangu alishindikana kutibiwa hospital na nikampeleka pale sasa ni mzima, ningekuwa nipo tanzania ningejitolea mimi mwenyewe siku yangu moja kumpeleka hapo, tafadhali kaka michuzi usidharau tafadhali niko chini ya miguu yako nakuomba mpeleke hapo na wallahi utakuja kuona maajabu, inapaswa ufike pale mapema mno kama saa kumi na moja alfajir, kaka nenda, kama umebanwa nenda jumapili, jamani dunia imejaa miujiza na huyo sheikh mwenyezi mungu amemjalia, aminini hakuna lisilowezekana kwa mungu, kwake huyo sheikh haitaji pesa yoyte, kaka kwa jinsi alivyowasaidia watu laiti kama angekuwa anachukua pesa basi asingekuwa na maisha aliyonayo, kwake huyo sheikh kikwete ni sawa na wewe, kama atakwenda nae atapanga foleni kama unavyopanga wewe, huko hakuna muarab,muhindi wala mwafrika, yani wote mko sawa na haki zenu ziko sawa, nenda kaka mkuranga wala si mbali ni nusu saa tu umefika tena kabla haujafika mkuranga mjini, naumia sana niko nje ya tanzania laiti ningekuwepo ningempleka mwenyewe kaka, simfanyiii promo kaka ni miujiza ambayo mimi nimeishuhudia kwa dada angu tena bila ya kutoa hata senti kaka,TAFADHALI MICHUZI MPELEKE HUKO HUYU BINT!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  12. Pole sana mdogo wetu Cecy. Hakuna kinachoshindikana kwa M/Mungu na Tuombe bila kuchoka. Tunakutakia usafiri salama na upone haraka mpendwa wetu Cecy.

    ReplyDelete
  13. InshaALLAh Mola wetu Mlezi twakuomba kwa unyenyekevu wa hali ya juu umponye binti huyu na umjaalie awe katika waja wako wema na wenye kukucha wewe ALLAh, tunakuomba kwani kwako hakuna lishindikanalo Mola wetu Mlezi unatenda utakalo na unamsamehe umtakae , Allahumma Amin inauma sana !

    ReplyDelete
  14. Watu wanne walimuona mtoto Cecilia na hali yake ya kuhuzunisha, watu hawa wote walikuwa wanamuamini Mungu ila ni watu wa rangi tofauti, baada ya kuambiwa ripoti ya Mabingwa na madakitari mtu mmoja ambaye ni:
    1.Mzungu alisema " Na tuangalie utafiti zaidi wa kitaalamu na mgonjwa tumjenge matumaini kwamba atapona, ni muhimu kuwa na Matumaini.
    2. Mchina akasema- Na tujaribu dawa za asili na utaalamu wa asili.
    3. Mhindi akasema - Na aendelee na dawa alizopewa na Daktari pamoja na aendelee kumuomba Mungu.
    4. Muafrika/mswahili - Yote ni Mungu, Yesu atamponya, Dua/rehma za Mungu zitamponya.
    Nakusudia kusema sisi Waafrika approach yetu kwenye matatizo always tunategemea Mungu tofauti na wenzetu na ndio sababu wagonjwa badala ya kukimbizwa hospitali wakati maradhi yanapoanza tunaelekeza nguvu kwenye maombezi na misikitini. Wenzetu sio kama hawaamini Mungu ila kwenye suala la ugonjwa wanaamini kimbilio lao kubwa ni kwenye sayansi.

    ReplyDelete
  15. Natuma neno la uponyaji likufikie Cecilia hapo ulipo neno la bwana ni nyundo ivunjayo vipandevipande, likavunje kila aina ya vijidudu vya maradhi mwilini mwako katika Jina la Yesu kristo. Amen

    ReplyDelete
  16. sina uwezo wa kufanya chochote bali nitakuombea mdogo wangu usikakte tamaaaa mungu yupo.................na bwana wetu yesu atatenda miujiza....

    ReplyDelete
  17. mnaonaje tufanye mpango tumpeleke kwa muombeaji Joshua wa emmanuel TV. Naamini uponyaji wake unaweza kupatikana na jina la Mungu likazidi kuinuliwa.
    kama itakubalika basi tuhamasisha tuchange.

    ReplyDelete
  18. Kwa mwenyezi Mungu hakuna lisilowezekana, Mwenyezi Mungu akusaidie, akupe moyo wa subira, tumuombee mwenzetu aondokane na hili tatizo. Amen

    ReplyDelete
  19. Mungu msaidie mja wako

    ReplyDelete
  20. Naomba tumuombee kwa m/mungu ampe salama na treatment aliyoshauriwa ili kutoa sumu iwe very effective kuliko watu wanavyofikiri kwamba ni heri sana angekuwa operated,Ila tuelewe kuwa wateule wa afya tulio nao hapa kwetu bado sana kiutendaji, iweje diagnosis tu ya sumu mwili tufunge safar za mamilioni

    ReplyDelete
  21. Innshallah mw/mungu atasaidia celina yote hiyo ni mitihani mola kwa nguvu na kwa uwezo utapona kwa baraka zake - ameen
    mdau
    UGIRIKI

    ReplyDelete
  22. Michuzi tafuta mkakati wa wanajamvi hapa tuweze kuchangia kiasi chochote kile hata kama ni sh 100, hakika watu watachangia sana, hali ya huyu mtoto inasikitisha na kila nikiangalia blogs na kukutana na hizi picha zake machozi yananilenga lenga, fanya hivyo pia watu waangalie kama kuna uwezekano wa huyu binti kupelekwa nchi nyingine nje ya India, kupona kwake kutaleta furaha kwa kila mtu aliyemuona, Nitamuandikia Mjengwa pia afanye kitu kama ninachokushauri

    ReplyDelete
  23. Jamani naomba tuwaombe madaktari wanaitwa, Doctors without Borders, wenyewe wanaweza kuja bongo wakikubali kesi yake, au wakamsafirisha wanakoona kunafaa. Mie naona kesi yake inakubalika. Lakini sina infor kamili za huyo mtoto na niko ughaibuni na sijui nani wa kuwasiliana naye kuhusu ilo, Ndugu Michuzi. Lakini mtu mwenye habari kamili za huyo mtoto anaweza kugoogle Doctors without Boarders na akaweka hizo habari za huyo mtoto na akajibu maswali wanayotaka. Mungu ambariki na kwa uwezo wake atapona tu.

    ReplyDelete
  24. Bado Juhudi na upendo unahitajika kwa kijana huyu na wengine wote ambao hawajafichuliwa na wasamaria wema. kwa mashirika ya umma na binasfi changieni haraka kama mnavyochangia mamilioni na mabilioni ya shilingi kwa mipira na entertainments nyenginezo ambazo hazileti tija ila ugonywa wa moyo tu.

    Kwa watanzania wote chururu si ndondondo toa ulichonauwezo nacho kuthibitisha upendo wako na imani ya bwana aliyembinguni.

    Mbiu ya mgambo hiyo bahati ya muhogo waupendao ni kidogo kumbe nao umo kutoa sumu kwa wanyonge kama Cecilia. Wanasayasi wa kitanzania kazi kwenu.

    ReplyDelete
  25. Always when i read about Cecilia i crying coz she is suffering alot. Imagine hana wazazi na ni mdogo wa kubeba matatizo yote haya by herself. Ana maswali mengi mwenyewe anajiuliza ambayo kwetu, kwake hana wa kuyajibu, nadhani swali lake la kwanza analojiuliza mara zote ni "ooh Mungu wangu kwanini mimi nilikukosea nini? Oh my God why me what i have done to you? Mungu akusaidie mdogo wangu. Ushauri wangu sisi tulioko nje UK/USA tutumiwe details zote za madaktari tuangalie hospitali ambazo zitaweza, but India it was the best. Mnaweza kututumia picha za alipokuwa India? Mimi niko Uk kama vipi tuwasiliane, sitaweza kuweka details zangu hewani hadi mcofirm kama is it ok as i suggest?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...