Baraka wa Chibiriti akiwa nyumbani kwake Cesena, Italy

Habari Mkuu, pole sana na majukumu.
Napenda sana kuwakilisha hoja yangu katika 
Blog a Jamii ambayo mimi naiita Blogu ya Taifa
 
Hivi hawa wanaoongea kiswahili na kuchanganya changanya na Kiingilishi, hivi ina maana hawajui kabisa Kiswahili fasaha au? Tuseme ukiongea Kiswahili moja kwa moja bila kuchanganya na kimombo utaonekana hujasoma? au sio mjanja? Mimi mara nyingi sana huwa najiuliza sana kuhusu swala hili sipati jibu....naombeni sana wadau nanyi mnisaidie. 


Mbona Kiswahili ni lugha tamu sana na yenye raha kabisa wakati ukiiongea? Sasa kwanini watu wanaiharibu haribu lugha hii kwa kuchanganya na lugha zingine ambazo hazipo kwenye kiswahili kabisa? 


Mimi napenda sana lugha ya Kiingereza na lugha nyingine nyingi....lakini sio ndo iwe mwanzo wa kuchanganya na lugha yangu nzuri na inayoeleweka kabisa ukiwa unaiongea, sasa kwanini mnaiharibu? Kama unaongea Kimombo, Kifaransa, nk......ongea moja kwa moja tujue kuwa unaongea hiyo basi, sio unatuletea za kuleta ili tujue kuwa wewe ni msomi au sijui nani. Hivi kweli umezaliwa na kukulia Tanzania unawezaje kusahau lugha yako? kweli kweliiii....duuuhhh kweli kazi ipo. 


Mimi nawafahamu wazungu wengi tu wanaoishi Tanzania, wanaongea kiswahili vizuri sana bila kuchanganya hata neno moja ya lugha zao, na hili je tusemeje? kwakweli tunaulimbukeni mkubwa sana bado.....wenzetu wanavyopenda lugha zao mpaka basi, tungejua hili sijui kama tungefanya hivi. Mimi ningefurahi sana kusikia watu wanaongea Kiswahili labda wanachanganya na makabila yao, sio lugha za watu wengine. Nilimwuliza rafiki yangu mmoja eti akaniambia kuwa maneno mengine hayapo kwenye Kiswahili, ilibidi nicheke tu....maneno gani ambayo yanakosekana kwenye kiswahili yakufanye uongee lugha za watu? Basi hata kama neno moja moja unalikosa......isiwe kila unapoongea unachanganya na hicho kimombo. 


Hebu naombeni nanyi wadau mnisaidie kuhusu swala hili, huwa sipati jibu kabisa......mbona lugha yetu ni nzuri sana na nitamu kuiongea hadi nje wanaisifia sana, sasa kwanini tusijivunie na kuiongea vizuri?
 
Basi ndo hilo nililo nalo moyoni linalo nikera....nawakilisha.
Ni mdau wa siku zote
BARAKA wa  CHIBIRITI,
Cesena, Italy.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. kwahilo naungana nawewe moja kwamoja yaani ilikuwa ni swali langu la kila siku nikiangalia maojiano ya watu toka nyumbani kwenye youtube inakera sana...mtu anajidai kuchanganya lugha,kiswahili ndo kakua ana kiongea leo anajidai kuchanyaga...mi nadhani siyo ulimbukeni maana hilo nineno zuri sana.Mimi kwamaoni yangu huo ni ujinga.
    Nyingine ni pale mtu Kazaliwa musoma kijijini,nakakulia huko na lugha yake anaijua fika.lakini akija mjini Dar au Arusha, au Nje ya nchi na kuishi muda kidogo tu ukimsemesha lugha yake eti anajidai hakuelewi.ukimuuliza ni vipi eti ahaa unajua nisikunyingi sana sijaongea lugha hiyo mhmm ni siku ngapi zinakufanya usahau lugha yako? haya sasa hata hicho kiingereza wanachojidai kukiongea pia hawakijui. nitakupa mfano; kuna dada mmoja nilikuwa naandikiaana naye sana kwenye e-mail siku moja akaanza kuniandikia anachanganya lugha nikamuuliza akasema kwani sielewi nini? basi kwakuwa nakielewa kiingereza kidogo nikachuna,ikaja kwenye Facebook ndo kabisaaa, basi safari hii sikumuuliza nikaanza kumuandikia na kumjibu kwa kiingereza tupu,akasema mbona unaniandikia kwa kiingereza je unajua unaye chat naye? nikajibu ndiyo najua,akaniuliza tena kwanini unaandika kiingereza tuuu mi sikuelewi saazingine, na hata maneno mengine, nikacheka tu kicheko ambacho hakukiona lakini inasikitisha.Sasa kama hujui kiingereza fasaha kwanini unaaandika nusu kiingereza nusu kiswahili kwanini usiandike kiswahili chote hali mimi ni msahili mwenzio?
    Mwingine niliyekuwa naye huko musoma yuko,marekani kanipigia simu kanisalimia kwa lugha yangu nikafurahi basi naminikaendeleza maongezi kwalugha hiyo make nafahamu anaifahamu lugha hiyo vizuri kuliko hata kiswahili.kanikatisha kasema duh sikumbuki maneno mengine tuongee kiswahili,mhmm sikusema kitu lakini nikasema moyoni huu ni ulimbukeni na ujinga kabisa.
    Ningeelewa kama ni mtu simfahamu anajaribu lugha maneno mawili matatu lakini siyo yeye aliyezaliwa nakukulia huko na tumeongea lugha hiyo mpaka tukiondoka tunamiaka 23 leo hunasema umesahau umesahau nini?Chibiriti nadhani hoja yako inatakiwa ipelekwe kwenyeluninga ya taifa kama TBC au ITV ijadiliwe labda watu wakiona watajifunza.Hongera kwa mawazo chanya kaka.

    ReplyDelete
  2. Bwana Chibiriti ulikuwa kimya siku nyingi sasa naona umerudi ulingoni tena, kuhusiana na hoja yako vipi uliona clip ya Wema Sepetu nini? manake huyu dada ndiye nguli wa kuharibu lugha, kusema kweli inaudhi tena saana tu, nakubaliana na wewe kabisa.

    ReplyDelete
  3. wengi wetu hatujui kwamba kiswahili ni lugha ya 7 duniani inayozungumzwa na watu wengi....

    ReplyDelete
  4. Kuchanganya kiswahili na kiingereza au kiswahili na kiarabu baadhi ya wakati ni lazima kutokana na ukosefu wa maneno ya kiswahili au mzungumzaji kutojuwa maneno ya kiswahili. Kama utaangalia msamiati uliotumika kwenye Windows 7 ya kiswahili basi wengi mtashindwa kutumia Windows 7 ya kiswahili.

    ReplyDelete
  5. Mr. Chibiriti
    Pole sana kwa mshangao wako!
    Watanzania wengi sana, Kuanzia Tanzania mpaka Ughaibuni hawafahamu Kiswahili vizuri wala Kiingereza. Kiswahili ni lugha ambayo bado inakua kwa kasi sana na inaukosefu wa tafsili nyingi za maneno. Kwa mfano mimi mwenyewe huwa na jaribu sana kuongea kiingereza lakini wakati mwingine naishiwa na tafsiri. Nimelelewa ni kiongea Kisukuma, Nimejifunza Kiswahili kutokea kwa jamii, cha darasani nilipata D ama F mara kwa mara, Nimejifunza kiingereza kupitia kwenye Runinga kwa kuongalia matukio mbalimbali na Taarifa za habari hususani CNN na BET za Marekani. Ningependa sana kuongea Kiswahili au Kiingereza chote bila kigugumizi lakini safari ni ndefu. Nimesikiliza Hotuba nyingi za viongozi wa Tanzania na Kenya na nimekuta hili tatizo ni la wengi. Nimetembelea Mwanza mwaka jana, 2010 nimekutanza na watoto wengi sana wenye umri kati ya 5-14 hawaongei Kiswahili kabisa, wao ni Kisukuma tu. Nimekuwa nje ya nchi toka mwaka 2000 na kuna maneno mengi yameongezeka au sikuyafahamu kama vile:- Ugavi, Uchakachuaji, Fisadi, Jokofu, Nderema, na Mengineyo mengi!

    Kwa hiyo kwa Maoni yangu, Watanzania tuzidi kuongea Kiswanglish kama kawaida kwa maongezi ya Kila siku na wenzetu.
    Ila Tuhutubie kwa Kiswahili fasaha, Kilichoandikwa kwenye hotuba na waandishi wa hotuba au kwa kufanya uchunguzi kabira ya kuhutubia

    Nimatumaini yangu, Mr. Chibiriti ataelewa
    Ahsante: Fumbuka, Alex.

    ReplyDelete
  6. wee kibatari hahaha kiberiti leo umegonga penyewe haswa, eti hawa wasanii wetu nao utawasikia u know u know kibao, halafu olee wako wajuwe umetoka ughaibuni utakoma, wanafikili nchi zote za ughaibuni wanaongea kingereza, mie sijui kingereza, lakini najuwa kifaransa kwa sababu ndiko ninakopiga box, bac niliporudi bongo nikapata kamrembo, yani alikuwa anainiambia maneno ya kingereza hata sielewi alikuwa anasemaje, nikamwambia mpenzi tuongee tu kiswahili ama kikwerau kifaransa ndizo lugha nijuazo, akasema eti keshatamba sana kwa wenzie kwamba jamaa yake anatoka mamtoni kwahiyo lazima auze na mimi, bac kazi ilikuwa nikikutana na hao wenzie, wananisemesha na mie sielewi kila kitu, msichana wangu alikuwa anajidai eti jamaa yangu kaka nje muda mrefu kakikosa kiswahili ndiyo maana sasa hajibu kingereza anataka wote tuongee naye kiswahili, sasa tukiwa kwenye yale mambo yetu, kusema ukweli mpaka wakati mwingine alikuwa ananikatisha, anasema maneno na mimi inabidi nifikilie kasemaje,sisi tuna kazi kweli,siku hizi ndiyo hali inazidi kuwa mbaya, tukienda nchi za watu tunalazimishwa kuzijua lugha zao, tukija nyumbani, wengine hawataki lugha yetu, chibiriti leo umegonga penyewe haswa, ni janga la taifa hilo, mpaka bungeni kuko hivyo hivyo nakwambia

    ReplyDelete
  7. Kuna dunia 'iliyofichika', na raia wake ni wale 'waliofichika' pia. Hii dunia huwa hatuioni wala kuifikiria, bali tunafahamu kuwa 'waliofichika' wapo. Tatizo, kutokana na kutoijua hii dunia, tunawashambulia na kuwahukumu sana hawa 'waliofichika' kana kwamba wanatoka tutokako sisi na hivyo wanapaswa wawe kama sisi. Hilo ni kosa.

    Dunia hii tuijuayo sote ni pana na imegawanyika gawanyika. Unapaswa kuwa muwazi sana katika kufikiria na kuona mambo ili uuone mgawanyo uliopo. Wanaochangaya lugha katika maongezi yao ni 'wafichika' watokao 'ufichika', ila ni wenzetu kabisa. Wao huwa wana dunia yao, wanaona mambo kwa tafsiri zao, na wanaishi kivyao baina yetu. Hawa wapo dunia nzima kwa uwiano tofauti tofauti. Hakuna anayeweza kuifuta dunia hii ya 'wafichika', hivyo tuwakaribishe kwetu na tuishi nao tu kama wenzetu. Dunia ya 'wafichika' ina umri sawa na ule wa utandawazi.

    ReplyDelete
  8. Mimi ni mtanzania nayependa sana lugha yangu ya kiswahili na nitaitetea siku zote. Hata hivyo pamoja na uzalendo wangu nimegundua kwamba Kiswahili bado kinakua na baadhi ya misamiati ya kitaalam kwenye lugha ya Kiingereza bado hatuna. Kwenye nyanja yangu ya Inofrmation Technlogy nimepata shida sana kueleza jambo kwa Kiswahili. Hii si kwa sababu nimeishi ughaibuni kwa mda mrefu bali ni kwamba sentensi haitengenezeki. Wakati mwingine neno linakuwa refu na kupoteza maana kwasababu linakosa tafsiri ya moja kwa moja. Asante kwa mdau aliyezungumzia Windows 7 ya kiswahili. Ukitembelea http://it4dev.blogspot.com/ kuna kura ya maoni kuhusu swala hili la Windows 7.

    ReplyDelete
  9. Chibiriti umeongea ukweli hao watu wanaodai kuwa kiswahili kina maneno machache sio kweli kabisa maneno yaliyoko kwenye kiingereza na kwenye kiswahili hayapo au ni magumu sana kuyapata na hata kama yapo hayatumiki sana ni michache sana mfano neno mass au density.

    Kinachoshangaza watu wanapenda sana kuchanganya lugha sijui wanataka kuonekana wasomi? Au ni nini? Mfano wabunge na mawaziri bungeni wanapokuwa wanatoa hoja bungeni, pia wanafunzi wa vyuo vikikuu wanapokuwa kwenye midaharo bila kuwasahahu watangazaji wa redio kama Loveness Malinzi unataka kuniambia huyu binti hawezi kuongea kiswahili akaeleweka mpaka achanganye na kiingereza?

    Baya zaidi linalonikera ni kuwa unakuta mtu alisoma shule ya msingi Kurasini, sekondari Jitegemee, sekondari ya juu Pugu na chuo Mzumbe huyu mtu hajawahi kukaa ulaya au Marekani tukasema labda miaka saba aliyoishi kule televisheni, magazeti, vilabuni alikokwenda, watu wanaomzunguka na makazini pote walikuwa wanatumia kiingereza kwahiyo anachanganya kidogo maana alipoteza mtiririko wa lugha kutokana na kuishi ughaibuni.

    Sasa mtu aliye soma Tanzania na kuishi muda wote Tanzania wakati kiingereza kinatumika shuleni tu lakini televisheni, magazeti, vilabuni, watu wanaomzunguka na makazini kote ni kiswahili kwanini mtu wa namna hii apoteze mtiririko wa lugha ya kiswahili mpaka imlazimu kuchanganya na kiingereza?

    Mwalimi Julius Nyerere aliwahi kusema watanzania ni watu wa ajabu sana mtu akiongea neno la kiingereza hata kama ni neno la kijinga anonekana wa maana akazidi kusema na mtu anyependa kuchanganya lugha huyo tu sio stadi katika lugha zote mbili achanganyazo ukimwambia sasa ongea kiingereza tu hataweza na ukimwambia sasa ongea kiswahili tu hataweza vilevile.

    ReplyDelete
  10. some of the words in English cannot be translated to swahili, and to answer your question Chibiliti,

    Kama alivyooleza huyo mchangiaji wa mwanzo, lazima ukubali kuna dunia ya watu waliofichika, and I must say I am one of them, I came to Europe since 1995, since that time I have been attending college, universities, professional courses, and work with almost all non - swahili speakers, for most part of the odd 16yrs of my life, therefore me personally, mixing the language become a part of adoptive engliswahili, I know I might a lone wolf on this but I am not the only one.

    I think you get the point..

    and now to be precise I have a young family, whom I try my best to communicate with them in Swahili, but unfortunately when their life style is purely surrounded by schools, play and so on all in english, Are you going to throw a blame on them as well, although we are trying really hard, encourage them to speak swahili while at home or meeting friends ...

    Chiberiti, It really depends on your lifestyle, if you are more from academic background, it is unfortunate that you will end up mixing language, because of the richness of words of other language such as english, but you are more from working background, socializing, communicate a lot more with swahili community, then swahili might stick with you no doubt.

    but, I agree with you that, some of the people in our society are acting, or pretender, although hawana athari kama wanayoipata jamii wa wafichika.

    shukran.

    ReplyDelete
  11. I am still confused kama hamjaniacha kwenye mataa kabisa. You know english na kiingereza bwana huwa vinaharibu kiswahili chetu. Kosa letu ni kufundisha lugha zote nusu nusu. Watu kiswahili fasaha hawajui na kiingereza ni cha kuibia na matokeo yake ni kuchanganya madawa. TUCHAGUE MOJA.

    ReplyDelete
  12. Tehe teh tee!

    We Kibiriti,

    Uza kwanza hiyo Kompyuta yako yenye CHOGO ununue FLAT SKRIIN bana. Bado unayo tu!?!

    Khaah!

    ReplyDelete
  13. mwanzoni mimi pia nilikua ninawaza kama wewe mtoa hoja hii, lakini baada ya kukaa kwa muda kidogo kwenye nchi za watu nikaanza kusahau maneno mengi ya kiswahili na hata kiingereza, kwa sasa nipo Urusi, kuna wakati kwenye simu nikiongea na watu nyumbani huwa ninachanganya lugha tatu bila hata ya kutambua, niv igumu sana, kwa sasa jambo zuri ni kwamba ninaweza kuandika tena kwa herufi zakilatini, lakini miaka miwili iliyopita ilikua ni tabu tupu, hata kuandika jina langu ilinibidi nifikirie kwanza!

    ReplyDelete
  14. Mbonza hili tatizo linaanzia bungeni, fikirieni wabunge waliochaguliwa na wazee wetu ambao hata hicho kiswahili shida halafu wao wanatoa/changia mada kwa kuchanganya na kingereza au bajeti inasomwa kwa kiinglish mi naona kote kuna problem

    ReplyDelete
  15. CHIBIRITI UNAOA LINI???!

    ReplyDelete
  16. Du, inaelekea huyu Chibiriti anakusanya vitu kutoka kwenye majumba ya makumbusho na kuvitumia, Angalia hiyo kompyuta yake, hata huku kwetu Temeke tumeshaacha kutumia hiyo Mizinga.
    Kazi kweli kweli mambo ya Ulaya hayo.

    ReplyDelete
  17. Hiyo PC yako kwenye picha nadhani ni wakati Steve Jobs bado dogo. Ukiiwasha shurti usubiri muda kutosha kumaliza shughuli zako zote.. uoge uende msalani, nk kabla haijaanza kazi. Hiyo dedication ya Steve Jobs

    ReplyDelete
  18. Jamani hiyo ni picha kutoka maktaba ya Michuzi. Sio latest.

    ReplyDelete
  19. Jamani ingawa nimechelewa sana kuona hoja ya huyo Kibiriti,,,sijui nimepatia?Ila namuunga mkono sana,,mimi hiki kitu najiuliza sana mara ya kwanza kuona mswahili aliye badirika kwa haraka sana,yule mrembo Flavian Mataka kitu kama hicho kama sijakosea jina lake,,jamani alitoka Dar kwenda sijui Japan au UK,,kwa wiki mbili tu.alikuja kasau Kiswahili kabisa,anaulizwa airport na waandishi wa Habari anashindwa kuongea kiswahili fasaha.
    Mimi nahisi watu kutokuongea au kuandika kiswahili moja kwa moja ni Ushamba,ujinga na Ulimbukeni wa hali ya juu mno...Mimi nilikuwa nakutana hasa na watoto wa mabalozi waliokulia nje yaani mtu anaenda nje anamiaka 4 anarudi kisha olewa na anazungumza kiswahili kizuri tu na kama kuna nino linamshinda unaona kweli anajitahidi akueleweshe bila kuchanganya pengine anahisi akikuwekea kizungu hutoelewa,,,Mimi pia ninavyojuwa wengi wanaofanya hivyo hawawezi kuongea kizungu moja kwa moja kwa kuwa kuna watu wengine wanajuwa kizungu watawagundua kasoro zao,kwa hiyo inabidi achomeke chomeke ili watu wajue nae ktk kizungu yumo,,,Wallahi mimi wananichefua mno kupita maelezo,,hiyo mdau huko juu kasema tangu amekuja ulaya ni 1995 hajakuna na waswahili,ndio maana anaongea kiswanglish,,no no no usitudanganye bwana,,ina maana huna mke?basi kama umeoa mzungu huwa hupigi simu nyumbani?au kukutana na waswahili,,kama si hivyo basi Unaukana UTz wako wewe ni mtumwa!
    Kiswahili ni kizuri mno na kwetu ni kuzuri sana maana mimi nasoma na wanafunzu makabira mbali mbali ila ukitaka kusema kitu chochote au mwalimu akiuliza kikwenu mnasemaje,,ukitamka walimu kila mara huwa wanasifia Lugha yangu ya kiswahili kuwa unamatamshi mazuri,,,,Hao watu huwezi kushindana nao waliokiona sasa ndo hicho ni kama kipofu aliyefungua macho akaona mwezi hata ukimuonyesha kitu kingine zaidi ya mwezi atakubishia mpaka kufa,,,

    ReplyDelete
  20. Wanaoongea kwa kuchanganya lugha zote mbili hawawezi kuongea lugha zote mbili kwa ufasaha.

    Hata ukiishi ughaibuni, huwezi sahau lugha yako hata siku moja!!
    Tena hao wanaochanganyaga lugha ndio unawasikia hawawezi kuongea kiingereza kabisaaaa. Chagua moja, utaishia kuchekwa!

    ReplyDelete
  21. LAKINI NANYI MNAOSEMA WATU KUSAHAU KISWAHILI NA KUBOBEA KWENYE KIINGEREZA INAKUWAJE BAADHI YENU MNA WAZAZI WOTE KABILA MOJA NA KUONGEA KABILA LA KWENU HAMUWEZI?

    MNA TOFAUTI GANI NA WALE AMBAO HAWAWEZI KUONGEA KISWAHILI FASAHA?

    MICHUZI HII MADA IPELEKE TENA JUU WATU WACHANGIE NI MUHIMU SANA MAANA WATU WENGI IMEWAPITA

    ReplyDelete
  22. Watanzania wengi hawajui vizuri Kiingereza. Wanapokuja huku mamtoni tunayaona. Wakiwa Bongo ndio hutamba na kiingereza cha kibongo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...