Ankal habari,

Kwa heshima kubwa naomba utoe kilio chetu kupitia blogu yetu ya jamii, kuhusu mabosi wetu tunaofanya nao kazi.

Sisi watumishi kada ya usekretari tunapata shida sana tuwapo ofisini Kama ifuatavyo:-

Kwanza ni kuchelewa kutoka kazini baada ya muda wa kazi.

Unakuta bosi anamkalisha ofisini Sekretari, hadi saa tatu usiku tena bila kazi yoyote ya msingi ili mradi tu bosi bado hajaondoka. Na hii ni kila siku.

Na muda huo bosi akitoka anaaga “haya tutaonana kesho”. Bila kujua huyo aliemkalisha mpaka usiku wa saa 3 au zaidi atafikaje kwake. Wengi wanadhurika ikiwa ni pamoja na kuporwa na vibaka.

Muda mwingine bosi anatoka wakati wa muda wa kazi, anarudi tena ofisini saa 9 au 10 alasili, ndio anaanza kazi hadi usiku.

Tatizo linakuja kwa wenye familia, tukitoka muda huo, mpaka kufika nyumbani ni saa 4 usiku au 5. Tukifika tuko hoi, hata tukidaiwa kile chakula cha usiku tunakuwa hatuwezi. Sasa hii inachangia kutuvurugia ndoa.

Kwani tumekuwa tumechoka sana kiakili na kimwili hasa Ukizingatia tunatakiwa kuwahi ofisini kabla mabosi hawajafika hiyo ni saa 12.00 asubuhi hadi moja kasoro. hilo sio tazito, tatizo linakuja kwenye muda wa kutoka.

Ombi letu kwa mabosi ni kuwa watufikirie na sisi kuwa ni binadamu na tuna familia zetu hasa watoto wanatuhitaji. Hivyo tunaomba ikifika saa 11 jioni turuhusiwe kurudi nyumbani. Basi tukicheleweshwa sana isipite saa 12 jioni.

Unakuta mabosi wengine hawana wenzi (Mke/mume) hivyo hawaoni umuhimu wa kuwahi kurudi nyumbani.


Pili, Siku za Mwisho wa wiki (weekend)
Ni siku za kupumzika ili jumatatu tuwe fresh kiakili. Lakini kwa sisi ma sekretari hilo hatuna. Tunatakiwa kuja kazini hata bila sababu za msingi, tena muda wa kutoka hata siku za weekend ni saa 12 jioni tukiwahi saa 10. jamani tuonewe huruma. Hii inachangia kutofanya kazi kwa ubora.

Mama Mh. Hawa ghasia sikiliza kilio chetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. ni kweli uncle pia muundo wa ma ps uangaliwe sijui wa sasa wameutoa wapi hivi kwa nini hakuna senior secretary au principal secretary kwenye muundo wetu please mama ghasia hebu tusaidie maana hata wahudumu kuna principal office asstant vipi huku kwa ma ps huo muundo mmeutoa wapi jamani.

    ReplyDelete
  2. HAAA KUMBE NDIO MAANA NDOA NYINGI KUMBE NDOA NYINGIZA MASECRETARY ZINAKUWA NA MIGOGOLO SABABU YA HAO MABOSI UCHWARA NI KWELI MAMA GHASIA HEBU LITOLEE TAMKO HILO KWA MUDA WA KAZI NA MWISHO WA WIKI WASIFANYISHWE KAZI MBONA TARATIBU ZIKO WAZI ZA UTUMISHI NA KAMA KUNA KAZI ZA ZIADA NI BORA WAJE WAZIFANYE SIKU YA PILI YAKE JAMANI EBU TUUHESHIMU HUO UTU WA MAMA/DADA/ZETU ILI TAIFA LIENDE SAWA NA MALEZI YA FAMILIA ZETU - Mdau Richie wa ughaibuni

    ReplyDelete
  3. mh! hilo nalo neno.........

    lakini kweli, nyie mabosi mmesikia? achani kuvuruga ndoa za watu! waruusuni masekretari wenu mapema atleast hata kumi na moja.

    pia kuna baadhi ya mabosi wanakuwa na malengo yao kuwachelewesha kutoka kazini ili panapokuwa kimya wawafanyie mambo ya ajabu. (aacheni tabia mbaya).

    ReplyDelete
  4. sina la kusema maana nikisema nitajaza page zote hapa ila hali ni mbaya kuna kipindi mi nilikua natoka mpaka saa nane au tisa kwa kweli nimeamua kuacha kazi niko kwingine tena najaribu kukinishinda naanza ujasiliamali tu. tedy

    ReplyDelete
  5. Sio hilo tena maboss wengine pamoja na kukuchelewesha pia huwa hawana utetezi pale inapotokea ps wake amepatwa na tatizo. Wengine roho mbaya nazo kazi kweli.

    ReplyDelete
  6. Mambo ya ma-ps na mabosi ndio hayo. Hakuna sababu ya ps kubaki baada ya saa za kazi isipokuwa kama bosi ana mipango mwengine na huyo ps wake. Overtime kufanya ni maamuzi ya mfanyakazi mwenyewe. Mambo ya kidikteta yameshapitiwa na wakati. Kila kitu sasa duniani kinafanywa kwa kufuata sera ambazo zimekubaliwa na utawala.

    ReplyDelete
  7. Sijui hiki kilio kimeletwa na mume wa sekretari au sectretari mwenyewe. Ni kweli kuna mabosi wanawaweka bila kazi na wakati mwingine hata akiwepo hatumwi chochote yupo yupo tu, wakati mwingine ni woga wa secretari kuaga kuwa anaondoka. Pia jamani kila kazi ina mazingira yake. ukiwa askari hukwepi lindo, muuguzi night ni zako.
    We unamshangaa sectretari, dereva je anayembeba huyo bosi kupeleka kwake kaskazini wakati yeye anaishi kusini; na kesho awahi tena kumchukua na hizi foleni!!!. Kuna kazi na kazi bwanaa. ila mwenye kazi anataka kutoka asiyenayo anataka kuingia. Kazi ipo. Ila wanaofanya hivyo bila sababu ya msingi ya kikazi waacheee!!!

    ReplyDelete
  8. Kuhusu mafunzo nalo liangaliwe pia. kada zote watakwenda masomoni ikifikia ya makatibu muhtasi - mhmmmm yaani itabidi ufanye kuomba/ubembeleze utafikiri sio haki yako. Mara itaonekana fedha zitakazotumika ni nyingi alimuradi visingizio kibalo.

    Mama Ghasia please wakumbushe kwamba nasisi tunastahili kwenda kwenye courses kwa ajili ya elimu na kurefresh.

    ReplyDelete
  9. Haya mambo ni ya kweli kabisa, Waziri sikia kilio hiki tafadhali.

    ReplyDelete
  10. Ukiangalia haswa wanaolalamika hapa ni mps wa ofisi za serikali! Lakini katika private sector nyingi secretari anaheshimika sana na anajiheshimu na anajua kazi na mipaka yake ni nini. Mimi mwenyewe ni secretary ninaejiamini na nimesomea na naijua taaluma yangu vema najua mipaka ya bosi na kazi yangu hivyo sikubali kunyanyasika kijinga na hata bosi mwenyewe kukufanyia jambo la kijinga anakuangalia mara mbili umekaa aje nao wanaogopa.

    Jambo lingine michuzi ni kwamba katika uombaji wa kazi hasa serikalini wanawapa kipaumbele masecretari ambao wamesoma katika vyuo vyao vya utumishi wa umma lakini secretary aliyesoma kwenye private institution kumfikiria kwao ni mbinde, na ma - ps wazuri wengi ni wale wanaosoma private institute huko hakuna longolongo kama hapo magogoni kwao na ndio hao wengi kutokana na kutokujiamini ndio wananingia ktka matatizo kama haya.

    ReplyDelete
  11. kwa aliyaandika habari hii nampa pongezi kwani ni tabu tupu hatuna hata muda wa kufanya mambo mengine, hatufui hatupiki hatuhudumii familia zetu tuko kazini kwanzia jumatatu hadi jumatatu tena twatoka usiku uonevu jamani haaaa tumechoka, hadi wachumba wanatuacha kwasabubu tuko bize, hooo Mhe. Hawa Ghasia sikia kilio chetu.

    ReplyDelete
  12. Poleni sana kina mama. Hivi hamna chama au jumuia yenu? Kama hamna basi anzisheni haraka. Na jee chama cha wafanyakazi kinashindwa kuwatetea? Au mnaogopa kuwashitaki mabosi? Au mnapata overtime?

    ReplyDelete
  13. Habari hii ni ukweli kabisa. Na kikawaida ni lazima PS awahi kazini na Kutoka kwake ni baada ya Boss kutoka, hii ipo kila mahali. Tunachopaswa kuomba na kutetea ni Waziri kuingilia kati ili Maboss watambue mchango wetu, Tunaonewa sana kimaslahi, mishahara ya MaPS si chochote na kiukweli sitaki hata mtoto wangu asomee kazi hii! ni utumwa usio wa kawaida. Mh. Waziri angalia upya maslahi ya maPS

    ReplyDelete
  14. Huku ni kuoneana wala sio kazi yaani ubinafsi umewazidi.Hakika kila kazi lazima ziwekwe taratibu maalum za kuajiri watu na bila kificho.Haiwezekani ukamuweka mtu mpaka muda unaotaka wewe kwakuwa ni bosi.Lazima unapoanza kazi ujue muda wa kuingia na wa kuondoka tena msainiane hiyo contract.Na kama kuna tatizo la kutoruhusiwa kuondoka muda wa kumaliza kazi bila matakwa yako then ashitakiwe kwa kumfanyisha kazi raia kama mtumwa.Tatizo linakuja kwa wafanyakazi kuogopa kufukuzwa kazi na bila kujua haki yake kama mfanyakazi.Kutokujua haki yako ni jambo baya sana pamoja na kwamba wapo wenyekujua lakini wanaogopa hata kama wakishitaki hawatashindwa kutokana na matajiri watatumia pesa yao kwa kushinda bila ya haki.Lakini kama watajitokeza wawili watatu na kuwaanika mabosi wao magazetini na ktk TV nadhani watakoma kwakuwa wataonekana wabaya na kila mtu.Au biashara zao zisusiwe kwa kutokuwa na ubinaadamu hapo ndio watatia akili.

    ReplyDelete
  15. chama kipo lakini ni kama kimekufa, overtime sh.5,000 tunapata baadhi tu wengine hakuna overtime, tena tunapata kwa kunyanyaswa, mara upunguziwe siku, mara nini yaani ni mateso. BY PS/SERIKALINI

    ReplyDelete
  16. Wengine wanazitafuta hata wako tayari kukaa mpaka asubuhi. Basi sijui itakuwaje.

    ReplyDelete
  17. chama kipo (TAPSEA) ila ufisadi mtupu kazi yao kuandaa Kongamano tu. Nothing else tatizo uongozi wa hiki chama haupo kwa ajili ya kuwasaidia maskeretari upo kwa ajili ya maslahi binafsi. Maskeretari tujipange hakuna wa kutusaidia kilio chetu but its our own effort. Tuchague viongozi ambao wenye nia na uwezo wa kufikisha kilio chetu sehemu husika. BY MDAU (PS/ PRIVATE SECTOR)

    ReplyDelete
  18. mabosi wao wana waweka ma ps utafikiri kunakazi ya maana bali unyanyasaji mara nichemshie chai wakati birika liko pale kila kitu unashindwa kujichemshia chai eti boss. akiwa na chochote cha kuandika boss anaandika kwenye karatasi wakati mezani kwake kuna computer anatoka na kikaratasi chake anampa ps chapa hii barua mara moja. ps akichapa ana print anampelekea boss anasahihisha anamrudishia badala ya kumuomba soft copy asahihihse mwenyewe ili mradi wastage of time. yote haya ni manyanyaso tu

    ReplyDelete
  19. Nyie vipi. naona mlengo wakina mama tu kwani wakinababa hatupo kwenye hii kada? Mimi kaka PS mwanaume kwakweli inaniuma sana mnanyanyaswa wakina mama. Mimi na bosi wangu tunaheshimiana sana kwasababu anajua sitaki mchezo na sina urembo mwanaume mwenzie. kazikazi. Bosi wangu mhindi.

    ReplyDelete
  20. jamani nakuunga mkono mdau ulietoa hii hoja ya mabosi kutuchelewesha masekretari. kweli wanatakiwa kufanya kazi ndani ya masaa ya kazi na kama unachelwa basi iwepo sababu ya msingi ya kukuweka ofisini na sio kwa kuwa boss yuko bored kwenda home mapema basi unabaki kumlinda hapo mpaka unaanza kung'atwa na mbu. badilikeni mabosi wetu mtatusaidia na sisi kufanya kazi zetu kwa ufanisi mzuri tukiwa na mapumziko ya kutosha kiwa ni pamoja na kuangalia familia.

    MMOJA KATI YA MASEKRETARI.

    ReplyDelete
  21. Ni kweli watumishi wetu wa kada hiyo mnapata matatizo mengi hasa linapokuja suala la kufika na kuondoka ofsini kabla na baada ya muda wa kazi uliopangwa na serikali kupitia Menejimenti ya Utumishi wa Umma,saa 1:30 asubuhi- 9:30 alasiri kwa kufuatana.
    Hata hivyo naomba makatibu wahitasi na watumishi wengine wa kada za chini,mfanye yafuatayo:
    1.Ombeni kuonana na Afisa Rasilimali watu ili mmjulishe suala hili bila woga kupitia kikao halali cha makatibu wahitasi.
    2.Kupitia ofsi ya rasilimali watu,muombeni mkuu wa idara,kitengo,wizara au asasi muwe na vikao vya mara kwa mara baina ya watumishi na menejimenti ili kukumbushana wajibu na njia thabiti za utendaji kazi ili kuboresha ufanisi na mahusiano kazini baina ya watumishi wa kada za chini na watendaji wakuu.
    3.Kupitia ofsi ya utumishi,hapo mnapofanya kazi,kumbusheni umhimu wa kuwa na chama cha makatibu wahitasi ili viongozi mnaowachagua wawatetee na kuhakikisha mnapata maslahi yenu kazini,ikiwa ni pamoja na suala la muda,motisha,kupandishwa madaraja,maboresho ya mishahara yenu nk.
    4.Mwisho,kama yote hayo hayatafanikiwa ndani ya miezi 6 kutoka mtakapoanza mchakato wa kuhakikisha kuna maboresho ya utendaji wenu wa kazi na uthabiti wa mahusiano kazini,fuateni ngazi nyingine ikiwa ni pamoja na kumjulisha katibu mkuu wa wizara husika,mtendaji mkuu wa idara ya serikali au asasi mnapofanyIa kazi.

    Kuna haja kubwa ya watendaji wakuu kulizingatia hili na kuwaheshimu watumishi wa kada za chini ili kuwe na uwiano baina ya majukumu ya ofsini na majukumu ya kijamii.[WORK-LIFE BALANCING].

    ReplyDelete
  22. Poleni sana masecretary kweli hilo ni tatizo sana na Mh Ghasia tunaomba uliangalie na kuwasaidia. Tatizo katika ofisi zetu za serikalini kuna swala la kuona kwamba kazi ya kutoa photocopy, kutype barua na kuandaa chai ni ya watu fulani na bosi hatakiwi kabisa kufanya hivyo. Na hii ndio inaleta tatizo hili, kama photocopier ipo, na printer ipo inakushinda nini wewe bosi kumuacha huyo secretary aende zake na uhangaike navyo mwenyewe muda huo wa usiku? Ndio maana mnakutana kwenye mikutano mikubwa wabosi wa serikalini hawajui hata kusoma email zao vizuri, they cant type a fast letter na hawako flexible. Utakaaje ofisini masaa sita bila hata kunyanyuka kidogo? yaani wakiamka ni kwenda chooni, maana chai wanaletewa, maji, chakula ni wao kunyayua simu tu! Hao secretaries wamegeuka vijakazi haswa.

    ReplyDelete
  23. hayo yaliyosemwwa hapo ni kweli kabisa! unakuta bosi mchana kutwa anzunguka tu wakati mwingine kwenye shughuli zake binafsi ikifika saa 11 jioni ndio anaanza kutoa kazi mpaka saa 3 usiku, hata ukitoka hajali kuwa unaendaje kila siku tunafika nyumbani saa 5 usiku hii ni haki kweli? Mhe. Ghasia tunaomba uangalie hili plse.

    ReplyDelete
  24. Mhe. H. Ghasia tunaomba usikie kilio cha masekretari, hatukatai kukaa mapaka usiku lkn kuwe na kazi za kufanya, tunakaa tu hakuna kazi basi tu umsubiri bosi aangalie TV Taarifa ya habari iishe ndio aondoke kisa kwake Pugu kuna foleni! kidogo chai, kidogo soda, kidogo mpigie fulani usiku saa 3!hii ni haki kweli? wanatufanya tusifanye kazi kwa moyo. wakati mwingine nachukua seek sheet ili nipumzike sio kwamba naumwa. kutoka usiku kila siku! natoka nyumbani saa 11:30 asubuhi narudi saa 5:30 usiku kila siku! nachokaaa

    ReplyDelete
  25. Jamani Masekretari tunavumilia sana! mimi huwa nakaa ofisini kumsubiri bosi hana hata kazi anaangalia taarifa ya habari kwenye Tv, Komedi na Music wakati mwingine anamtuma dereva wake amletee Wisky ananywea ofisini siku nikona anakunywa wisky namuaga mawili, akubali au akatae! akiamua anadraft barua atarekebisha mpaka ifike saa 4 anarudia yaleyele aliyofuta alimradi tu akukomoe ukapande daladala ufike saa 6 usiku nyummbani kwako. naomba mhe. Ghasia atusaidie kuweka mambo sawa tunanyanyasika kisa kada ya chini!

    ReplyDelete
  26. WE ACHA TU! NAMPA HONGERA HUYU ALIYETOA HII MADA! KWANI MASEKRETARI WENGI HAWAJUI HAKI ZAO WANAFIKIRI KUKAA OFISINI MPKA SAA ANAYOTAKA BOSI NDIO KAZI, MWELEZE UKWELI BOSI KAMA HAKUNA KAZI YEYE ANACHEZA KARATA KWENYE KOMPUTA WE ONDOKA!

    ReplyDelete
  27. pia ngazi za mishahara zitazamwe. Watu wapo wana miaka zaidi ya 25 kazini na wamefikia mwisho wa ngazi ya mishahara hakuna nyongeza. Fikiria mtu anapata mshahara huo huo kwa zaidi ya miaka 9 walioajiriwa jana wanamkuta!!! Mhe. Waziri, jamani kweli Utumishi unawajali watumishi walio chini ya wizara yao???? Ukisoma vitu vingine hawakubali kukubalisha kazi.

    ReplyDelete
  28. Eh Wajameni,

    Poleni sana ma PS. Hii inatokea pale mtu anapoamua kutomthamini binadamu mwenzake. Halafu mtu kama huyo anapofikiri kuwa hauna choice bali kumtumikia kwa lolote atakalosema basi ndiyo mambo yanakuwa kama hivyo.
    Ninakumbuka miaka mingi iliyopita nilifanya kazi kwenye kampuni binafsi, na mambo yao yalikuwa hivyo hivyo. Bosi alikuwa anapiga porojo na kazi zinatolewa saa kumi na nusu, na zinahitajika kesho yake asubuhi. Kuondoka hapo ni saa tano na nusu usiku (uzuri alikuwa ananipeleka mpaka nyumbani).
    Wakati ukafika nikachoka nikasema liwalo na liwe; saa kumi na nusu bosi anataka kuleta kazi nikamuaga kuwa ninakwenda kanisani. Hakuamini ujasiri niliokuwa nao. Na walikuwa wananitegemea sana Nilikuwa ninajua kiingereza sana na kazi yangu haikuwa na makosa. Baada ya hapo mambo yalibadilika sana. Mshahara na heshima vilipanda sana. (Hii ni miaka 14 iliyopita).

    Kila mtu ana mazingira yake tofauti. Kutegemea na mazingira yako ninatoa ushauri ikiwezekana umueleze bosi kama yeye anapata muda kutoa kazi usiku, unaweza kumuambia akutayarishie kazi usiku halafu wewe uifanye asubuhi. Usikatae kazi, ila ushauri arrangement tofauti ya kazi. Usiwe na hofu, hofu yako inampa nguvu kukunyanyasa.
    Usisahau kumkabidhi Mungu kila unachofanya. Mithali 3:6

    by Kana Ka Nsungu

    ReplyDelete
  29. Secretary oyee, tafuteni kozi nyingine muwakimbie hamuoni walimu siku hizi nani anataka ujinga, mtu akipata nafasi ya kwenda chuo kikuu anachomoka zake na mshahara anawaachia hesabu mbele kwa mbele. Tatizo hamtaki kujiendeleza na kufikiria ajira nyingine. fanyeni hivyo muone kama hawa mabosi wawatashika adabu zao. Wakina mama someni jamani, jiendelezeni la sivyo mtabaki kunyanyaswa tu na hakuna atakayeleta mabadiliko ni nyie wenyewe kuchukua hatua. Mimi nilisomea usekretari Magogoni, na sasa nina shahada ya uzamili na nina kazi nzuri tu. Someni wadada!

    ReplyDelete
  30. Mie bosi wangu anaangalia mpira kwenye web site hata kuchana karatasi moja ndogo aliyokuwa anandika na kuikosea hawezi uje umchanie kweli kama watumwa.

    Jamani kile chama cha masekretari kiangaliwe upya na kiundiwe muundo mpya viongozi wapya wa kutetea haki zetu wachaguliwe na kuwe na mabadiliko. Tuwe serious na sio makongamano tu kwenda kuuza sura tunajiponza na kujishusha wenyewe, kongamano la mwisho sijaenda ila nilishukuru sikwenda nasikia masecretary vurugu mtindo mmoja kugombea vijizawadi - hapa si ndo tunazidi kujishusha na kuonekana hamnazo!!

    Michuzi hebu tutengenezee/tushauri au post hili swala zima kwenye website special ya masecretary.

    ReplyDelete
  31. Mimi nimeunga mkono mambo mengine na mengine hapana.
    Kweli tunasikitika kuwekwa ofisini mpaka usiku na hujui unarudi namna gani nyumbani, pili boss anaweza kuwa kwenye kikao anasema husiondoke mpaka wamalize kikao, sawa hatukatai lakini na sisi mtuangalie maana yeye akitoka huko mfuko umetuna, mimi naambiwa kwaheri tutaonana kesho imetoka hiyo. Mama Hawa naomba utuandikie waraka ambao utatulinda sisi kwa muda wa kutoka kazini, angalau na sisi tuweze kuonana na familia zetu, na hata kama sina familia na mimi nataka nifaangaike niweze kupata nauli ya kujia kazini na mambo mengine

    ReplyDelete
  32. Naomba tusifanywe kama watumwa wa aina fulani tuonekane na sisi tuna familia. Na kimaslai pia tuangaliwe siyo tungojee kubana fedha ya chai au ya vikao

    ReplyDelete
  33. jamani kwa anaejua e-mail, ya Mh. Hawa ghasia, mtumieni hii. Ma-PS mlioko UTUMISHI kuna baadhi yenu matatizo haya yanawapata mfikishieni tafadhali. tumechoka.

    ReplyDelete
  34. hiyo ni kweli kabisa, bosi wakati wa muda wa kazi yeye ni kuzurura tu ila ikifika saa 11 jioni ndo anaanza kudrafti barua.

    ReplyDelete
  35. mdau aliyesema tuweke vikao na Maafisa Raslimali watu, naona hujui kinachoendelea, hao ndo wanaoongoza kwa kuwaweka maPS wao hadi usiku

    ReplyDelete
  36. "migogoro na migongano ya kazini ni ukosefu wa nidhamu, viongozi pia wajibu wenu mkubwa ni kulinda heshima na kudumisha nidhamu ya kazi." Huu ni wimbo wa mwaka 47, wakati huo hata nyimbo za kushitua wafanyakazi waka kada zote makazini zilikuwepo. Ushauri wangu, ni kwamba zifanyike semina za mara kwa mara maofisini kwa ajili ya kuelimishana nidhamu makazini ikiwamo kuheshimiana, pia kimaslahi kwa wakubwa kwa wadogo makazini.Semina ya MAADILI. Lakini unakuta mtu amejifunza maadili hayo alipokuwa chuoni akishaanza kazi anasahau kabisaaa anafanya tu makusudi kunyanyasa wenzake. Isichukuliwe eti kwa sababu mtu ana cheo kidogo ndio anyanyaswe hapana kila mfanyakazi ana haki zake za msingi za kibinadamu. Kikubwa ndugu zangu maps poleni sana hapa mapungufu ya kimaadili yanachangia sana naona huu utandandawazi. Fanyeni mpango wa kukumbushana hizo semina za mara kwa mara za maadili kukumbushana na sheria za kazi, zisisomwe tu vyuoni hata makazini ziendlezwe! Mtaongea mengi wahimizeni tapsea hao wawafanyie sheria za kuwalinda nyinyi mps.

    ReplyDelete
  37. Poleni sana Ma-PS, hawa mabosi nawashangaa sana, anakupa kazi za binafsi labda pengine dissertation ya kurasa 150 ya rafiki yake unaipiga chapana huambulii chochote mwisho ukishamaliza anakupa asante. Hii asante wakati umekunja mgongo kurasa zote hizo na haihusiani na kazi yako, yeye hapo amelipwa milioni 10 za kuandika na kufanya utafiti wa dissertation yake lakini anakuuliza kila siku na kukusisitiza kwa ni hujamaliza hata siku ya wikiendi unachapa kazi hiyo isiyokupa malipo yoyote ya ziada, vyuo vikuu ndio tabia zao, mabosi hawa kwa kweli hawaeleweki, ukidai kulipwa nako wanapunguza masaa uliyoyafanyia kazi. Wengine wanadiriki hata kukuletea adabu mbaya. Tuache kuwaogopa hawa wakuu wetu ukweli ukimweleza bila woga mbona hataweza kukuweka kazini hadi hiyo usiku. Mimi sikubali aniweke hadi usiku halafu usafiri nikatafute daladala wakati yeye anausafiri wa Serikali, sikubali vinginevyo kesho yake na siku zijazo nitakuwa namuaga muda wa saa za kazi zilizopangwa ikifika natoka bila woga. Tuchachamae tuwaeleze ukweli bila woga. Mwingine hata E-mail anakuambia umprintie kwa sababu sijui hawezi au vipi, ikija katika malipo hawakujui. Wakati umefika wa kusema sheria zirejeshwe. Mh. Mama Hawa Ghasia usifumbie macho tatizo hili litolee neno zito la kueleweka imetosha kwa yanayotendeka.

    ReplyDelete
  38. HIYO INAELEWEKA SANA KWAMBA NI MOJA YA KAZI YAKO MFANYAKAZI YOYOTE KUMTII BOSS WAKO LAKINI SI KWA KUPITILIZA INAWEZA IKATOKEA UTUMWA,KUNA MABOSS WAZURI NA WABAYA LAKINI KUNA MA PS WABAYA NA AZURI, MA PS WENGI WANAONA RAHA SANA KUTEMBEA NA MABOSS WAO ILI MAISHA YAO YAWE MEPESI KUMBE NDIO WANAJIPA UGUMU WA MAISHA,NA UJUE MAPENZI KAZINI NI KARAHA, KWANI AKIKUCHOKA KESHO ATALETA MWINGINE MBELE YAKO NA UKILALAMA ATAKUFUKUZISHA KAZI.BY FREE HARAKATI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...