Wanaharakati wa haki za kibinadamu wa Dar es Salaam pengine kwa kusukumwa na uzalendo, ushabiki wa kisiasa au vyote wanaandaa mandamano ya kupinga kulipwa tozo ya zaidi ya Tshs. Bilioni 110 kwa kampuni ya Dowans. Wapo wanasiasa wa chama tawala na wa vyama vya upinzani ambao wanaunga mkono harakati za taasisi hizo kupinga malipo ya tozo hiyo.
Wakati tunaangalia hayo lazima tukubali kwamba nchi hii inaongozwa na utawala wa sheria na bila kuangalia kama Dowans ni ya nani tukubali kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Biashara ICC ndiyo iliyotoza tozo hiyo kwa kampuni hiyo. Watanzania wengi ambao wanataka tozo hiyo isilipwe hawazingatii kwamba kama ICC ikiombwa na Dowans inaweza kukaza hukumu na kuitangaza Tanzania kwenye vyombo vingine vya Kimataifa, hatua ambayo inaweza kusababisha mali za Tanzania zikakamatwa mpaka pale tozo hiyo itakapolipwa.
Suala lingine la msingi la kuzingatia ni kwamba kadri tunavyoendelea kubishana na kuendelea kukataa kulipa deni ndivyo riba itakavyozidi kukua na deni kuongezeka. Deni halisi lilikuwa bilioni 94 na sasa ni zaidi ya bilioni 110.
Tunachotakiwa kufanya ni kile ambacho serikali inafanya sasa cha kutafuta njia rahisi ya kukaa na Dowans na kupata ufumbuzi unaoweza kuipa nchi ahueni. Maandamano na kelele za majukwaani au kwenye vyombo vya habari hazina tija kwa sasa.
Naomba kutoa hoja
Mdau Mkere Ketwa


Napenda kuchangia hoja hii kama ifuatavyo:
ReplyDelete.Kwamba kosa limekwishafanyika na ndilo linalotugharimu. Hili ndilo la msingi la kukubali
.Pili ni kwamba kesi imefanyika muda mrefu na tumeshindwa na tunatakiwa kulipa.
. Watanzania tunajipambanua mbele ya Mataifa kwamba tunapenda uadilifu kwa msingi huo ili kuthibitisha uadilifu wetu tunatakiwa kulipa hii tozo! hilo halina ubishi. Nikweli inauma lakini hatuna jinsi.
Chakufanya ni kwamba waliotufikisha hapa si wanafahamika hao ndio tunatakiwa tuibane serikali yetu tukufu ambayo inataka kuthibitisha mbele ya Mataifa kwamba ni ADILIFU na ingependa kuonekana hivyo iwabane hao waliotuingiza mkenge! Bila hivyo itakuwa ni unafiki kujifanya tuonekane ni waadilifu wakati watu waliofanya madudu kwa makusudi tunawaacha waendelee kutanua wakitucheka ujinga hilo siliungi mkono.
NI LAZIMA HAO HAO WALIOTUFIKISHA HAPA WABANWE NDIO TUTAONEKANA TUKO MAKINI OTHERWISE NI WIZI MTUPU.
Asanteni Watanzania wenzangu wenye uchungu na nchi yetu kwa kunisoma.
nchi hii ina watu wenye matatizo sana na mmoja wao ni wewe....i mean mleta hoja. Dowans hawajulikani tutawezaje kukaa nao na kujadiliana?? ki ufupi ni kama Majini/mapepo hivi yanademand kufanyiwa kitu yet hayaonekani! cha msingi ni kutolipa..ni bora lawama kuliko fedheha.
ReplyDeletenaomba unijulishe Dowans ilirithi mikoba kwa nani? sio kwamba tunashabikia tunataka kujua kinagaubaga jinsi swala hili lilivyo maana ni kodi yetu inalipwa. Haiwezekani watu wote wawe ni washabiki wa siasa bila kuwa na uelewa wa swala hili waanze kushabikia deni lisilipwe, naomba uwe mzalendo tafadhali, na si mkereketwa tu, angalia maisha yalivyopanda , wanafunzi wa elimu wa juu wamwkosa mikopo, waalimu ndo usiseme halafu tuwalipe tu Dowans waliorithi kampuni hewa Ya Richmond inaingia akilini hiyo?
ReplyDeleteMtoa mada nani kakutuma? Wewe unajua ICC inaendeshwaje na kwa manufaa ya nani kama si mabepari? Wanaharakati ni suluhisho kwani wana uwezo wa ku mobilize dunia kuona ni jinsi gani hii mijizi imetuibia; Kama si wanaharakati tena wa UK BAE wangerudisha pesa yetu? Mimi na support wana harakati kwani dunia ikijua huu wizi there is no body including ICC can do anything. Wanaharakati nawashauri muanze sasa ku network na global civil society tuwatie adabu hawa wezi wetu.
ReplyDeleteNaomba kurekebisha jambo moja, to put the record straight. Ifahamike kwamba ICC haina uwezo wa kukazia hukumu, na ndio maana ilibidi hukumu ile isajiliwe na mahakama kuu ya Tanzania ambayo ndio ina uwezo wa kisheria kukazia hukumu ile. Hivyo madai ya Mkereketwa (wa nini?) kwamba Dowans inaweza kurudi ICC kukazia hukumu na Tanzania sijui ikafilisiwa mali zake nk si sahihi kisheria.
ReplyDeleteAsante.
huyu alie andika hii atakuwa fisadi,Unaogopa kufungiwa? Unamuogopa nani? Gadafi na Nchi yake mbona hawajaenda mtetea hao unaowaogopa.Kalipe wewe hizo pesa ulizo iba za kifisadi.Hakuna kulipa mwanzo mwisho
ReplyDeleteDunderhead!
ReplyDeleteJibu mbona ni simple.
ReplyDelete1. wafukuze kazi watu wote walioshika katika mikataba hii.
2.warudishe rushwa au pasenti wilizochukua.
3.Mmiliki wa dowans na kampuni kabla ya dowans wajulikane na walipataje mkabata huu na nani alitoa rukhusu ya kusaini nao.
4.hakuna kulipa kama walikujua dowans wakufuata mkabata kihalali na pia walipe vipi wakati wakutoa service..
wajinga ndio waliwao...tz
Nasikitika sana.Lakini Hiyo ni athari ya viboko kwa watawaliwa na kujiamini kupita kiasi kwa watawala.Leo utazuia mandamano kesho jiandae kupambana kivita na hao hao.Hata waköloni hawakujua kuwa ubabe sio suluhu!
ReplyDeletekwanini
bajeti 2011/2012
1.bilion 172.6 makusanyo ya serikali za mitaa. walimu hao,watendaji hao,miraadi ya maji hiyo.
2.Bilion 57 kununua chakula cha ziada.je mvua zitanyesha?mangungo jibu!
Bilion 50 Tanzania investment bank
ikize mtaji.wajisiliamali hao.soma bajeti ili Mtaji wa TIB 90!ua benk ulipe Deni ukakope tena. saidia "tawala".Unachelewesha ambacho nasemma kwa njia hio lazima kitatokea.
Nakusaidia hakikisha mangungo hamiliki hata pete kabla ya kulipa deni.ukiweza kuonyesha hasira hazarani kwa mangungo na kundi lake hutazuia maandamano ya kukupongeza na hoja zako.
Kwa deni hilo Mangungo na wenzake anazo pesa kuliko "tawala":
Mangungo ni kiongozi aliyesifika kwa mikataba ya umma iliyokuwa na manufaa kwake enzi za ukoloni.
hawajaisha.
kachukue kwa kundi la mangungo harafu tangaza hicho kiwango nafikiri mtayamaliza nadni kwa ndani anazo usibishe :Haaa vijiseti tu!
Mbogolo 0758950950
Mafisadi kama huyu alieleta mada ingekuwa kule kwenye tawala za kimla tungesema akatwe kichwa !
ReplyDeleteHayamkini aliyetoa hoja ni mtu mwenye uwezo mdogo sana wa kufikiri na kutafakari,na ni lazima atakuwa ni mmoja wapo anayenufaika na hiyo dowa inzi ,kwa ni lini mtanzania alikuwa na nafuu mpaka tutafute nafuu kwenye dowa nzi?
ReplyDeleteWatanzania wajinga kweli. Kubisha jadi yao. Solution zao za kibabe kibabe. Wanamchoma jambazi bila ya kumhukumu.
ReplyDelete