Hatukujua asubuhi ile Mungu angekuita.
Katika maisha tulikupenda na katika kifo hivyo hivyo. 

Tulivunjika moyo kukupoteza, hukwenda peke yako bali sehemu yetu ilikwenda pamoja nawe siku ile Mungu alipokuita nyumbani.

Umetuachia kumbukumbu nzuri, upendo wako ni muongozo wetu. Japo hatukuoni wakati wote uko pamoja nasi. Kiungo katika familia yetu kimevunjika, maisha yetu hayako sawa tena. 
Lakini kadri Mungu atakavyotuita mmoja mmoja viungo vitaungana tena.

Unakumbukwa na Mume wako, watoto, 
wajukuu, ndugu, jamaa na marafiki.

Kutakuwa na Misa ya Kumbukumbu siku ya Jumatano 
tarehe 2 Novemba 2011 saa 11 jioni 
katika makaburi ya KONDO ( Tegeta ), Dar es salaam


Nyote Mnakaribishwa


Mawasiliano simu namba 
+255 754 434632/+255 656 238471
(Francesca Msafiri)

BWANA ALITOA,  NA BWANA AMETWAA
JINA LAKE NA LIHIMIDIWE
AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Poleni sana wapendwa. Tutaendelea kumkumbuka daima bibi yetu kwa ukarimu wake. Mungu ailaze pema poponi roho yake, pia awape nguvu na baraka wanafamilia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...