Makamo wa kwanza wa rais wa Zanzibar 
Maalim seif Sharif Hamad
Na Marzuok Khamis -Maelezo,Pemba.

Makamo wa kwanza wa rais wa Zanzibar Maalim seif Sharif Hamad amekitaka kikosi maalum cha kuzuia magendo ya karafuu cha Msuka, Mkoa wa Kaskazini Pemba kufanya kazi kwa mashirikiano zaidi ili kuhakikisha zao la Karafuu msimu huu halitoroshwi nje ya nchi kwa njia ya magendo.

Maalim seif ameeleza hayo leo huko Msuka alipokuwa akiendelea na ziara yake yakutembelea na kujionea shughuli mbali mbali za ununuzi wa zao hilo katika vituo ikiwa ni mfululizo wa ziara yake ya siku nne kisiwani Pemba.

Amesema zao la karafuu ni zao tegemezi kwa uchumi wa Zanzibar hivyo iwapo wajanja wachache watawaruhusu kulisafirisha zao hilo kwa njia ya magendo itakuwa ni hasara kubwa kwa taifa katika kuendeleza uchumi wake.

Hivyo amekisisitiza kikosi hicho kuhakikisha kuwa kinatekeleza wajibu wake ili kuhakikisha zao la karafuu msimu huu halitoroshwi hata kilo moja kwa njia ya magendo.
Amefahamisha kwamba msimu wa uchumaji uliopiata inadaiwa baadhi ya Askari wa vikosi vya SMZ wasiokuwa waaminifu wakishirikiana na raia katika kulitorosha zao hilo hivyo ametahadharisha kuwa msimu huu serikali iko macho na haitomvumilia mtu yeyote atakaebainika kujishirikisha na vitendo hivyo.

Mapema Makamu huyo wa kwanza ameipongeza hatua ya wananchi kwa kujitokeza kuuza kwa wingi karafuu zao katika vituo mbali mbali vya ununuzi wa karafuu.Vituo alivyovitembelea ni pamoja na kituo cha Finya, Chonga ,Wambaa,Mtambile na kikosi maalum chakuzuia magendo kilichoko Msuka Pemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. maalim kwa nini usiache tu raia wakauza karafuu watakako wao na kwenye maslahi kwao zaid,
    umesahau hotuba zako kabla hujaingia serikaliniiii!
    kwamba itakua ruksa mtu kuuza karafuu kokote anakotakaaa,
    sasa vipi tena maalim,mbona kigeugeuuuu!
    waache ndugu zetu wauze karafuu kwa maslahi zaidi wanakopenda.

    ReplyDelete
  2. mtoa maoni hapo juu,bei ya karafuu sasa hivi imepanda mpaka TSH.15000 kutoka 3000 kwa kilo na nis erikali ndio inayonunua,sasa wewe unahamasisha nchi yako kuhujumiwa?maana kuna wakati karafuu zilijaa kenya halafu huku kwetu zikaadimika kabisa wakati zinatoka huku,kama vile ambavyo sukari inatoroshwa huku wananchi wanataabika.magendo ni lazima yakomeshwe na ikitokea kuuza nje basi ufatwe utaratibu mzuri.maalim seif alisema wananchi wauze karafuu popote kipindi kile sababu bei ilikua ndogo.nadhani unatakiwa umpongeze kwa kushiriki vizuri kuijenga nchi.

    ReplyDelete
  3. sijui vyema mambo ya karafuu ila tu kutoka kwenye bei ya tsh.3000 adi tsh.15000 serikali inaitaji pongezi sana ata kma iyo bei imepanda ndani ya ya miaka 3 basi hawajachelewa kwli wanalengo la kuwakwamua wakulima basi na watanzania bara wawaongezee watu wa kusini kuhusu zao la korosho zenji oheeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  4. Mbona Rais wetu wa Tanganyika haongeagi kuhusu kilimo chetu cha kahawa,ndizi,maparachichi, mahindi, mchele, maharagwe n.k? Au hakunaga kilimo Tz sikuhizi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...