Na Danford Mpumilwa
Kabinti kangu a.k.a. Investment, Leah Danford Mpumilwa hivi majuzi kali-graduate kutoka shule ya sekondari ya wanawake ya St Theresa of the Child Jesus, hapo Kisongo, Arusha. Na mimi kama dingi mhusika nilijitutumua na kikosi changu kwenda kukapa pongezi na kukakumbusha kuwa huo ni mwanzo tu wa safari ndefu ya kutafuta elimu ingawa yeye alijiona ameukata. 


Na kaliponiomba kwamba sasa ni wakati mwafaka wa kumnunulia Lap Top nilikajibu kuwa kasubiri hadi katakapofaulu kuingia University. Ingawa jibu hilo lilitokana haswa na mambo mengine ukwasi chechefu nilionao. Lakini keki kaliipata haswa kama invyoonekana hapo chini;
 Hapa ni mawaidha kwa kwenda mbele; kwamba akiingia chuo atalamba laptop....
        Akiwa na dingi na wadogo zake Rhoda na Tuli 
  Siku ya furaha kwa Tuli na wote
 Kikosi kamili kilikuwepo kutoa hamasa ya elimu 

 Keki ilikatwa na kuonjwa na kikosi chote  
               

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Safi sana !!!

    ReplyDelete
  2. Kaka Mpumilwa kabinti ketu nakapa hongera sana, usisahau kukakumbusha ajiepushe na fedha za mafisadi watakaokuwa interested before hiyo university.

    Massoud Abiola Jr.

    ReplyDelete
  3. hako ka-Tuli...duh! inabidi Mzee ufuge ka-mbwa mapemaaaaa....!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...