Hatukujua asubuhi ile Mungu angekuita.
Katika maisha tulikupenda na katika kifo hivyo hivyo.
Tulivunjika moyo kukupoteza, hukwenda peke yako bali sehemu yetu ilikwenda pamoja nawe siku ile Mungu alipokuita nyumbani.
Umetuachia kumbukumbu nzuri, upendo wako ni muongozo wetu. Japo hatukuoni wakati wote uko pamoja nasi. Kiungo katika familia yetu kimevunjika, maisha yetu hayako sawa tena.
Lakini kadri Mungu atakavyotuita mmoja mmoja viungo vitaungana tena.
Unakumbukwa na Mume wako, watoto,
wajukuu, ndugu, jamaa na marafiki.
Kutakuwa na Misa ya Kumbukumbu siku ya Jumatano
tarehe 2 Novemba 2011 saa 11 jioni
tarehe 2 Novemba 2011 saa 11 jioni
katika makaburi ya KONDO ( Tegeta ), Dar es salaam
Nyote Mnakaribishwa
Mawasiliano simu namba
+255 754 434632/+255 656 238471
(Francesca Msafiri)
BWANA ALITOA, NA BWANA AMETWAA
JINA LAKE NA LIHIMIDIWE
AMINA



Poleni sana wapendwa. Tutaendelea kumkumbuka daima bibi yetu kwa ukarimu wake. Mungu ailaze pema poponi roho yake, pia awape nguvu na baraka wanafamilia.
ReplyDelete